Tundu Lissu si wa kupuuzwa, ni wa kusikilizwa kwa makini

Umaskini ndiyo unaowafanya wana CCM wengi kukikumbatia chama hicho vinginevyo wengi wanaunga mkono "No Reforms No Election!
 
Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa na madhehebu ya dini hivi karibuni mmesikika kwamba wako watu wanaviashiria vya kuleta uvunjivu wa amani kutokana na hoja za kuleta mabadiliko katka uchaguzi wetu.Hii inatusikitisha sana tunaofuatilia hoja za wapinzani.hivi mpinzani akisema 1+1=2 na sio 1+1=3 kosa lake la kuvunja amani ni lipi?Si dunia nzima wajua jawabu ni 2?Tufafanueni basi ili tuliamini jibu lenu
 
Huyu jamaa Tundu Lissu siyo mtu wa kumchukulia kwa mchezo mchezo/mazoea! ccm wajitafakari mapema kabla hawajaumbuka. Huyu mtu siyo wa kawaida.

Imagine alishambuliwa kwa risasi zaidi ya 30! Na 16 kati ya hizo ziliingia mwilini! Na bado bado alipona eti!! Na risasi nyingine bado anaishi nazo mwilini mpaka sasa!

Kwenye uchaguzi wa chama chake alifanikiwa kumuangusha Mwenyekiti wake wa chama aliyedumu madarakani kwa zaidi ya miaka 20! Huku akiwa na ushawishi wa kila aina ndani ya hicho chama, pamoja na serikalini!

Bado ukiangalia mikutano yake ya hadhara, unakuta watu wengi wamejitokeza! Tena wakiwa hawajasombwa kwa malori kutoka maeneo ya jirani, kama inavyotokea kwa chama tawala!

Mwisho kabisa ukiangalia sera na hoja zao zote zina mashiko! Kuanzia ishu ya no reform no election, ugumu wa maisha, ufisadi uliokithiri nchini, ukosefu mkubwa wa ajira, suala la muungano uliojaa kero nyingi, nk.

Serikali na chama tawala nadhani wangejitahidi tu kuajiri polisi wa kutosha mwaka huu! Maana wasitegemee kama watapata mteremko kwenye uchaguzi wa mwaka huu. Huyu jamaa anayeitwa Tundu Lissu na yule msaidizi wake John Heche, siyo watu wepesi hata kidogo! Na huwa hawaamini katika kile kinachoitwa busara, hekima, au maridhiano ya kinafiki. Ni hayo tu.
 
Nimeshindwa kuvumilia kutofuatilia na kushiriki siasa. Tangu miaka ya 80 nilipojiunga CCM baada ya kuhitimu masomo yangu pale Mlimani, nimejionea mengi. Nimewaona na kufanya kazi na wanasiasa waongo, wakweli, halisi na bandia. Wengi bado wapo, achilia mbali wale waliotangulia mbele ya haki.

Nimeshiriki harakati nyingi za kichama na kiserikali kutokea 'vyombo vyetu'. Nami, hakika, nimebahatika kuwa kiongozi chamani na serikalini katika awamu mbalimbali za kiuongozi. Najivunia, bila kujisifia, kutoa mchango wangu kwenye ushindi wa kishindo kuliko nyundo wa CCM yangu kabla na baada ya vyama vingi kama shilingi.

Nimewaona na kuwasikia wanasiasa wengi. Wapo wanaosema wasichokipenda, kukiamini na kukijua. Wapo wanaosema wanaokijua lakini wasichokiamini. Wapo wanaosema wanachokijua, wanachokiamini lakini hawawezi 'kukisimamia'. Wapo, wachache mno, wanaosema wanachokiamini, wanachokijua, wanachokipenda na wanaweza kukisimamia.

