Ukisema kuwa kufikia 2025 Tanzania itakuwa haina 'wanyonge' tena, itabidi pia uhakikishe kwamba miradi yote mipya na mikuu kuu ambayo itahitajika kuwepo nayo itakuwa yote imekamilika kabisa! Mambo yasiyowezekana.
Hata kama kwa muujiza, yote hayo yatakuwa yametimizwa, dunia hii mabeberu watakuwa wamekwisha?
Na hawa wanaotupiga vita ya kiuchumi nao tutawafanyaje kama jemadari wetu mashuhuri tutamwachia asiendelee kulilinda taifa hili?
Jambo pekee linaloweza kuzuia kuendelea kuwepo kwenye madaraka ni hilo lisiloweza kuzuiwa na binaadam yeyote.
Vinginevyo, huyu yupo sana, ili mradi tu bado atakuwa anamiliki bunduki, mabomu ya machozi na vyombo vingine vyote tulivyomkabidhi ili avitumie kufanya kazi zetu, na badala yake akavigeuza kuwa vifaa vyake vya kumlinda na kutetea kila anachotaka.
Kwa hiyo ni unafiki mtupu kuendelea kuleta mada kama hizi kama hadaa kwa wanaJF.