Tundu Lissu: Suala la kuongeza muda wa Rais ni ajenda ya Rais Magufuli

Tundu Lissu: Suala la kuongeza muda wa Rais ni ajenda ya Rais Magufuli

Anamuogopa nini mzee, anataka aje agombee tena 2025.
 
Lisu ni debe tupu lile
Wewe ni debe lililo jaa, jikite basi kwenye hoja, kwa kuwa wewe ni iron boy ngoja nikusaidie; hoja hapa ni KUONGEZA MUDA WA KUKAA MADARAKANI NI AGENDA YA MAGUFULI.
Lissu achana naye, yule ni muujiza unao ishi.
 
Mbona alishasema mara nyingi kwenye mikutano yake,
Alimwambia mzee mwinyi na mbunge msukuma.
Akasema hataongeza hata dakika?
Mi naona magufuti aendelee ili bwana lisu aendelee kukaa huko mpaka azeeke aje kama akina kambona.
Yaani unataka kuua mende kwa bunduki? Aisee.
 
kwa maoni yangu binafsi, bado hadi leo hii trh 8/3/2021 bado sijaona mtu mwenye uwezo mkubwa wa kiutendaji na Uongozi kama Rais JPM.

Imara, Jasiri, Mfuatiliaji, mkali panapostahili, Mbana matumizi ya serikali, mwadilifu, mchapakazi asiye choka, mzalendo wa kweli, asiye mnafiki, msema kweli bila woga, anaye jali wanyonge n.k, lkn kubwa zaidi Mcha Mungu na mwenye kuheshimu Imani za watu wengine.
 
Yeye mwenyewe alishawahi kutoa kauli zinazoashiria kuwa yeye mwenyewe anafaa na hajawahi kuwapo mwingine:
1. Miaka yote toka uhuru 'haya' hayakufanyika.
2. Mnipigie kura ili nimalizie miradi hii mikubwa.
3. .....
4. .....

Utadhani kila kinachoonekana sasa alifanya yeye na hata Mwalimu hakufanya lolote na maana!

Utadhani ni lazima miradi aliyoanza ni lazima amalize yeye, huku hata miradi mingi aliyoanzisha mzee wa Msoga, kaiendeleza yeye wa 'Chuttle'!

Hii agenda inayopigiwa debe ni yake mwenyewe. Haihitaji ubongo mkubwa kuliko wa kuku kuuelewa ushahidi wa kimazingira ulio wazi.
 
Kama Magufuli angekuwa hataki kuongeza muda, hakika hakuna mwanaCCM angepanua mdomo wake kulinena hilo. Kila mwenye akili anajua kuwa hili linasemwa semwa sana kwa sababu yeye anapenda iwe hivyo.
La vyuma vimekaza halisikiki tena! Alilishukia kama mwewe ashukiavyo vifaranga. Hakulipenda. Katoa amri kabisa wakamatwe. Kimya! Hili sasa maandamano yanaratibiwa. Yana baraka zote za Muroto na Mambokesho. Matembezi ya hiari ya Mwamakula hata mimba yake kutungwa ni haramu. Ikizaliwa washirilki ni mkong'oto wa mbwa koko tena mwizi. Gesi letu la pulisi linajua mkulu kalalia wapi. Maria Sarungi kwao si mwanaharakati bali mchochezi. Lakini Musiba ni mwanaharakati tena huru!
 
Mbona alishatoka na clip ipo mitandaoni akiongea na Pole pole.
Akasema hana mpango wa kuchezea katiba
 
Kuondoshwa kwa Bashiru kutoka nafasi ya ukatibu mkuu wa CCM na kupewa ukatibu mkuu kiongozi wa ikulu unaweza kutumika na kushadadisha mashabiki kuhusu suala hili. Msimamo wa Kakurwa siku zote ulikuwa kwamba hakuna kitu chochote kile kama cha kubalisha ukomo wa kuitumikia nafasi ya urais kwa mujibu wa katiba iliyopo.
La ukomo wa urais akiliongelea JPM hata hewa inayomzunguka inakataa anachosema. Kwa kuwa hakuna ukweli hata chembe. Akilisemea Bashiru hata chekechea anajua anamaanisha hilo. Hakuna unafiki. Kama chekechea katambua, je, JPM si zaidi?