Kati ya hao wachache mno, Tundu Lissu, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, ni mmojawapo. Ukimtazama na kumsikiliza, anamaanisha. Haogopi kubaki peke yake. Haogopi kupingwa kwa hoja na viroja. Haogopi kukosolewa bila 'kushambuliwa'. Haogopi kuonesha msimamo wake dhahiri kwa umahiri.

Kiutaniutani, kuanzia kwenye kampeni zake za Uenyekiti wa CHADEMA, hoja yake ya No reforms, no election inabamba. Msingi wa hoja yake ni kuwa sheria na taratibu za kiuchaguzi zinapaswa kufanyiwa marekebisho makubwa ili kuonesha wazi kuwa kuna uhakika wa uchaguzi huru na wa haki. Si ana hoja hapo?

Lissu anaiuza hoja yake kwa kutoa matukio ya kichaguzi katika chaguzi zilizotangulia tangu kuanza kwa chaguzi zilizojumuisha vyama vingi. Kuna mambo hujirudia tu kwakuwa sheria, kanuni na taratibu za kiuchaguzi zinatengeneza vichaka vya uhakika vya kujificha.

Kuenguliwa wagombea kwa sababu za ajabu; kuvurugwa kwa mikutano ya kampeni; kukwamishwa na kutothaminiwa kwa mawakala; uchaguzi kusimamiwa na kuratibiwa na wateule wa Rais ambaye aidha anagombea au anamtangaza mgombea; kuwepo na magumashi kwenye kutangazwa matokeo na mambo mengineyo ya kudhuru mwili na kuharibu mali ni mambo yanayokataliwa na Lissu.

Kwa miaka yangu hii inayokaribia 80 na uzoefu wangu kisiasa wa zaidi ya miaka 40, naiona hoja ya Lissu na naiona kama yenye faida kwa wote. Hivi, hata makada wa CCM hawapendi kuwa na haki ya kuchagua na kuchaguliwa bila kuchakachuliwa? Haki ya kuchagua na kuchaguliwa ni haki ya kikatiba. Lissu ana hoja ya haja.

Tafadhali Mama, Lissu asipuuzwe!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)
🤣🤣TUPATUPA umepigaje pigaje hapo??
Andiko safi, chief ulipotea sana hapa jukwaani!!

Karibu tena
 
Hapo kwenye "Vyombo vyetu" nimeelewa,

Nimeshindwa kukuelewa uliporudisha mpira kwa uliyemuita " Mama" amsikizr Lissu.

Yaani mwizi aende kwa Polisi kwa hiari yake wakubaliane kuacha wizi!
 
Mbwa akiwa anabweka sana anarushiwa mfupa anaacha kubweka anaanza kulamba mfupa, kwahiyo atatupiwa mfupa tu
 
Ngoja wake kina Lucas wasio jua kureason wao ni kupinga Kila kitu ikiwa kimetoka kwa mtu wasio mpenda lisu ana hoja Tena yenye mashiko kwa taifa zima na wote watanufaika iwe ccm Hadi chauma huko
Tanzania mpya inakuja tusipuuze
Plus
Tlaatlaah 🚮
 
wasira nae analia hapa harafu mseme lisu anakosea ,alipigwa za uso ubunge wa bunda enzi akiwa nccr
 
Attachments

  • 6017471-46d1e509592bd73d8313972ca4ec270.mp4
    805.6 KB
Ukweli ni ukweli tu, atakama walio wengi hawaamini huko. Muda ni mwalimu mzuri, tunangoja....
 
My friends ladies and gentlemen,

kwa maoni yangu huru, nadhani ni muhimu sana, huyo tapeli wa kuomba kuchangiwa pesa kwa mtindo wa tone tone, na genge lake la vibaka wa siasa ndani ya chama chao, yafaa kupuuzwa na kuogopwa kama ukoma,

kwasabb ni maadui wa demokrasia, na hawataki kabisa kuskia mambo ya demokrasia, ila wanataka tu kutapeli wananchi pesa kidigitali kwaajili ya kunywa wisky na nyama.

