Tundu Lissu: Rais Samia ameuza bandari zetu zote zilizopo na zitakazokuwepo

Tundu Lissu: Rais Samia ameuza bandari zetu zote zilizopo na zitakazokuwepo

Hujui tofauti ya IGA na hga,hujui pia tofauti ya contract na agreement...hakuna anayekuchanganya,ni umbumbumbu wako tu
Huna kitu aisee.
Unataka kulazimisha kuendeleza upotoshaji wa jambo ambalo tayari watu wamekwisha lielewa muda kitambo.

Hata uchanganye hayo maneno vipi, ukweli utabaki ule ule kwamba huwezi kuvitenganisha yaliyomo kwenye IGA (Agreement), na mikataba (contract) zitakazotokana na makubaliano hayo. IGA ndiyo basis ' ya hiyo mikataba itakayofuata.
Ubovu katika IGA unazaa ubovu zaidi kwenye 'contracts'.

Kama nchi ina katiba mbovu, itazaa sheria mbovu zinazotokana na katiba hiyo.
 
Huna kitu aisee.
Unataka kulazimisha kuendeleza upotoshaji wa jambo ambalo tayari watu wamekwisha lielewa muda kitambo.

Hata uchanganye hayo maneno vipi, ukweli utabaki ule ule kwamba huwezi kuvitenganisha yaliyomo kwenye IGA (Agreement), na mikataba (contract) zitakazotokana na makubaliano hayo. IGA ndiyo basis ' ya hiyo mikataba itakayofuata.
Ubovu katika IGA unazaa ubovu zaidi kwenye 'contracts'.

Kama nchi ina katiba mbovu, itazaa sheria mbovu zinazotokana na katiba hiyo.
Hapo umemaanisha IGA ni hga
 
Na kalamu Maria Sarungi-Tsehai

Port of Dar - TPA and Benki ya Dunia
Nawarudisha mwaka 2017/18 Benki ya Dunia ilikubali na kuingia mkataba wa mkopo wa maendeleo na serikali wa kuimarisha Bandari ya Dar es Salaam chini ya mradi unaoitwa Dar es Salaam Maritime Gateway Project ambapo dola za kimarekani (USD) milioni 400 ilitolewa kuimarisha miundombunu halisi (phyiscal) na dola milioni 21 kwa ajili ya kuimarisha taasisi na kusaidia kutekeleza mradi Mamlaka ya kutekeleza mradi huu ni TPA - pesa ilienda huko Mradi unaisha 30 June 2024 (mwakani) Kwa kifupi sisi wananchi tutalipa deni hili sehemu kubwa ya milioni 421 iliyotolewa na Benki ya Dunia na kuwekezwa ktk kuimarisha bandari Sasa tuchambue ripoti nini kimefanyika, na kwa nini DP World imetajwa katika ripoti hii?
Katika muhtasari wa Dar es Salaam Maritime Gateway Project report iliyotolewa February 2023 (mwaka huu) inaonyesha kuwa utekelezaji umezidi kuzorota na RISK ya mradi umeongezeka na kuwa SUBSTANTIAL yaani kuna hatari mradi kutotimiza malengo Inaelezwa kuwa mradi huu ulioidhinishwa 2017 na kuanza kutekelezwa 2018 ina mikataba 7 ikiwemo mashirika 5 ya consulting. Utekelezaji bado siyo mzuri na lengo la kuONGEZA UFANISI wa ports and terminals zote zinazoendeshwa na TPA, na kuijengea uwezo kuwa MENEJA na DEVELOPER (mwendelezaji) wa ports zingine huku ikiendelea kutathmini uwekezaji binafsi (tulikuwa bado hatujafikia hiyo hatua)
Katika ripoti ya World Bank ghafla DP World imeibuka Sasa ngoja niwaeleweshe Sehemu ya mkopo na msaada wa $421 milioni kuna pesa ya kujenga mfumo wa IT wa bandari kupitia TPA. Ripoti ya Benki ya Feb 2023 walisema hakuna maendeleo ILA TPA imesema imeingia makubaliano (MoU) na DP World kujenga mfumo huu wa IT ELEWENI: DP World watalipwa kutoka pesa hizi za mkopo wa Benki ya Dunia kusaidia “mifumo isomane” hawawekezi Pili kwa mujibu wa serikali walisema ile MoU ya TPA na DPW ni kuhusu mfumo wa IT (tunaambiwa ilisainiwa Feb 2022) Imekuwaje consultancy ya DPW ya IT imegeuzwa kuwa IGA na tunatoa bandari zetu kwa kusema eti DPW watatusaidia mifumo isomane alafu tunawapa uendeshaji wa bandari ambao UMESHAKAMILIKA kwa uwekezaji mkubwa wa mradi huu? Hii dili ilianza kama CONSULTANCY na kugeuzwa UPORAJI.

