Tundu Lissu: Suala la kuongeza muda wa Rais ni ajenda ya Rais Magufuli

Tundu Lissu: Suala la kuongeza muda wa Rais ni ajenda ya Rais Magufuli

Kwahiyo wale jamaa ambao wao badala ya kujadili Matatizo ya wananchi kama vile maji,elimu ,unyonywaji unaofanywa na HESLB kupitia hako kamtindo kao ka Retention fee, bara bara nk, wao wamejikita kujadili kitu ambacho Rais hataki ni wasaliti wa wananchi na pia ni wachochezi siyo? Kwani hivi nyimbo vya dola haviwezi wachukulia hatua? Maana wanamzushia Rais pia wanazusha taharuki bila sababu
 
Mimi ningekuwa Magufuli ningeongeza muda ili kuwafunza hawa wanaoweka maneno. Amesashasema zaidi ya mara mbili ila hawakomi kumzushia. Well, I grant their wishes!
 
Unaishi nchi gani wewe? unauhakika kua rais hajawahi kukanusha kelele za yeye kuongezewa muda, ulitaka aongee vipi na aongelee wapi ili umuelewe? jitahidi kufuatilia taarifa mkuu
 
Hivi anayeongea hapa anasemaje? Kwa nini mtu asingiziwe maneno ya uongo
 
Tunapotoa tuhuma tumtendee haki tunayemtuhumu hata kama tunamchukia kiasi gani.
 
Hapo ndipo unaona upinzani tulio nao nchi hii ni wanamna hipi,wao sasahivi baada ya kuibua ajenda za maana maana wao wanaibuka na jambo kuongeza mda,yaani hata kwa akili ya kawaida Magufuri ajatumikia hata mwaka kwa muhula wake wa miaka 5,awaze kuongeza miaka mingine?lissu asubuli mpaka 2024 ndio aje na ngojera hizi sasahivi tunataka waibue hoja za kucharenge serikali kama enzi za dkt Slaa,aache mambo ya nadharia.
 
Hapo ndipo unaona upinzani tulio nao nchi hii ni wanamna hipi,wao sasahivi baada ya kuibua ajenda za maana maana wao wanaibuka na jambo kuongeza mda,yaani hata kwa akili ya kawaida Magufuri ajatumikia hata mwaka kwa muhula wake wa miaka 5,awaze kuongeza miaka mingine?lissu asubuli mpaka 2024 ndio aje na ngojera hizi sasahivi tunataka waibue hoja za kucharenge serikali kama enzi za dkt Slaa,aache mambo ya nadharia.
Enzi za m5 tena ibua hoja ww hapo.
 
Labda Lissu amuogope Jiwe kwa matumizi ya yale marisasi yake 36, ila kwa ujenzi wa hoja majukwaani Jiwe ni mwepesi kama unyoya kwa Lissu!
 
Haya Pia ni mawazo yako Nyani Sema umetumia mgongo wa Lissu kuwasilisha hili swala.

Ila kwa taarifa yenu Magufuli hana mpango wa kuongeza hata nukta ila wale visabengo pessimists wa
sio na uhakika na utukufu after JPMs regime ndo wanamshawishi.Kwa kuthibitisha hilo JPM amemweka Bashiru kama right hand mtu ambae msimamo wake ni thabiti kuhusu rais kuongeza mda.
Bashiru huyu bashiru?temea mate chini mkuu kama alikuwa na misimamo ni enzi akiwa cuf cyo ccm &cku hizi ni hamnazo kabisa
 
Hivi ni kwa nini walimchomoa?
Mim nipo nkasi, yule bwana alijikaanga mwenyew na ccm makao makuu walimpendelea kwakurudisha jina lake licha ya kutokubalika kwake ila watu walimchoka kutokana na kauli zake..
 
Bwana mkubwa sijui kwanini siku moja hajitokezi kuwakumbusha wanaopiga kelele za kumtaka aongeze muda wa utawala, kuwa yeye ni muumini wa katiba...
Ukimya upi unaozungumzia? JPM binafsi yake ametamka hatoongeza muda.. mimi binafsi yangu nimemsikia akitamka mara 2. Chama chake kupitia KATIBU MKUU kimetoa tamko kwamba hataongeza muda.

Mpaka hapo unataka kauli gani zaidi?

Hao wanaotaka aongezewe Muda ni mapenzi yao, na wanao UHURU wa kujenga hoja yoyote watakayoona inafaa. Au unataka awapangie wabunge cha kujadili. Haya leo akisema marufuku mbunge kujadili ukomo wa uraisi. Wewe ukaona sawa kesho akisema marufuku mbunge kujadili upotevu wa 1.5Trilion utaona sawa pia!?

Hata hivyo kama Mbunge akiona JPM anafaa kuongesewa muda ni dhambi? Ni kosa!? Au kavunja Katiba?
 
Raia wengi wa Tanzania wameanza kuhoji iwapo Rais John Magufuli ni buheri baada ya kutoonekana hadharani kwa wiki mbili sasa.

Magufuli alionekana mara mwisho kanisani tarehe 21 February 2021.

Aliyekuwa mpinzani wake katika Uchaguzi Mkuu wa Urais 2020 Tundu Antiphas Lissu, ameitaka Kurugenzi ya mawasiliano ya Ikulu kutoa taarifa ya iwapo Rais ni mzima ili kuwaondolea wananchi hofu.

“Afya ya Rais ni suala la umma. Kikwete alipotibiwa tezi dume Marekani tuliambiwa. Mkapa alipotibiwa nyonga Uswisi tulijulishwa. Baba wa Taifa alipougua saratani ya damu London hatukufichwa. Kwa nini kuna kigugumizi juu ya afya ya Rais Magufuli? Au ndio kila zama na kitabu chake?” Ameandika Tundu Lissu kwenye ukurasa wake wa twitter.

Hii sio mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kubaki kimya kwa muda mrefu. Ikumbukwe October mwaka 2019 hakuonekana hadharani kwa takriban siku 18 na ikawa hali ni tete kwenye mitandaoni, baadhi ya watu wakisema alikwenda Ujerumani kwa ajili ya upasuaji wa moyo. Baadae Rais alijitokeza kuwaapisha viongozi mbalimbali.

Hofu iliyoko sasa hivi inachochewa na uwepo wa janga la corona ulimwenguni na kunao wanadiriki kusema Rais anaugua Covid19.
 
Back
Top Bottom