Ni muhimu kujihadhari na huyo yahaya kibaraka wa mambwenyenye ya Magharibi 🐒
 
Nimeshindwa kuvumilia kutofuatilia na kushiriki siasa. Tangu miaka ya 80 nilipojiunga CCM baada ya kuhitimu masomo yangu pale Mlimani, nimejionea mengi. Nimewaona na kufanya kazi na wanasiasa waongo, wakweli, halisi na bandia. Wengi bado wapo, achilia mbali wale waliotangulia mbele ya haki.

Nimeshiriki harakati nyingi za kichama na kiserikali kutokea 'vyombo vyetu'. Nami, hakika, nimebahatika kuwa kiongozi chamani na serikalini katika awamu mbalimbali za kiuongozi. Najivunia, bila kujisifia, kutoa mchango wangu kwenye ushindi wa kishindo kuliko nyundo wa CCM yangu kabla na baada ya vyama vingi kama shilingi.

Nimewaona na kuwasikia wanasiasa wengi. Wapo wanaosema wasichokipenda, kukiamini na kukijua. Wapo wanaosema wanaokijua lakini wasichokiamini. Wapo wanaosema wanachokijua, wanachokiamini lakini hawawezi 'kukisimamia'. Wapo, wachache mno, wanaosema wanachokiamini, wanachokijua, wanachokipenda na wanaweza kukisimamia.

Kati ya hao wachache mno, Tundu Lissu, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, ni mmojawapo. Ukimtazama na kumsikiliza, anamaanisha. Haogopi kubaki peke yake. Haogopi kupingwa kwa hoja na viroja. Haogopi kukosolewa bila 'kushambuliwa'. Haogopi kuonesha msimamo wake dhahiri kwa umahiri.

Kiutaniutani, kuanzia kwenye kampeni zake za Uenyekiti wa CHADEMA, hoja yake ya No reforms, no election inabamba. Msingi wa hoja yake ni kuwa sheria na taratibu za kiuchaguzi zinapaswa kufanyiwa marekebisho makubwa ili kuonesha wazi kuwa kuna uhakika wa uchaguzi huru na wa haki. Si ana hoja hapo?

Lissu anaiuza hoja yake kwa kutoa matukio ya kichaguzi katika chaguzi zilizotangulia tangu kuanza kwa chaguzi zilizojumuisha vyama vingi. Kuna mambo hujirudia tu kwakuwa sheria, kanuni na taratibu za kiuchaguzi zinatengeneza vichaka vya uhakika vya kujificha.

Kuenguliwa wagombea kwa sababu za ajabu; kuvurugwa kwa mikutano ya kampeni; kukwamishwa na kutothaminiwa kwa mawakala; uchaguzi kusimamiwa na kuratibiwa na wateule wa Rais ambaye aidha anagombea au anamtangaza mgombea; kuwepo na magumashi kwenye kutangazwa matokeo na mambo mengineyo ya kudhuru mwili na kuharibu mali ni mambo yanayokataliwa na Lissu.

Kwa miaka yangu hii inayokaribia 80 na uzoefu wangu kisiasa wa zaidi ya miaka 40, naiona hoja ya Lissu na naiona kama yenye faida kwa wote. Hivi, hata makada wa CCM hawapendi kuwa na haki ya kuchagua na kuchaguliwa bila kuchakachuliwa? Haki ya kuchagua na kuchaguliwa ni haki ya kikatiba. Lissu ana hoja ya haja.

Tafadhali Mama, Lissu asipuuzwe!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)
hasanteeee wasalimie wazee wetu Butiku na Warioba waachie nakala moja ya huu ujumbe
 
Kwa kifupi niseme hivi,mwenye nyuzi nyingine kama uzi huu asisite kuandika.Sisi wasomaji makini tupo,tutasoma na kuunga mkono hoja nzito kwa maslahi ya umma!
 
Back
Top Bottom