Tundu Lissu si wa kupuuzwa, ni wa kusikilizwa kwa makini

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Nimeshindwa kuvumilia kutofuatilia na kushiriki siasa. Tangu miaka ya 80 nilipojiunga CCM baada ya kuhitimu masomo yangu pale Mlimani, nimejionea mengi. Nimewaona na kufanya kazi na wanasiasa waongo, wakweli, halisi na bandia. Wengi bado wapo, achilia mbali wale waliotangulia mbele ya haki.

Nimeshiriki harakati nyingi za kichama na kiserikali kutokea 'vyombo vyetu'. Nami, hakika, nimebahatika kuwa kiongozi chamani na serikalini katika awamu mbalimbali za kiuongozi. Najivunia, bila kujisifia, kutoa mchango wangu kwenye ushindi wa kishindo kuliko nyundo wa CCM yangu kabla na baada ya vyama vingi kama shilingi.

Nimewaona na kuwasikia wanasiasa wengi. Wapo wanaosema wasichokipenda, kukiamini na kukijua. Wapo wanaosema wanaokijua lakini wasichokiamini. Wapo wanaosema wanachokijua, wanachokiamini lakini hawawezi 'kukisimamia'. Wapo, wachache mno, wanaosema wanachokiamini, wanachokijua, wanachokipenda na wanaweza kukisimamia.

Kati ya hao wachache mno, Tundu Lissu, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, ni mmojawapo. Ukimtazama na kumsikiliza, anamaanisha. Haogopi kubaki peke yake. Haogopi kupingwa kwa hoja na viroja. Haogopi kukosolewa bila 'kushambuliwa'. Haogopi kuonesha msimamo wake dhahiri kwa umahiri.

Kiutaniutani, kuanzia kwenye kampeni zake za Uenyekiti wa CHADEMA, hoja yake ya No reforms, no election inabamba. Msingi wa hoja yake ni kuwa sheria na taratibu za kiuchaguzi zinapaswa kufanyiwa marekebisho makubwa ili kuonesha wazi kuwa kuna uhakika wa uchaguzi huru na wa haki. Si ana hoja hapo?

Lissu anaiuza hoja yake kwa kutoa matukio ya kichaguzi katika chaguzi zilizotangulia tangu kuanza kwa chaguzi zilizojumuisha vyama vingi. Kuna mambo hujirudia tu kwakuwa sheria, kanuni na taratibu za kiuchaguzi zinatengeneza vichaka vya uhakika vya kujificha.

Kuenguliwa wagombea kwa sababu za ajabu; kuvurugwa kwa mikutano ya kampeni; kukwamishwa na kutothaminiwa kwa mawakala; uchaguzi kusimamiwa na kuratibiwa na wateule wa Rais ambaye aidha anagombea au anamtangaza mgombea; kuwepo na magumashi kwenye kutangazwa matokeo na mambo mengineyo ya kudhuru mwili na kuharibu mali ni mambo yanayokataliwa na Lissu.

Kwa miaka yangu hii inayokaribia 80 na uzoefu wangu kisiasa wa zaidi ya miaka 40, naiona hoja ya Lissu na naiona kama yenye faida kwa wote. Hivi, hata makada wa CCM hawapendi kuwa na haki ya kuchagua na kuchaguliwa bila kuchakachuliwa? Haki ya kuchagua na kuchaguliwa ni haki ya kikatiba. Lissu ana hoja ya haja.

Tafadhali Mama, Lissu asipuuzwe!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)
 
Ngoja wake kina Lucas wasio jua kureason wao ni kupinga Kila kitu ikiwa kimetoka kwa mtu wasio mpenda lisu ana hoja Tena yenye mashiko kwa taifa zima na wote watanufaika iwe ccm Hadi chauma huko
Tanzania mpya inakuja tusipuuze
 
Wapo wanaotuamba tusimuunge mkono lisu kwenye ni reforms no election kwa sababu akiitisha maandamano hatutakuwepo!
Wao hawazungumzii uzito na umuhimu wa hoja ya lisu hapana. Wanazungumzia maandamano sasa.
 
Hakika Lissu et al wana HOJA wasikilizwe..Naendelea kumuombea Mh Rais azidi kupata BUSARA na HEKIMA za kuwaepuka viongozi wafitni wasiopenda kuona Mama Tanzania anastawi
 
No reforms no election is a no brainer.

Maana yake ni kwamba huhitaji ubongo mkubwa kujua ukweli huu.

Na hizo reforms hazijaanza kuongelewa leo. Zimeongelewa na Jaji Nyalali kwenye ripoti yake, zimeongelewa na Jaji Kisanga kwenye ripoti yake, zimeongelewa na Jaji Bomani kwenye ripoti yaje, zineongelewa na Jaji Warioba kwenye ripoti yake. Tume nne hizo za Nyalali, Kisanga, Bomani na Warioba, zote zimeongelea reforms. Tangu kabla CHADEMA haijazaliwa wakati wa ripoti ya Jaji Nyalali.

Tatizo ni, Watanzania wataelewa na kuunga mkono?
 
