Tundu Lissu ni mjanja sana. Tafadhali msimguse. Mwache ashindwe au ashinde kwa haki

Tundu Lissu ni mjanja sana. Tafadhali msimguse. Mwache ashindwe au ashinde kwa haki

Niwajulishe tu wenzangu na mimi kuhusu Lissu na namna ninavyoweza kumchukulia. Iko wazi kuwa Tundu Lissu ni kijana/Mzee mwenye uwezo mkubwa kiakili. Hili linaweza kuthibitishwa na watu wanaofanya nae kazi na hata sisi watu wa siasa. Huko kwenye taaluma yake mambo ya haki, sheria na wajibu ndio kabisaa! Ni nondo huyu jamaa.

Sasa kuna ka-kauli amekuwa akikaongelea sana toka alipoanza maandalizi ya kuja nyumbani kutoka Ubelgiji kwenye matibabu yake. Nako ni haka. 'mimi sina ulinzi binafsi wala chama changu hakina ulinzi wa kunihakikishia usalama wangu, ni serikali na polisi vyenye wajibu wa kisheria kunilinda na kulinda usalama wa mali na raia wake"

Hii kauli ameiongea zaidi ya mara kumi au kumi na tano kila anapopata fursa ya kuongea na vyombo vya habari vya ndani au nje ya nchi.

Wataalam wa mambo ya usalama na ulinzi mtakubaliana na mimi kuwa hatusikilizi kile anachosema na kuonesha wazi (an eye to see not the revealed but what is hidden).

Mnavyomjua Lissu na tishio alilokuwa nalo la usalama wake huku akiwa ndiye mpinzani anayeogopwa hawezi kuwa mjinga kiasi hicho akaingia nchini kichwa kichwa.

Please washikaji mnaotaka ujiko kwa kumsumbua sumbua kwa njia mnazojua nyie nawatahadharisha msije kusema hatukuwambia kitakacho wakuta mtajuta ninyi na familia zenu.

Mwacheni afanye siasa zake kama hazivunji sheria za nchi mpeni uwanja huru. Akishindwa kila mtu ataona. La akidhulumiwa wazi wazi mnamjua Yule ni Toto Tundu. Hatokubali. Mkidharua juu yenu. Mkiuchukua ushauri huu au mkauacha huu yenu pia

Nawatakia kikao chema Mlimani City. Watanzania tunatarajia Mgombea asiye na mashaka wala makandokando.

Aluta continua!✌✌✌
Tundu Lissu hajawahi kuwa tishio kwa sakata lolote lile.
Sana sana ana kauli za kuudhi.
Hisia za wengi ni kuwa walio mkong'oli ni wale aliowaudhi.
Otherwise ana maneno makali kama moto wa karatasi ambao hauunguzi pori!
Na Tanzania ni pori kubwa!!
 
Tusimfanye Lissu akawa ana over right , ni raia kama raia wengine.

Kama amekuja kijasusi basi intelijensia ya nchi itamalizana nae. Ni swala la mda tu. Kinachombeba ni kwa kuwa TZ ni inchi ya watu wapenda Amani na hawapendi makando kando. Angekuwa nchi za wenzetu angekuwa anachezea mechi za mchangani.
Unachokituhumu kwa Lissu, ni vise versa kwa hao wanaojiona wazalendo zaidi
 
Ni kweli hatumpaishi lakini atendewe haki. Kama havunji sheria za nchi asisumbuliwe.

Mwanakulitafuta mwanakulipata. Atakayeshupaza shingo atajuta yeye na Familia yake.
Sheria gani zaidi ya wanaovunja katiba ya nchi ?!
 
Heri yako usie mlemavu . Mungu hajawahi kudhihakiwa .
Tunajadili criminality , haichagui mlemavu au mzima, akivunja sheria tupa kureeee!! haijalishi eti nami ntakuja kuwa mlemavu au la, kikubwa afuate sheria za nchi tu
 
Tunajadili criminality , haichagui mlemavu au mzima, akivunja sheria tupa kureeee!! haijalishi eti nami ntakuja kuwa mlemavu au la, kikubwa afuate sheria za nchi tu
Sheria zipi za kufuatwa. Hizi zinazovunjwa na watunga sheria ??!!
 
Mkuu ulichokuwa unafikiria nami nilishafikiria ila kwasababu sio mtu wa kuanzishaga thread jukwaa hili nilishindwa kuliweka hili jambo mapema humu.
Mtu aliyepitia situation ya mh Lissu so rahisi kwake kurudi katika mazingira yaleyale yaliyotaka kuondoa uhai wake hapo kabla labda awe amethibitisha uwezekano wa kuwepo salama na hata ikitokea maisha yake yakakatishwa basi huko nyuma kuna jambo kubwa litatokea kwa sababu ya kifo chake.
A brilian guy has been all this time preparing for the coming situation which is general election, sasa mtu amguse...
Yetu macho na masikio
 
Mkuu ungepitia post yako tena mara nyingine kabla hujapost, ina typing error nyingi.

Ila hapo kwa Lissu tunamtakia kila la heri
Content umeielewa au umefanya kazi ya kupitia typing error pekee ?
 
Mkuu ulichokuwa unafikiria nami nilishafikiria ila kwasababu sio mtu wa kuanzishaga thread jukwaa hili nilishindwa kuliweka hili jambo mapema humu.
Mtu aliyepitia situation ya mh Lissu so rahisi kwake kurudi katika mazingira yaleyale yaliyotaka kuondoa uhai wake hapo kabla labda awe amethibitisha uwezekano wa kuwepo usalama na hata ikitokea maisha yake yakakatishwa basi huko nyuma kuna jambo kubwa litatokea kwa sababu ya kifo chake.
A brilian guy has been all this time preparing for the coming situation which is general election, sasa mtu amguse...
Yetu macho na masikio
 
Back
Top Bottom