Tundu Lissu: Mkataba wa bandari ni suala nyeti sana

Kwa upande wangu niipongeze serikali ya mh Rais Samia kwa kumtafuta mbia kuiendesha bandari.Wazawa walikuwa wanaendesha kwa kufanya usimamizi ila wizi ulikithiri na mapato mengi yaliishia kwa walafi na mafisadi na kuifanya bandari ya Dar es salaam isiyo na ufanisi tena ikizidiwa na mombasa port wakati sisi kama nchi tunahudumia nchi nyingi kuliko Kenya.
Kongole kwa hatua hii ya kuwapa DP waiendeshe ili mapato yapatikane kwa manufaa ya nchi.
 
Weka ushabiki wa kivyama pembeni tumia akili Yako kutafakari hoja
 
Hapo tutegemee ajira za kidini, kina amii lazima waje kujaza nafasi za vijana wa taganywiker
 
Zito kumwamini ni kazi sana,
 
Tatizo Tanzania hatuna mahakama.

Kama marehemu angekuwa mzalendo wa kweli, kwanza angehakikisha nchi inakuwa na mahakama. Bahati mbaya yeye mwenyewe akashiriki kikamilifu kuua mahakama.

Kama huna mahakama zilzo huru, hiyo migogoro itapelekwa kwenye hii idara ya Rais? Marehemu mwenyewe alishindwa kuwashawishi Barrick kukubali migogoro kumalizwa nchini, Kabudi wake akaridhia migogoro yote kati ya Serikali na Barrick itamalizwa na mahakama ya Singapore, na haitaruhusuwa kukata rufaa.
 
Hivi hii sheria ya Magufuli sio kwenye madini tu? Sidhani kama ni mikataba yote.
Hata huko kwenye madini ilikwishafutwa. Ilikuwa kuwahadaa wajinga.

Mkataba wa Barrick na Serikali unatamka kuwa migogoro itaamliwa na mahakama ya Singapore, na hakuna kukata rufaa, na hata kukiwa na mgogoro, Serikali ni marufuku kusimamisha uzalishaji au exports.
 
Sio mkataba ule ni framework tu

Shida ni TPA juzi mkurugenzi wao kafanya interview; sasa badala ya kuwaita TBC pia.

Unaita vyombo uchwara vya online TV ambao awaoni umuhimu wa kuweka content yote; wao wanachagua visehemu wanavyodhani muhimu na kufupisha ili kupata views. Wanajua wakiweka kipindi cha zaidi ya lisaa bundle mgogoro so akitoangaliwa.

Inaonekana kuna maelezo mengi sana ya msingi ambayo yamekatwa kwenye kile kipindi cha bandari ndio ujinga wa kuita vyombo uchwara au kutowakumbusha waweke yote ili watu wasikie kila kitu alichosema.
 
Marehemu aliziua mahakama zote kwa kuwateua maafisa wa TISS kuwa majaji. Sasa hizo mahakama za kushughulia migogoro ya kimataifa zingetoka wapi?

Hata Barrick, tena wakati wa uhai wake, walilikataa hilo sharti, na Serikali ikaridhia migogoro yoyote ikaamliwe na mahakama ya Singapore.

Kama yeye mwenyewe aliyeianzisha hiyo sheria, aliidharau kwenye mkataba na Barrick, unategemea kweli hiyo sheria itakuja kufanya kazi?

Kama tunataka mahakama zetu zishughulikie migogoro ya mikataba ya kimataifa, kwanza tuunde mahakama huru yenye majaji wenye weledi na uadilifu siyo hawa wanaipewa amri na Rais.
 
Umeelewaa lakini au umecoment ili uonekane upo?

Kama una kumbu kumbu vizuri wakati Magufuli anaoambana na wazungu wa madini, Lissu alikua akiktahadharisha kwamba kinachotakiwa kufanyika kwanza Ni kubadili Sheria zetu ili kucomply na uvunjaji wa mikataba kwani tukivunja mikataba bila kufumua sheria zetu tushtakiwa!

Na kwa kumbukumbu sahihi Ni kwamba Sheria ilipelekwa Bungeni kwa hati ya dharura na haikuangalia mikataba yote isipokua madini tu!

Na ndicho kilichoikoa Tanzania kushtakiwa MIGA, na sio kuhamisha goli!

Laiti Kama angekua na utulivu Magufuli akaangalia Sheria za mikataba yote tysingekutana na haya ya Sasa.

Sasa kwa sababu mchakato huu wa bandari ulianza muda mrefu kimya kimya wakati mama anafanya ziara dubai, na kwa sababu sisi sio wa kuhoji Ni wapiga zumari tu, anachosema Tundu Lisu Ni kwamba mkataba unaooenda Bungeni Ni kwamba mkataba unaenda kulazimisha Bunge kubadili Sheria zetu ili kukidhi matakwa ya mkataba Jambo ambalo Ni hatari Sana!


Badala ya wewe kuungana na wazalendo na watu wenye mapenzi mema na nchi hii unaacha kupambana na adui halisi unahamisha goli unaaza kumshambulia mtu. Hatari sana
 
Sioni umuhimu ya vyuo vyetu mpaka kuendesha bandari wenye nchi kuona ufanisi ni kuomba mtu aje.
 
TPA hawezi kuuongelea mkataba Ni kihere here tu, ukiangalia parts zilisoaini HAKUNA mahala TPA ametajwa na Kuna uchambuzi umefanywa na mtaalamu mmoja kwenye huo mkataba, shughuli za TPA hazinajoneshwa kabisa huku kikatiba na kisheria TPA anatanbulika Kama msimamizi wa bandari zote!
Kiufupi tu Ni kwamba TPA ataondlolewa kwenye usimamizi wa bandari zetu pale Sheria mpya itakapotungwa ili kukidhi mahitaji ya mkataba!
Kwa TPA kusema Ni miezi au miaka kumi na mbili hawajui hata hicho kipengele Kiko wapi sababu mkataba haoneshi time Frame
 
Soma article 16 TPA ndio inatoa mwongozo sehemu gani za kuwekeza na kusimamia ‘project activities’.

Soma article 3 (2) kutakuwa na kamati ya pande mbili inayopanga sehemu za kuwekeza na phases. Kamati itakayokuwa inawasilisha mapendekezo kwa waziri wizarani.

Sasa unadhani kwenye hiyo kamati upande wa Tanzania itakuwa na hakina zaidi ya watu wa TPA na pengine wizara ya fedha.
 
Ndio kama magu aliweka taratibu kuwa migogoro ya maliasilia iamuliwe na mahakam zetu ,wao wanatak waende Africa ya kusini
 
Yeye anataka tuende Laindon kwenye mahakama zetu ili apate cha kuongea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…