Tundu Lissu: Tuna Rais Mzanzibari anayeweza kwenda Ngorongoro na kutoa Amri kwa Wanajeshi wafukuze wamasai wote

"Leo tuna miaka 60 tukiitwa Tanzania, ndiyo maana tuna rais ambaye ni mzanzibari, siyo mtanganyika. Anaweza kwenda ngorongoro akatoa amri kwa wanajeshi hawa, akasema fukuza wamasai wote ngorongoro wapeleke Msomera Handeni, 547Km kutoka ngorongoro."
Mbona nyinyi watanganyika mumetuwala miaka 57 na amri zote zinatoka kwenu, lakini watu wakisema munalalamika?
 
Angekuwa anajua mengi asingeliwa anaropoka. Angekuwa anaongea pointi. Mfano, anasema tuna Rais Mzanzibar. Sawa. Yeye anapowaongelea Wmasai, yeye Lissu ni Mmasai?
We bado mtoto wa shule huna unalojua kuhusu hi nchi endelea kusoma silabi mwambatano,cheki mlivyo na roho mbaya,ubinafsi na ukabila, Lissu anamtetea yeyote anayeonewa,kwahiyo samia anawanyanyasa wamasai kwasababu siyo mmasai,basi kama ni hivyo hafai kuwa raisi hata kwa sekunde tumkatae kwa nguvu zote
 
Lissu amesema ukweli mtupu. Sijui wamasai wamemkosea nini Rais Samia na serikali yake ya awamu ya 6.
 
Jamaa hanaga mkopo huyo mnamalizana hapohapo mchana kweupe kama alivokuwa jiwe Magufuli.
Hawa watu JPM na Lissu wanafanana sana kiuzalendo. Ila Mbowe sina uhakika akipewa asali. Lissu anaweza kuungwa mkono na wengi akiacha kumkandia JPM kila siku na kuchukua nchi. Sababu jina la JPM linawakilisha Watanzania wengi maskini.
 
Ngoja mechi ya timu yangu kubwa ya Simba iishe nikujibu.
 
Lissu katika ubora wake
 
* Police kutoa maelekezo juu ya maandamano kutumia upande mmoja wa barabara ni kawaida kwa kuwa CDM wameitisha maandamano ya AMANi
Sasa:-
Why atake shughuli zingine kusimama wkt waandamanaji wanatembea barabarani?

* Hoja kuwa Rais wetu ameuza mbuga za wanyama kwa kuwa ni Mzanzibari - huu ni uchochezi wa wazi

* Hoja ya kuwa Wamasaai wanaondolewa ktk ardhi yao haina msingi -
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…