Tundu Lissu na wenzake waachiwa kwa dhamana

Tundu Lissu na wenzake waachiwa kwa dhamana

Jeshi la Polisi mkoani Arusha limempatia dhamama Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu na viongozi wengine wa chama hicho waliokamatwa muda huu saa 2 usiku jijini Arusha.

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Elisa Mungure amesema viongozi hao wametakiwa kesho saa tatu asubuhi kuripoti polisi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo iliyotolewa leo Jumapili Septemba 10, 2023 ilisema kuwa Lissu na wenzake watatu walishikiliwa kwa tuhuma za kufanya mikusanyiko isiyo halali na kuzuia polisi kufanya kazi zao.

Mwandishi wa Habari kutoka Jambo TV, Oscar Kasubi aliyekuwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani humo naye ameachiwa usiku huu.

Arusha Zone

===

Pia soma:

Tundu Lissu akamatwa na Polisi akiwa Ngorongoro hotel Wilayani Karatu

Jeshi la Polisi: Tunamshikilia Tundu Lissu kwa kufanya mikusanyiko isiyo halali na kuzuia Polisi kufanya kazi yake

Mtu yupo hotelini chumbani kwake huo mkusanyiko ulikuaje!?mbona kama atawashinda mapema sana mahakamani,kwann hamkusubiria atoke nje!?

Kuna muda jeshi letu huwa silielewi
Kabisa!
 
Unatabiri kuwa kesho jua litawaka! Kukamatwa viongozi wa Chadema ni jambo la lazima kama ambavyo jua litawaka kesho.
Alitabiri 2022 na hata kabla Lissu hajarudi. Alafu yeye yuko Zimbabwe, sasa amfatilie Lisu wa nini? Ila alisema watakamatwa na wenzake.
 
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limempatia dhamama Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu na viongozi wengine wa chama hicho waliokamatwa muda huu saa 2 usiku jijini Arusha.

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Elisa Mungure amesema viongozi hao wametakiwa kesho saa tatu asubuhi kuripoti polisi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo iliyotolewa leo Jumapili Septemba 10, 2023 ilisema kuwa Lissu na wenzake watatu walishikiliwa kwa tuhuma za kufanya mikusanyiko isiyo halali na kuzuia polisi kufanya kazi zao.

Mwandishi wa Habari kutoka Jambo TV, Oscar Kasubi aliyekuwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani humo naye ameachiwa usiku huu.

Arusha Zone

===

Pia soma:

Tundu Lissu akamatwa na Polisi akiwa Ngorongoro hotel Wilayani Karatu

Jeshi la Polisi: Tunamshikilia Tundu Lissu kwa kufanya mikusanyiko isiyo halali na kuzuia Polisi kufanya kazi yake
Namuona lodi lofa hahahah Afadhali naona kakosa perdiem ya leo. Ila IGP anamhujumu sana Mama yetu Dkt Samia. Lisu amuache tu hana influence na siasa za bongo ni mtafuta huruma ya wafadhili anavyopiga kerere ndiyo anaongeza wafadhili wa ngo yake maana hana mshahara
 
Kumbe dhamana hata weekend unapata!? Police vueni gwanda mpande jukwaani Kama mnataka kuwa wanaSiasa
Hahahahahahaha yaani IGP anamuangusha sana Dkt Samia jamani. Ungekuwa wewe wangesema weekend ni dhamana
 
Yes watu wamejua pia kwamba jamaa hashauriki na hasikilizi mtu.

Yes watu wamejua kua viongozi waandamizi kitaifa wamejitenga nae.

Yes wamejua kua jamaa kawaambia waandamizi wenzie kwamba waeendelee tu na kazi zao binafsi yeye anaweza kupiga kazi bila msaada wala ushauri wao.
Kama ana amini anacho fanya ni sahihi aendelee kufanya tena kwa nguvu zote Wala hakuna shida
 
Risasa zilishindwa sembuse taaluma yake? [emoji16][emoji16]

Labda waliamua kumpotezea muda tu lakini eti nihofu Lisu kakamatwa hata mbwa wa polisi hawezi mng’ata Lissu.
Aibu ni kwa polisi na matamko yenye mihuri sijui huwa hafikirii na kujihoji kwanza kabla wamkate?
 
Faiza Foxy. Umeongea kinyume chake ukweli ni kuwa Tundu Lissu ana First Class Degree ya SHERIA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM. Ukumbuke Jason's SHULE ya vipaji MAALUM ILBORU.
Best Student Faculty of LAW.
Upo?
Huyo dada yupo wazi kichwani
 
Unafanyeje mikutano ya HADHARA bila ya kibali cha polisi ?!![emoji15][emoji15][emoji1787]

TL ni wakili wa aina gani ?!!!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Hakuna sheria inayowapa Polisi kutoa kibali cha Mikutano ya Kisiasa. Unless jeshi hilo ni sehemu ya Siasa. Bali Chama cha siasa kinatakiwa kuwapa taarifa tu ili kulinda usalama ambayo ndio kazi yao ya msingi kabisa. Siyo kuzuia mikutano ya kisiasa.
 
Akili za polisi wetu aibu sana,
Ni watu kama vijana wanaocheza singeli au mdundiko!
Siku zote wanatsfuta kiki za kijinga, yaani wana operate kama kuku asiye na kichwa!
Wiki hii vijana wa jwatz walipita maeneo mbali mbali wakichukua mabegi na nguo zenye kufanana na nguo zao, sasa kwa akili ndogo tu, kwa vile hizo nguo hazikutoka wala kuibiwa jeshini,ilibidi zichomwe moto! Sasa makenge Yale na umaskini wao utakuta yamezibeba yameenda kugawana!
Tatizo LA kuajiri vilaza failures wa form 4 div 4!
Mkuu tabia yako ta kutukana haifai na sisi waungwana hatukuungi mkono.

Unaweza kutoa maoni yako bila kutoa matusi na kauli za kukashifunwengine.
 
Back
Top Bottom