Tundu Lissu, too late a hero!

Tundu Lissu, too late a hero!

Kuua sekta binafsi
Kubambikizia Kodi
Kesi za uhujumu uchumi
Wafungwa wa kisiasa
Kupora uchaguzi
Kuvuruga uchumi
Chuki kwa matajiri

JPM was a saddist
Wafungwa wa kisiasi ni kina nani ukiwa mwanasiasa haimaanishi uwe juu ya sheria kwamba ukivunja sheria ndio uogopwe kama mwanasiasa
 
Kuua sekta binafsi
Kubambikizia Kodi
Kesi za uhujumu uchumi
Wafungwa wa kisiasa
Kupora uchaguzi
Kuvuruga uchumi
Chuki kwa matajiri

JPM was a saddist
Uchaguzi ulikuwa halali na Magufuli alishinda uchaguzi tatizo wapinzani waliokosa sera kila walilolikosoa Magufuli alitekeleza mkabaki kupiga kelele haki za binadamu, democrasia hakuna
 
Kuua sekta binafsi
Kubambikizia Kodi
Kesi za uhujumu uchumi
Wafungwa wa kisiasa
Kupora uchaguzi
Kuvuruga uchumi
Chuki kwa matajiri

JPM was a saddist
Alivuruga uchumi wa mafisadi ila uchumi wa wananchi mbona tuliingia uchumi wa kati na mfumuko wa bei haukuwa mkubwa kama sasa wewe unasemea uchumi upi?
 
Alivuruga uchumi wa mafisadi ila uchumi wa wananchi mbona tuliingia uchumi wa kati na mfumuko wa bei haukuwa mkubwa kama sasa wewe unasemea uchumi upi?
Aliua Uchumi wa sekta binafsi sababu alihamisha ukwasi kutoka benki za biashara kwenda BOT!! So pesa kwenye mzunguko ikaisha mwisho wa siku Hela ikapotea mtaani.

Alifungia ajira miaka yote 7 hivyo kuongeza wimbi la waliokosa ajira.

alibambikizia watu madeni ya Kodi mwisho wa siku biashara nyingi sana zilifungwa na watu kupoteza ajira.

Kushuka kwa bei haimaanishi uchumi ni mzuri ila purchasing power ni ndogo. Ila ukiona mfumuko wa bei elewa kwamba mzunguko wa pesa ni mkubwa sana hivyo pesa inashuka thamani maana wengi wanayo!!
 
Uchaguzi ulikuwa halali na Magufuli alishinda uchaguzi tatizo wapinzani waliokosa sera kila walilolikosoa Magufuli alitekeleza mkabaki kupiga kelele haki za binadamu, democrasia hakuna
Sio kweli kwenye kata yangu kuanzia serikali za mtaa mpaka diwani na mbunge walipita bila kupingwa. Huku tulipiga kura ya Rais peke yake ambayo Nako walijitokeza watu 200 tu maana hakukuwa na kampeni kabisa sababu hakukuwa na uchaguzi.

Sasa utasemaje uchaguzi ni huru na haki wakati hatukuchagua viongozi wetu?
 
Wafungwa wa kisiasi ni kina nani ukiwa mwanasiasa haimaanishi uwe juu ya sheria kwamba ukivunja sheria ndio uogopwe kama mwanasiasa
Wafungwa wa kisiasa wametolewa zaidi ya 400 mpaka Sasa na Mama Samia Sasa unapoleta ujuaji wakati makamu wa huyo shetani wenu amekiri ni wafungwa wa kisiasa basi utakua hujitambui.
 
Sio kweli kwenye kata yangu kuanzia serikali za mtaa mpaka diwani na mbunge walipita bila kupingwa. Huku tulipiga kura ya Rais peke yake ambayo Nako walijitokeza watu 200 tu maana hakukuwa na kampeni kabisa sababu hakukuwa na uchaguzi.

