Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Rais Magufuli alitoa rushwa Kibiti Mil. 5 na akanunua jogoo laki moja wakati kashapitishwa kugombea Urais. Nitamuwekea pingamizi

LOPOLOPO anaforce king ili atandikwe aanze kulia lia kwa mabeberu si mnaona mnaona wamenichapa tena.hizo strategy za chama chake maana ndio waliomvunja mguu...
Chama chake wamemsokomeza akaongee pumba kwenye mkutano wa chama cha wenzao , ha ha kweli ccm baba lao.
 
NEC. hawatampatia fomu maana ana kesi za kujibu lakini pia ana zuio la maadili ya utumishi wa umma. Lakini ningeshauri wampe.
hujwahi kusikia kuwa hata uoge vipi mjini huendi sasa ndo itakavyokuwa kwenye uchaguzi hata iweje ccm watashinda tu...nape yukowapi kwan sikuhizi mtaalamu wa bao la mkono..lamsingi tuwape muda hakuna marefu yasiyo na ncha
 
Bila kumkosea mtu heshima ila Kina Kinana wanahitajika kurudi kuiongoza CCM, Kina Bashiru PolePole na wenzao hoja kwa hoja hawamuwezi huyu Tundu Lissu. Pia sijui kama wana vifua vya kuvumilia mashambulizi ya TL. Kumbuka kazi ya Uchambuzi wa Miradi na Uchumi ishafanywa na ZZK Lissu hana haja ya kutumbia yeye ni atack atack atack.
Naanza kuelewa kwa nini walimnyeshea mvua ya risasi.

Na hii miaka 5 wasingefungia mikutano ya hadhara kijani hali ingekuwa tete mnoo.

Unforgetable
 
Kwani kampeni zimeshaanza? Nyinyi kwenye vichwa vyenu ni zero brain! chochote anachosema Msaliti Lissu mnaingia kichwa kichwa tu.

Hajawahi kusimama kampeni. Huhitaji elimu kubwa kujua dhamira ya muamala ule.
 
Kama huwezi tenganisha hayo, mkuu nakushauri achana na hii mada.
Jibu hoja,unamtenganisha wakati gani? Anamjibu raia aliyeuliza kuhusu stand anaanza kuponda chaguo la wananchi la mbunge wao kwakuwa anatoka upinzani? Hata aliyemuuzia jogoo amevaa sare ya chama cha Magufuli.
 
Lissu sio mahakamani ni mkutano wa kuchagua mwakilishi wa Chadema. Acha kutoka kwenye mstari, kazi yako ni kuwashawishi wajumbe kuwa wewe ndio bora kuliko wale wengine kugombea Uraisi kwa tiketi ya chadema.

Subiri kwanza uchukuwe form ya NEC uone kama umewekewa ka uzibe ndipo mabomu yako ya atomic huyafyatue ikibidi mbele ya safari.
 
Ukishaleta katiba mpya maana yake umeleta maji, shule,barabara na maisha Bora kwa kila mtu.tumekosa maisha Bora kutokana na kuongozwa na viongozi wabovu Kama akina Magu,makonda,mtungi,Ndugai and the like though we have everything.Na katiba na inatoa fursa ya hawa vilaza kuendelea kutudumaza
 
Jogoo hoyeee! Lakini ile shilingi laki moja aliyopewa yule mwenye jogoo wa kwenda kwa mama mzazi hadharani imeshaleta hoja ya mapingamizi sasa.
 
Kumuwekea pingamizi ni kupoteza muda. Unamweeaje pingamizi mgombea ambaye unajua utamshinda? Kumwekea pingamizi ni kumuonea!
 
Endeleeni tu na ujinga wenu. Tunakusanya ushahidi wote mwaka huu. Mawakili wa Amsterdam hawako mbali sana na mahakama ya ICC. Lolote mtakalofanya mwaka huu mjue tu mwisho wenu ni aibu tu .
Kuna mama mmoja alishangilia kauli ya kuuawa kwa Zito huko bungeni. Sijui mama huyu yuko wapi siku hizi? Usimtakie binadamu mwenzio kifo bila muumba kutaka. Utatangulia wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…