Tundu Lissu: Nitakwenda Chato, nitamwambia Magufuli amka uone Rais Samia anavyofanya

Tundu Lissu: Nitakwenda Chato, nitamwambia Magufuli amka uone Rais Samia anavyofanya

"Nilihapa sitafanya mkutano Chato ila nitakwenda hata waweke mapolisi nitakwenda Chato, nitakwenda kumuasha Magufuli amka Magufuli amka uone wanavyofanya" Tundu Lissu

"Magufuli hakuiba tusimsingizie wala hakusaini huo mkataba, Magufuli mnajua mambo yake hakuwahi kuiba" Tundu Lissu

"Umewahi kuona wapi CCM wanazunguka nchi nzima kutetea Mkataba wa bandari,kuna nini,kuna maslahi yapi ya ziada,wameacha ilani yao Wameamua wafe na Mwenyekiti wao" Tundu Lissu

"Nani kama Mama,mama gani anauza Mali za familia,Mama gani anagawa cha kwetu kwa watu tusiowajua,Mama gani anakula chakula cha watoto wake" Tundu Lissu

"Kama ni mwizi tutamuita mwizi,amegawa bandari zetu kwa waarabu,atuambie manufaa ya huu mkataba yako wapi kwenye mkataba sio kupiga maneno na hayapo kwenye mkataba " Tundu Lissu

View attachment 2701509
Huyu jamaa yenu ana ule ugonjwa wa kutenda kwanza halafu baadaye ndiyo anafikiria kwamba alikosea. Hata Mhe. Rais Samia atakuja kumlilia kesho. Lissu hana nidhamu ya ubongo na ulimi; ndiyo maana alidiriki hadi kumtukana Mwalimu ambaye ni Baba wa Taifa, mwanamamujumui makini wa Afrika, mwanazuoni na mtu anayeheshimiwa duniani, ikabidi Mzee Mtei aombe radhi. Dk. Magufuli alimtukanaa weweee....! #Lissu hatabiriki akili zake 🙏🙏🙏
 
Kwenye siasa sijui kuna nini. Mwanasiasa haeleweki.

Ukifuata upepo hutaelewa. Lisu amekuwa wazi kwa mambo aliyompinga Magufuli. Good governance.

Rule of law, demokrasia . CCM kilishindwa kumuunga mkono Magu, akahujumiwa hadi kifo chake.
 
We kilaza sijui unamuelewa lisu? Point yake iko kwenye kugawa bure mali za nchi basi, kuna seheme Lisu aliwahi tamka Magu ni mwizi? Point yake iko hapo
Unamuelewesha Lissu au mwanzisha thread?
 
"Nilihapa sitafanya mkutano Chato ila nitakwenda hata waweke mapolisi nitakwenda Chato, nitakwenda kumuasha Magufuli amka Magufuli amka uone wanavyofanya...

Hizi ni kavukavu, hakuna kulemba tena.

Sioni maana ya kufumbafumba maneno; kufanya hivyo ndiyo jadi ya CCM, na hasa huyo mwenyekiti wao.

Kufumbafumba maneno CCM wanakupenda sana, kwa sababu wanao ujuzi wa kufanya hivyo, wakiendelea kuwazubaisha wananchi wasielewe kinachoendelea.

Kufumbafumba maneno ni kuchanganya akili za wananchi wasielewe uhalisia wa kinachoendelea.

Samia ni fundi mkubwa katika fani hiyo; lakini taratibu watu wameanza kuelewa hadaa nyingi anazozitumia.
 
wewe hujamwelewa Lisu. Lisu is very objective, ukweli anausema kama ulivyo na uongo anausema kama ulivyo. Mimi Magufuli nilikuwa namuunga mkono at the beggining...
Hata mm Sina chama chochote!!!

Hata Mimi sikupenda matumizi makubwa kupinga wakosoaji,

Bt alikuwa na Nia njema kulipeleka Taifa Mahali pazuri.

Lissu kama anaweza kutimiza Maono ya Magu, aungwe mkono maana ni jasiri na mkweli.
 
Pumbavu kabisa huyu. Yeye si ndiye alikuwa anamtukana na kumuita kila aina ya maneno. Sasa ameona hana tija wala kukubalika kwenye jamii anajitafutizia kiki kupitia JPM.
Shetani anaachaje kutukanwa?
 
wewe hujamwelewa Lisu. Lisu is very objective, ukweli anausema kama ulivyo na uongo anausema kama ulivyo. Mimi Magufuli nilikuwa namuunga mkono at the beggining ....
Same to me, dhalimu kwangu amegoma kuniingia kabisa. Hata hizi sifa za Lissu namuona hana maana kabisa.
 
Mwehu tu huyo hana jipya.

Akitoka hapo aende na kwa nyerere.

Wote hao ameshawatukana.
Kama kuna mwehu kumzidi Lissu, huyo atakuwa siyo mwingine bali 'FaizaFox'
Huyu hana mfano zaidi yake katika uwehu.
Ushahidi upo humu JF, kwa hiyo hapa hasingiziwi kuhusu uwehu wake.

Hata hiyo mistari michache tu aliyoandika hapo inadhihirisha uwehu alionao.
 
Niliwambia zamani CHADEMA

Kumtukana Magu live jukwaani ni LAZIMA uwe umelewa kama kamanda Fulani pale furahisha.

Magufuli aliipenda Nchi hii na alikuwa MZALENDO 🇹🇿 🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿

Lissu kwann hukumkubali Akali akiwa hai🙏🙏🙏🙏????

Nenda Chato ukatubu, ingawa TOBA yako Si Rahisi kusikika sababu Nabii Magu, hayupo kaburini,

Yuko Mbinguni.

Mungu ibariki TANZANIA.

Amen.


..Lissu alisema Magufuli alijaribu kumuua.
 
Back
Top Bottom