Sasa utasemaje uchaguzi ni huru na haki wakati hatukuchagua viongozi wetu?
Kuna uchaguzi ulipita wapinzani hakulalamika kuibiwa kura embu taja?hata kipindi cha kikwete mkilalamika wamechakachua
 
Kuna uchaguzi ulipita wapinzani hakulalamika kuibiwa kura embu taja?hata kipindi cha kikwete mkilalamika wamechakachua
Umeona kokote nimeongelea kuibiwa kura 2020? Nimesema HATUKUPIGA kura sababu wagombea wote wa CCM kwenye Jimbo, kata, mtaa, na vitongoji walipita bila kupingwa. Kiufupi hata kampeni hazikufanyika Kulikua na kura Moja tu ya Urais basi!!

Sasa wapi nimeongelea kuiba kura hapo?
 
Lisu ni debe tupu lile
Akili zake ni ukoo wenu wote combined. Pole sana maana hata akijiunga CCM atapewa uanasheria mkuu huku wewe unabaki kulialia mtandaoni.

Mlitukana wapinzani wangapi? Leo wote walioenda CCM wakazawadiwa uwaziri na ubunge nyie mmebaki kutukana tu.

Mnatia huruma sana
 
Wataje hao wafungwa na makosa yao
Madiwani 14 wa Tunduma walipewa murder case ila Samia kawaachia wote.

Wanachama wawili Bariadi walipewa kesi ya mauaji na kufungwa miaka 30 ila Samia kawatoa.

Wapo kina Sanga nao walipewa murder case kule Iringa.

Kuna Bawacha zaidi ya nane pale Singida walipewa kesi ya uhujumu uchumi kisa kuwa mawakala wa Lissu.

List ni ndefu kuanzia Newala mpaka kule Tarime.
 
Hujasema kitu mkuu, soko huria ni policy yetu muda sasa.
Mengine uliyogusia ni just details in a particular field.

Sera ya majimbo bado hamjaielezea kwa kina chake na mpangilio wa kisiasa.
Soko huria Tanzania? Kasome vizuri katiba ya CCM, Tanzania inafanya Mixed economy ila Kwa Chadema ni pure capitalism serikali anabaki kuwa regulator tu with minimum interference kwenye soko.

Sera ya majimbo mbona imeelezwa vizuri sana, kwamba Rais ni mmoja ila kunakua na serikali za majimbo ambazo technically ni kama Sasa tuna halmashauri, madiwani, meya, mkuu wa mkoa ila Tuseme wanapewa nguvu zaidi Ili iwe functional government. So kinachobadilika ni resource allocation, statutory powers, autonomy, na mambo kama hayo ila serikali kuu inabaki kwenye jeshi, sera ya fedha, macro-economy na mambo machache sana ila mengi yanafanyika huko majimboni.
 
OIP.3_5yolqYLIYvqZw-oF5O_gHaE8

Masikini Tundu Lissu, amerudi toka ughaibuni sasa.
Lakini si kishujaa!

Lalamiko lake la kwanza alipoonana na Mama Samia huko Ubelgiji, ilikuwa pesayake, mafao.
Ni kweli mlo hata kwa mwanasiasa ni muhimu, ataishije?
Mambo ya siasa yakawa secondary, hayakuwa na umuhimu sana kwake.

Mama Samia kaondoa fitna za kisiasa zilizoachwa na mtangulizi wake, Magufuli.
Sasa Mbowe yuko huru, Lissu karudi Bongo.

Lakini mapokezi ya Lissu yamekuwa ile wazungu wanasema , lukewarm, vuguvugu, na si motomoto.

Hilo Lissu hajui, nimatokeo ya mama Samia kukubalika kwa wananchi walio wengi, ukilinganisha na mwendazake.
Hivyo hata sababu za kumpinga mama wazi wazi hzionekani kuwa na maana sana.

Lissu( na CHADEMA) akubali asikubali, playing field imebadilika sana.

Sasa Lissu anazunguka mikoani akilia kama Yohana Mbatizaji.
Lakini yeye hana njia yoyote ya kuonyesha, njia nzuri kuliko ya CCM na mama Samia.

Na hilo ndo paradox.
Lissu kadoda, hana jipya.
Ile confrontational style yake haina tija kwake wala kwa siasa za Tanzania.
Namshauri akubali tu kuwa a political backbencher, asuburi aone upepo kwanza.

Kwa sasa hivi Lissu is irrelevant.

Unamsema lisu wakati uhakika wa lunch huna,
 
Back
Top Bottom