Hebu fikiria mizee kama Wasira haioni aibu kuongozwa na kupiga magoti kwa Saa100 amabaye kismsingi yupo hapo kwasababu ya mapungufu y katiba na mfumo mbovu wa uchaguzi!!. Na lile pua lake kama kiko.... Pumbaza zao ccm wote...
 
"kwamba kila uchaguzi lazima kuwe na matukio ya watu kuuwawa na kuumizwa?" hii hoja ya Lisu imenigusa sana kama binadamu mwenye ubinadamu, mtu mwenye utu. Ni dhahiri kabisa hayo hutokea katika chaguzi zetu, je kuna shida gani serikali kukaa na wadau wa siasa na uchaguzi kuona namna ya kukomesha haya?! binafsi sioni shida kabisa sababu ni kwa manufaa ya maisha ya watu.
 
Nimeshindwa kuvumilia kutofuatilia na kushiriki siasa. Tangu miaka ya 80 nilipojiunga CCM baada ya kuhitimu masomo yangu pale Mlimani, nimejionea mengi. Nimewaona na kufanya kazi na wanasiasa waongo, wakweli, halisi na bandia. Wengi bado wapo, achilia mbali wale waliotangulia mbele ya haki.

Nimeshiriki harakati nyingi za kichama na kiserikali kutokea 'vyombo vyetu'. Nami, hakika, nimebahatika kuwa kiongozi chamani na serikalini katika awamu mbalimbali za kiuongozi. Najivunia, bila kujisifia, kutoa mchango wangu kwenye ushindi wa kishindo kuliko nyundo wa CCM yangu kabla na baada ya vyama vingi kama shilingi.

Nimewaona na kuwasikia wanasiasa wengi. Wapo wanaosema wasichokipenda, kukiamini na kukijua. Wapo wanaosema wanaokijua lakini wasichokiamini. Wapo wanaosema wanachokijua, wanachokiamini lakini hawawezi 'kukisimamia'. Wapo, wachache mno, wanaosema wanachokiamini, wanachokijua, wanachokipenda na wanaweza kukisimamia.

Kati ya hao wachache mno, Tundu Lissu, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, ni mmojawapo. Ukimtazama na kumsikiliza, anamaanisha. Haogopi kubaki peke yake. Haogopi kupingwa kwa hoja na viroja. Haogopi kukosolewa bila 'kushambuliwa'. Haogopi kuonesha msimamo wake dhahiri kwa umahiri.

Kiutaniutani, kuanzia kwenye kampeni zake za Uenyekiti wa CHADEMA, hoja yake ya No reforms, no election inabamba. Msingi wa hoja yake ni kuwa sheria na taratibu za kiuchaguzi zinapaswa kufanyiwa marekebisho makubwa ili kuonesha wazi kuwa kuna uhakika wa uchaguzi huru na wa haki. Si ana hoja hapo?

Lissu anaiuza hoja yake kwa kutoa matukio ya kichaguzi katika chaguzi zilizotangulia tangu kuanza kwa chaguzi zilizojumuisha vyama vingi. Kuna mambo hujirudia tu kwakuwa sheria, kanuni na taratibu za kiuchaguzi zinatengeneza vichaka vya uhakika vya kujificha.

Kuenguliwa wagombea kwa sababu za ajabu; kuvurugwa kwa mikutano ya kampeni; kukwamishwa na kutothaminiwa kwa mawakala; uchaguzi kusimamiwa na kuratibiwa na wateule wa Rais ambaye aidha anagombea au anamtangaza mgombea; kuwepo na magumashi kwenye kutangazwa matokeo na mambo mengineyo ya kudhuru mwili na kuharibu mali ni mambo yanayokataliwa na Lissu.

Kwa miaka yangu hii inayokaribia 80 na uzoefu wangu kisiasa wa zaidi ya miaka 40, naiona hoja ya Lissu na naiona kama yenye faida kwa wote. Hivi, hata makada wa CCM hawapendi kuwa na haki ya kuchagua na kuchaguliwa bila kuchakachuliwa? Haki ya kuchagua na kuchaguliwa ni haki ya kikatiba. Lissu ana hoja ya haja.

Tafadhali Mama, Lissu asipuuzwe!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)
Naaam
 
Duniani kote hakuna uchaguzi wa haki!Bali takwa la wenye Dola ndilo lishindalo uchguzi!!

Uchaguzi was wabunge labda ndio unaweza kuwa wa haki lakini sio kwa majimbo yote hasa ya kimkakati kwamba wayaache yaende kama watu watakavyo!!

Lisu ana hoja lakini hoja zake haziwezi kukidhi dhana za kiutawala na kiouongozi ambazo Dola imejiwekea!!

Hasta mataifa makubwa Hali IPO hivyo hivyo japo kw aTanzania na CCM tulipaswa kuwa smart kidogo kuliko ilivyo sasa!!

Angalau upinzani uwe asilimia 40 bungeni Kwa afya ya taifa!pia angalau tuwe na chama mbadala kama ccm B ambayo itashinda uchaguzi mkuu na kinda serikali kama mbinu ya kuhodhi na ku spin joto na vugu vugu la upinzani nchini kuliko kutumia marungu na maji ya washa washa hiyo ingesaidia sana!!