Pesa za mkopo wa World Bank zimetumika (na kukamilika) kupanua na kuimarisha Gati 1-7 na kujenga gati mpya Gerezani kupanua mlango wa bandari hadi Gati 11 kuboresha na kuunganisha na reli Kupanua na kuimarisha Gati 8-11 Kuna RORO terminal ilijengwa na kukamilishwa Sasa tuangalie wanachodai DP World kufanya kwa mujibu wa IGA Cha kwanza kikubwa eti kujenga, kuendesha na kusimamia RoRo terminal na Gati 1-4 na gati 5-7 Yaani pesa zote zimewekezwa za walipa kodi kupitia mradi wa sasa wa WB alafu wao wanakuja kuendesha na kusimamia? Wanawekeza nini?? Ndiyo maana mkataba haujawekwa thamani ya uwekezaji wao kumbe wanadandia mradi unaoelekea kukamilika waje wajisifu! Nyieeeeeeeeee! Mnaotetea mkataba huu mnajua kuwa mnatumika kutetea ulaji wa genge ndogo!?
 
Kuna nguvu kubwa nje ya Serikali (parallel government) kuliko Serikali yenyewe .Ndicho ninachokiona.Ni mfano wa genge la Mafia au Yakuza.
 
Mkataba ufutwe tu hakuna namna ,haiwezekani kina AMIJEI wapige mnada bandari zote za Bara huku za kwao wakiziacha ,tukikaa kimya kisa muungano tutaangukia pua ...Hakuna mzanzibar hata mmoja anayeutaka Muungano.
 
Tundu Lissu,

Vipi ile migodi uliyokuwa ukiipigia debe sana wakati wa Kikwete? Mbona hukuisemea wakati wa Magu au alikunyamazisha?
 
Huo ndiyo ulio ukweli:



Amlaumu nani huyu?

IMG_20230706_074248.jpg


Mama na achutame tu kuteleza si kuanguka.
 
Tungepata majembe ishirini kama haya tanganyika,

Hakiaka bandari zote zingerudi!!

R.I.P MTIKILA
Hii kauli yako inaonesha hujiamini, na wala huwaamini waliopo, unakosea.

Watu wapo na mapambano ya kuzikomboa bandari zetu yameshaanza kwa njia tofauti, muhimu yaendelee.
 
Tatizo la mama ni mvivu sana huwa hasomi anacholetewa ye ni kusaini baada ya kuwa amewaagiza 'muende kulitizama'!.
 
SIMLAUMU RAIS WETU MPENDWA NAWALAUMU WASHAURI WAKE NA WAANDAAJI WA MKATABA HUO!, HAWA WOTE NDIO WA KULAUMIWA, RAIS HUWA NA MAMBO MENGI, NA HUTEUWA WASAIDIZI MAKINI ILI WAMSAIDIE, PALE WANAPOSHINDWA KUMSAIDIA NDIPO HUWA SHIDA.
Yeye hana akili ya kujua baya na zuri?
 
Back
Top Bottom