Kumtumbua KM wa ccm ni tricky sana kuliko kumtumbua KMK wa ikulu. Kuna siku balozi mteule atatembelea nchi fulani na kubaki huko. Kimya. Ikulu inapata ambaye angalau aliishakaimu naibu KM wizara ya ndani ya ofisi ya makamu wa rais. Sikia tu mkuu nchi hii kuna vyeo na hata vya ziada. Utashangaa wakati wapo wafanyakazi hewa.

Ofisi hewa, mhudumu ofisi hewa, ofisa hewa wa cheo hewa akifanya kazi hewa na kupokea mshahara hewa wa hela halali! Kila kitu hewa. Kama maji ni uhai, hewa si zaidi?
 
Kuna watu walisema wataandamana kushinikiza aongezewe muda. Sasa jiulize watazuiwa au wataruhusiwa. Je, kama wataruhusiwa halafu lijitokeze kundi lingine lipinge asiongezewe muda itakuwaje.

Halafu ikiwa ni sawa wanajitokeza watu wanasema aongezewe muda, je, itavumilika wajitokeze watu hata humo bungeni wakatae hilo kwa kuitetea katiba? Mbona wasema ni uhuru wa maoni. Ni uhuru upi huo wa upande mmoja.
 
Hili jambo wala halihitaji ushahidi,ni wazi kabisa,Hao wengine wanatumika tu,
Kumbuka yule mbunge wa nkasi,wamemtoa bungeni kimkakati,angalia walioingia sasa,ni zaidi yake,unadhani kuna bahati mbaya hapo
Litakuwa limepitishwa kwenye chama
 
MKUU Aspirin atamke mara ngapi.

Au huwa husikilizi TBC?
TBC? Hapana...

Kama alishatamka, hawa wanaoendelea kukampeni wanamdharau au wanamwona boya??

Hivi unaamini kama kweli akiwakaripia kuwa hataki kusikia huu mjadala ukiendelea wataendelea kushupaa??

Unadhani kwanini hawakaripii??
 
Japokuwa Magufuli ameshajuwa record “akipinga” kuongezewa hata dakika moja baada ya muda wake kuisha, hii haitowazuia akina Ndugai kuanzisha mchakato wao bungeni
 
Hivi unaamini kuna kiongozi wa Africa hataki kuongeza muda akipata mwanya...?

Kila kitu analipiwa na mshahara bado mkubwa , marupurupu kibao., na ulinzi muda wote na kufanya chochote bila kuhojiwa..

Jiwe anaelewa kila kitu ndio maana hata makundi yalioanzwishwa ya kuunga mkono kutoa ukomo wa muda wa utawala kwa kufanya maandano ya amani lakini hawajachukuliwa hatua ilhali askofu Emmanuel alianzisha kitu kama hicho ila kwa kudai katiba mpya tunajua nini kiliffuata
 
Kama, kipande cha picha mwendo ulichokitundika hapa ni cha bwana TAL na kwamba maneno hayo hajalishwa kupitia mifumo tundu ya Tarakinishi basi hakuna haja ya kusumbua ubongo hii inathibitisha ni kwa kiwango gani anamwogopa pindi akiwania tena kinyang'anyiro hicho hawezi ambulia chochote angalau za huruma alizopata mwaka jana 2020.

The man is remotely expressing his real hatred towards Dr. Magufuli to psychologically attempt whirl-deflecting the political polarity (political party ideology in power and opposition influence on the contrary)
 
Back
Top Bottom