Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Sijapokea wito kutoka Tume ya Uchaguzi. Sitarajii kuacha Kampeni kwa kuitikia wito kutoka mitandaoni

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Sijapokea wito kutoka Tume ya Uchaguzi. Sitarajii kuacha Kampeni kwa kuitikia wito kutoka mitandaoni

Mgombea Urais kupitia Chadema amesema hajapokea malalamiko yoyote kuhusiana na uchaguzi na hajapokea wito wowote wa kufika tume zaidi ya kusikia kwenye mitandao
Hivyo hawezi kuacha Kampeni kwa maneno ya mitandaoni

=====

=> Sijapokea malalamiko yoyote juu ya jambo lolote linalohusiana na kampeni za Uchaguzi Mkuu huu kutoka NEC. Sijapokea wito wowote kuhusu jambo lolote linalohusiana na kampeni za Uchaguzi Mkuu huu kutoka NEC. Sitarajii kuacha kampeni ili kuitikia wito wa mitandaoni wa mtu yeyote!

=> Mkurugenzi wa Uchaguzi huyu ni kada wa CCM, by his own admission. Na ni mteule wa Rais Magufuli, mgombea Urais kwenye Uchaguzi Mkuu huu. Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Makamishna wote wa Tume ya Uchaguzi na Wasimamizi wa Uchaguzi wote ni wateule wa Magufuli. Huo uhuru uko wapi?

=> I've not received any complaint against my conduct of the election campaign from NEC. I've not received any summons from NEC on any matter concerning my conduct of the campaign. I don't intend to attend any purported hearing on any matter concerning my conduct of the campaign.


Mambo yamepamba moto. Ni mwendo washeria na siasa. Sasa huyu vyote anaviweza. Kamatia hapo na ongeza makali kidoo. - NI MWENDO WA KANYAGA TWENDE TU.
 
Kama ni hivyo, wanasema hiyo ni CCM mpya. Slogan yao ni MATAGA
Basi kama ndo kwa uelewa yako ndiyo hiyo hiyo naomba uipigie kura CCM ili iendelee kuliongoza Taifa hili na kuniletea maendeleo tunaomba kura yako na familia yako.


JPM 2020-2025
CCM USHINDI NI JADI
 
Mi kwa ushauri wangu,neck wangeachana na lisu,ccm itashinda hamna haja ya kupanick,,kana kasema uongo atajijua mwenyewe,,kampeni za kisiasa duniani kote ziko hivyo,,waache wagombea wajinafasi,
Mahera aondoe wasiwasi tutashinda huu uchaguzi
 
Maana ya wito wa kisheria unamaanisha nini?. Je mpaka upokee summons au barua na usaini kwenye dispatch?. Kama ndo hivyo Lissu yuko sawa.
 
Majibu yako huku,

Uchaguzi 2020 - Tume imemwita Tundu Lissu, lakini haina mamlaka wala uwezo wa kumuadhibu

Wampelekee tu ameruka viunzi vingi vizito vikiwemo vyakumrest in Peace imeshindikana..Tume inaupendeleo wa wazi mgombea mwingine anatubagua kwa kuongea kilugha ambacho wengi hatuelewi na pia amesikika akibagua wapga kura wasiompigia kura waziwazi kuwa hatapeleka maendeleo huku kodi zao akiztaka kuendesha nchi bila kujali mshikamano wa Taifa hili toka Enzi za Julius Kambarage Nyerere RIP. Tume imekaa kimya na Msajiri amekaa kimya!! Watu wanataka fair play ili nchi hii iwe mfano wa democracy makini!!
 
Nakuabaliana na wewe kwamba Chadema wanaweza kuogopa kuandamana baada ya uchaguzi.

Kumbe unajua wataogopa tu maana husemi na unajua wana haki. Asante

Majibu yako huku,

Uchaguzi 2020 - Tume imemwita Tundu Lissu, lakini haina mamlaka wala uwezo wa kumuadhibu


Kwa vile Kikwete aliwahi kusema hivyo ndio unafikiri Lisu ana chochote?

Siku ile mnazindua kampeni mbagala alaiwajaza upepo kwamba andamaneni nchi nzima kushinikiza walioenguliwa kurudishwa. Sikuona hata mbu ikiandamana au sijui hamkumuelewa kwamba kasema anzeni kuandamana?

Baada ya 28 oktoba Lisu ataijua rangi halisi ya wanachadema!

Amuulize Slaa
 
Hivi mnagombea Uraisi wa JMTZ au tls? Huyo Tundu Lisu anauwa chadema ni bora Mbowe na wachaga waingilie kati kuokoa chama chenu, mwenzenu anafikiri yuko darasani akibishana kuhusu sheria na vilaza wenzake, ...
 
Basi kama ndo kwa uelewa yako ndiyo hiyo hiyo naomba uipigie kura CCM ili iendelee kuliongoza Taifa hili na kuniletea maendeleo tunaomba kura yako na familia yako.


JPM 2020-2025
CCM USHINDI NI JADI
Mimi niko CCM ya zamani. Sifungaman na CCM mpya.
 
Kwa Mujibu wa Taarifa ya Dk. Wilson Mahera Tume ndiyo mlalamikaji na mlalamikiwa ni Tundu Lissu!

Sasa tujiulize,

1. Inawezekanaje Tume ilalamike, imuite inayemlalamikia na iamue kwa haki?

2. Kama Mheshimiwa Lissu akitoa ushahidi wake kwa Tume,nani atathibitisha ushahidi ule kuwa ni wa kweli?

3. Ikiwa ushahidi utabainika ni wa kweli,je Tume iko tayari kuwajibika kwa kujiuzulu?
 
Back
Top Bottom