Mimi ni muumini was kinachotokea pale America,jinsi Republicans na Democrat's wanavyopokezana madaraka!!hizo ni mbinu za idara na dola Ili ku spin matumizi ya nguvu na sarakasi nyingi kwenye chaguzi zetu!!
 
Nimeshindwa kuvumilia kutofuatilia na kushiriki siasa. Tangu miaka ya 80 nilipojiunga CCM baada ya kuhitimu masomo yangu pale Mlimani, nimejionea mengi. Nimewaona na kufanya kazi na wanasiasa waongo, wakweli, halisi na bandia. Wengi bado wapo, achilia mbali wale waliotangulia mbele ya haki.

Nimeshiriki harakati nyingi za kichama na kiserikali kutokea 'vyombo vyetu'. Nami, hakika, nimebahatika kuwa kiongozi chamani na serikalini katika awamu mbalimbali za kiuongozi. Najivunia, bila kujisifia, kutoa mchango wangu kwenye ushindi wa kishindo kuliko nyundo wa CCM yangu kabla na baada ya vyama vingi kama shilingi.

Nimewaona na kuwasikia wanasiasa wengi. Wapo wanaosema wasichokipenda, kukiamini na kukijua. Wapo wanaosema wanaokijua lakini wasichokiamini. Wapo wanaosema wanachokijua, wanachokiamini lakini hawawezi 'kukisimamia'. Wapo, wachache mno, wanaosema wanachokiamini, wanachokijua, wanachokipenda na wanaweza kukisimamia.

Kati ya hao wachache mno, Tundu Lissu, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, ni mmojawapo. Ukimtazama na kumsikiliza, anamaanisha. Haogopi kubaki peke yake. Haogopi kupingwa kwa hoja na viroja. Haogopi kukosolewa bila 'kushambuliwa'. Haogopi kuonesha msimamo wake dhahiri kwa umahiri.

Kiutaniutani, kuanzia kwenye kampeni zake za Uenyekiti wa CHADEMA, hoja yake ya No reforms, no election inabamba. Msingi wa hoja yake ni kuwa sheria na taratibu za kiuchaguzi zinapaswa kufanyiwa marekebisho makubwa ili kuonesha wazi kuwa kuna uhakika wa uchaguzi huru na wa haki. Si ana hoja hapo?

Lissu anaiuza hoja yake kwa kutoa matukio ya kichaguzi katika chaguzi zilizotangulia tangu kuanza kwa chaguzi zilizojumuisha vyama vingi. Kuna mambo hujirudia tu kwakuwa sheria, kanuni na taratibu za kiuchaguzi zinatengeneza vichaka vya uhakika vya kujificha.

Kuenguliwa wagombea kwa sababu za ajabu; kuvurugwa kwa mikutano ya kampeni; kukwamishwa na kutothaminiwa kwa mawakala; uchaguzi kusimamiwa na kuratibiwa na wateule wa Rais ambaye aidha anagombea au anamtangaza mgombea; kuwepo na magumashi kwenye kutangazwa matokeo na mambo mengineyo ya kudhuru mwili na kuharibu mali ni mambo yanayokataliwa na Lissu.

Kwa miaka yangu hii inayokaribia 80 na uzoefu wangu kisiasa wa zaidi ya miaka 40, naiona hoja ya Lissu na naiona kama yenye faida kwa wote. Hivi, hata makada wa CCM hawapendi kuwa na haki ya kuchagua na kuchaguliwa bila kuchakachuliwa? Haki ya kuchagua na kuchaguliwa ni haki ya kikatiba. Lissu ana hoja ya haja.

Tafadhali Mama, Lissu asipuuzwe!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)
Mzee, shida ya wanaccm ni kukosa uzalendo, na thamani maisha ya raia ni zero, kwa ssb ya egoism
 
wampuuze waione nguvu ya umma yenye backup ya nguvu za mbinguni.

Huyu mtu hakupona marisasi yale yote bure
 
Ni ajabu sana kuona kuna wazee bado wana akili TIMAMU kama wewe,.....wazee wengi sasa wamegeuka WAPUMBAVU wakubwa wa kushindwa kutofautisha CCM na Mungu,.... wao ni kuabudu CCM tu,.....❗❗🚮
 
No reforms no election is a no brainer.

Maana yake ni kwamba huhitaji ubongo mkubwa kujua ukweli huu.

Na hizo reforms hazijaanza kuongelewa leo. Zimeongelewa na Jaji Nyalali kwenye ripoti yake, zimeongelewa na Jaji Kisanga kwenye ripoti yake, zimeongelewa na Jaji Bomani kwenye ripoti yaje, zineongelewa na Jaji Warioba kwenye ripoti yake. Tume nne hizo za Nyalali, Kisanga, Bomani na Warioba, zote zimeongelea reforms. Tangu kabla CHADEMA haijazaliwa wakati wa ripoti ya Jaji Nyalali.

Tatizo ni, Watanzania wataelewa na kuunga mkono?
wataelewa, hata kama sio wote. hadi sasa wameendelea kuelewa
 
Back
Top Bottom