Hilo suala la Muungano ni la siku nyingi sana toka mzee Nyerere akiwa hai, zilishaundwa tume nyingi sana, kutafuta, suluhu. Miongoni mwa tume maarufu ni tume ya Nyalali. Hakuna hoja ambaye ni ya maana kuwa, ni kitu kipya.
CDM wanashindwa kuwashawishi, watanzania kwa kuwa ni chama kisichokuwa na milengo kamili. Na, mm pia ni naona kuwa bado hakina hoja za msingi kuiondoa CCM. Chama chenyewe kimekuwa chama cha makando kando. Mfano, mwenyekiti wa chama amekuwa wa kudumu. Je, utaweza vipi kukosoa huku ukiwa, ww huna democracy. Mwaka 2015 walimsimamisha marehemu Lowasa. Lakin tayari walishawadanganya watanzania kuwa, alikuwa fisadi.
Kwa upande wangu naamini watanzania tunahitaji vyama imara, na visivyohitaji maslahi zaidi ili kuiondoa CCM. ACT na CDM sio vyama vya kutusaidia.