dikteta2020
JF-Expert Member
- Aug 14, 2018
- 595
- 3,991
Yupo Arusha anaongea na waandishi muda huu na huo ndiyo ujumbe wake kwa tume. Malalamiko hayapelekwi CHADEMA wala Twitter bali anapelekewa yeye.
Tundu Lissu amesema kuwa yeye ndiye aliyesaini hati ya maadili ya tume na lolote linalomhusu yeye kuhusu maadili ya uchaguzi ni lazima apelekewe yeye kwa maandishi.
Lissu amesema kuwa anasikia tu huko mitandaoni kuwa vyama vya NRA na CCM vimepeleka malalamiko dhidi yake kwa tume ya uchaguzi kuwa anakiuka maadili ya uchaguzi ambayo aliyasaini.
Hivyo basi amesema mpaka leo asubuhi hajapelekewa malalamiko yoyote kimaandishi yakimhusu kutoka tume hivyo anaendelea na ratiba yake kama ilivyopangwa na tume.
=======
Mgombea urais kupitia tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu amesema,
“Nikichaguliwa kuwa Rais nitaunda Serikali ya Chadema kwasababu ya Katiba inavyosema. Kama kutakuwa na uhitaji itabidi tubadilishe Katiba kwanza, na moja ya maazimio ya Chadema ikishinda Uchaguzi Mkuu ndani ya siku 100 tutaanzisha mchakato wa Katiba mpya.”Tundu Lissu
“Bob Amsterdam ni Mawakili wangu, wanashughulika na maswala yangu yote yakisheria ya ndani na nje ya Nchi. Kama Tume imeandikiwa barua basi Mawakili wangu wamekuwa wakitimiza wajibu wao, Kama nilivyosema uchaguzi mkuu hatutaki mchezo, na Chadema lazima tushinde uchaguzi huu.”TL