Tundu Lissu: Nitakwenda Chato, nitamwambia Magufuli amka uone Rais Samia anavyofanya

Tundu Lissu: Nitakwenda Chato, nitamwambia Magufuli amka uone Rais Samia anavyofanya

Jamaa huyu kiboko, kama siasa zenyewe ndio hizo bora tuendelee kushabikia mipira tu, siasa za kutukana viongozi?
 
Huyu si alikuwa anabeza watu kuaga mwili
Akasema marehemu anazungushwa sana nk ujinga.

Hakujua kama kutakuwa Kuna kumkumbula,na hataonekana tena kwenye sura ya Dunia.

Sasa naye ameshamkumbuka kama sisi tu team Dikteta.
Mbona wakina Nape wa CCM na Kinana walimtukana Magu na Kinana kwa sasa ni Kaimu mwenyekiti? Lisu point yake iko kwenye kugawa bure mali za Umma
 
"Nilihapa sitafanya mkutano Chato ila nitakwenda hata waweke mapolisi nitakwenda Chato, nitakwenda kumuasha Magufuli amka Magufuli amka uone wanavyofanya" Tundu Lissu

"Magufuli hakuiba tusimsingizie wala hakusaini huo mkataba, Magufuli mnajua mambo yake hakuwahi kuiba" Tundu Lissu

"Umewahi kuona wapi CCM wanazunguka nchi nzima kutetea Mkataba wa bandari,kuna nini,kuna maslahi yapi ya ziada,wameacha ilani yao Wameamua wafe na Mwenyekiti wao" Tundu Lissu

"Nani kama Mama,mama gani anauza Mali za familia,Mama gani anagawa cha kwetu kwa watu tusiowajua,Mama gani anakula chakula cha watoto wake" Tundu Lissu

"Kama ni mwizi tutamuita mwizi,amegawa bandari zetu kwa waarabu,atuambie manufaa ya huu mkataba yako wapi kwenye mkataba sio kupiga maneno na hayapo kwenye mkataba " Tundu Lissu

View attachment 2701509
hajamlilia magufuli, this is a wrong interpretation. naweka msikilize...

 
Hii movement natambua fika ni game linachezwa kwa wanasiasa fulani kuungana dhidi magenge fulani yanayotaka kujimilikisha nchi.
Good move!!
 
-Moja ya Sifa kubwa ya inabii ni kwamba atimizae unabii anakua hajijua kua anatimiza neno fulani, angalia Petro aliambiwana Yesu kua atamkana, lkn Petro akabisha ila siku alipomkana baada ya hilo kufanyika ndipo akakumbuka kua Yesu alisema, basi akaanza kulia.

Angalia Tena Yesu alisema kua mmoja kati ya wanafunzi wake atamsaliti, basi Yuda akabisha kwa hasira sana hata kusema ataefanya hilo hatomuacha, lkn huyohuyo Yuda akawa msaliti namba moja, akamuuza Yesu na baada ya kumuuza ndo akagutuka na kukumbuka kua Yesu alishawai kusema na akagundua kua ametenda kosa, akalia na kwenda kujinyonga, angalia tena, Yohana baada ya kutimiza unabii na kumbatiza Yesu basi Yohana akafifia.

-Kwahyo tukija kwa lissu, ni kwamba lissu anatimiza unabii na neno la magufuli la kwamba mtanikumbuka bila kujijua. Yeye lissu anaweza kudhani kua kufanya hivyo kutampatia umaarufu na kukubalika Kama vile Yuda alivyodhani kua kumuuza Yesu kutamtajirisha, lakin ukweli ni kwamba baada ya lissu kutimiza unabii huo ni kwamba neno la mtanikumbuka linakwenda kutimia na lissu anakwenda kufifia maana alimfanyia mabaya sana Nabii Magufuli. Yani hivi navyoongea ni kwamba lissu hajui anenayo maana ameingiwa na roho wa Mungu ili kumshurutisha kutimiza neno la Nabii John, ila baada ya kutimiza hilo atagutuka na atapigwa na barafu na roho wa Mungu, na atakua mpole na huwenda akawa mchungaji ili kuishi kujutia hila alizozifnya kwa malaika John.

- Ni nani nchi hii, Ni mtu gani nchi hii alietamani kua MALAIKA huko mbinguni Kama sio Magufuli? Ni kwanini ni Yeye tu ndio alikua rais pekee ktk nchi hii aliekua akijikonect/ kujihusisha na habari za mbinguni? Ni rais pekee aliemtaja sana Mungu wa mbinguni tangu kuumbwa kwa nchi hii, Ni rais pekee aliesema anatenda mema ili siku akifa akapewe cheo cha MALAIKA MKUU huko mbinguni, ni kipindi chake tu ambapo Mungu alitajwa sana ktk historia ya nchi hii, Ni kipindi chake ndipo matatizo ya kisayansi Kama Corona yalipotatuliwa kwa neno la Mungu, alitia moyo maskini, na alijitoa sadaka kwa kauli zake na matendo yake.

Kiufupi alifanya matendo yote ya kinabii na mambo ya mbinguni, ishara zote zilikua wazi. Hivyo nikasema kua alikua MALAIKA ila sisi hatukutambua ntakosea? Nakoseaje akati hata huko Sodoma malaika walienda kwa rutu lkn watu wa mji ule walijua ni watu tu?

-Kiufupi Magufuli hakua kiumbe wa dunia hii na kwa ishara na maneno yake alijionesha Ila kwakua sisi ni vilaza Basi hatukufunguliwa.
-Sasa niwaambie tu kua wale wooote mlieshindana nae kwa hira basi muungane na lissu kwenda chato kuhiji, hata neno lenyewe alilotamka lissu la kuhiji si neno la kawaida, Ni neno la Kimungumungu. Mwende ili nchi ipate amani
 
Back
Top Bottom