Tundu Lissu: Nitakwenda Chato, nitamwambia Magufuli amka uone Rais Samia anavyofanya

Tundu Lissu: Nitakwenda Chato, nitamwambia Magufuli amka uone Rais Samia anavyofanya

Mhe Tundu Lissu awataka watanzania kujiuliza Rais mpaka kasaini Mkataba wa DP Word amepewa kiasi gani mpaka awauze watanzania bila kuonyesha bei.


#+255KatibaMpya #OkoaBandariZetu
 

Attachments

  • VID-20230729-WA0176.mp4
    17.9 MB
"Nilihapa sitafanya mkutano Chato ila nitakwenda hata waweke mapolisi nitakwenda Chato, nitakwenda kumuasha Magufuli amka Magufuli amka uone wanavyofanya.

"Magufuli hakuiba tusimsingizie wala hakusaini huo mkataba, Magufuli mnajua mambo yake hakuwahi kuiba.

"Umewahi kuona wapi CCM wanazunguka nchi nzima kutetea Mkataba wa bandari, kuna nini, kuna maslahi yapi ya ziada, wameacha ilani yao wameamua wafe na Mwenyekiti wao!

"Nani kama Mama, Mama gani anauza mali za familia? Mama gani anagawa cha kwetu kwa watu tusiowajua? Mama gani anakula chakula cha watoto wake?

"Kama ni mwizi tutamuita mwizi, amegawa bandari zetu kwa Waarabu, atuambie manufaa ya huu mkataba yako wapi kwenye mkataba sio kupiga maneno na hayapo kwenye mkataba."

View attachment 2701509
Pia soma: Tundu Lissu: Hakuna Rais kwenye nchi hii amewahi kutufanyia kitu mbaya kama Rais Samia
Retired unakumbuka nilisema mwaka 2025 kete ni JPM. CC Erythrocyte umeuona ukweli JPM hakuiba si maneno yangu ni testmony ya Boss wako
 
Back
Top Bottom