Tundu Lissu ni mjanja sana. Tafadhali msimguse. Mwache ashindwe au ashinde kwa haki

Tundu Lissu ni mjanja sana. Tafadhali msimguse. Mwache ashindwe au ashinde kwa haki

Rasterman

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2015
Posts
33,856
Reaction score
44,204
Niwajulishe tu wenzangu na mimi kuhusu Lissu na namna ninavyoweza kumchukulia. Iko wazi kuwa Tundu Lissu ni kijana/Mzee mwenye uwezo mkubwa kiakili. Hili linaweza kuthibitishwa na watu wanaofanya nae kazi na hata sisi watu wa siasa. Huko kwenye taaluma yake mambo ya haki, sheria na wajibu ndio kabisaa! Ni nondo huyu jamaa.

Sasa kuna ka-kauli amekuwa akikaongelea sana toka alipoanza maandalizi ya kuja nyumbani kutoka Ubelgiji kwenye matibabu yake. Nako ni haka. 'mimi sina ulinzi binafsi wala chama changu hakina ulinzi wa kunihakikishia usalama wangu, ni serikali na polisi vyenye wajibu wa kisheria kunilinda na kulinda usalama wa mali na raia wake"

Hii kauli ameiongea zaidi ya mara kumi au kumi na tano kila anapopata fursa ya kuongea na vyombo vya habari vya ndani au nje ya nchi.

Wataalam wa mambo ya usalama na ulinzi mtakubaliana na mimi kuwa hatusikilizi kile anachosema na kuonesha wazi (an eye to see not the revealed but what is hidden).

Mnavyomjua Lissu na tishio alilokuwa nalo la usalama wake huku akiwa ndiye mpinzani anayeogopwa hawezi kuwa mjinga kiasi hicho akaingia nchini kichwa kichwa.

Please washikaji mnaotaka ujiko kwa kumsumbua sumbua kwa njia mnazojua nyie nawatahadharisha msije kusema hatukuwambia kitakacho wakuta mtajuta ninyi na familia zenu.

Mwacheni afanye siasa zake kama hazivunji sheria za nchi mpeni uwanja huru. Akishindwa kila mtu ataona. La akidhulumiwa wazi wazi mnamjua Yule ni Toto Tundu. Hatokubali. Mkidharua juu yenu. Mkiuchukua ushauri huu au mkauacha huu yenu pia

Nawatakia kikao chema Mlimani City. Watanzania tunatarajia Mgombea asiye na mashaka wala makandokando.

Aluta continua!✌✌✌
 
Mkuu ungepitia post yako tena mara nyingine kabla hujapost, ina typing error nyingi.

Ila hapo kwa Lissu tunamtakia kila la heri
 
Mkuu ungepitia post yako tena mara nyingine kabla hujapost, ina typing error nyingi.

Ila hapo kwa Lissu tunamtakia kila la heri
Nimesharekebisha mkuu. Asante kwa ushauri wako.
 
Na mgombea wa aina hiyo tutampata tu kutoka cdm na ni mh Lissu

photo%20266%2012-18-0.jpeg
 
Kwani lengo la attempt lilikuwa lipi na unajuaje kwamba kwa kilichotokea lengo halijatimia? Sio kila adui ni m'bora akiwa kafa
 
Back
Top Bottom