Tundu Lissu: Tunasikia taarifa watu wanakufa kwa Corona lakini haisemwi wazi. Serikali imerekebisha Sheria inayozuia kupeana taarifa

Tundu Lissu: Tunasikia taarifa watu wanakufa kwa Corona lakini haisemwi wazi. Serikali imerekebisha Sheria inayozuia kupeana taarifa

Toka mwanzo nimesema ya kuwa CHADEMA kila siku inaendelea kujipotezea sifa kwa Aina ya watu wanao Wategemea

Tundu Lissu leo katika Mahojiano yake na KTN anakiri kuwa Tanzania hali ya corona ni mbaya jambo ambalo sio kweli tena anakiri mbele ya Taifa Ambalo siku zote limekua likijaribu kutuchafua katika sura ya Dunia.

Tundu Lissu anailaumu serikal kuwa inaficha Taarifa za janga la corona na kusema kuwa serikali haijachukua hatua na kusema kipindi hiki cha Corona mpaka kufikia uchaguzi hali itakua Mbaya Sana.
Vip wao kama chadema hawato endesha kampeni? Ili kuokoa Wafuas wao wengi kama wanajua kuelekea kampen Hali itakua mbaya?

Kwanini anayasema haya wakati yeye alipotoka ubelgij hakuvaa mask kujikinga wala hawakutoa ushauri wowote wa tahadhari.

Pia Tundu Lissu anasema watanzania hatuchukui Tahadhari yoyote ya kuachiana nafasi vipi kwao CHADEMA hizo nafasi wao Wana achiana?, au wao hawaugui corona?

Na vipi wao kama viongozi mbona hata siku moja hawaamrishi wafuasi wao kuachiana nafasi bali wanawaamrisha Tena kwa Nguvu nyingi Wakusanyike.

Tundu Lissu kumbuka unavyozidi kuichafua nchi hata ukiwa Rais jua tu utakua na kazi mbili, moja kuisafisha na nyingine kuikuza kiuchumi kazi ambayo itakua ngumu kwako.

Naomba Wanasiasa tuwe makini sana wakati huu wa kampeni heshima ya Tanzania ni muhimu sana kuliko kitu chochote,
tuache kuropoka tuongee.

Msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Kuukimbia ukweli hakutatusaidia:

Watanzania, Kuukimbia ukweli hakutatusaidia

Heko Lissu hauko peke yako kwenye hili.

Mchana ni mchana haijalishi ni wapumbavu wangapi wangependa kwa kiasi gani kujidanganya kuwa ni usiku.

Koleo na liitwe kwa jina lake kwani koleo siyo kijiko!
 
Kuna watu wakiamka huacha akili zao ndani, Lissu amefika na anaanza kuchimba kaburi lake mwenyewe.
“Whosoever diggeth a pit shall fall therein: and he that rolleth a stone, it will return upon him.” __Proverb 26:27 (Methali 26:27)
#Lissu_Katoa_boko
 
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Kuukimbia ukweli hakutatusaidia:

Watanzania, Kuukimbia ukweli hakutatusaidia

Heko Lissu hauko peke yako kwenye hili.

Mchana ni mchana haijalishi ni wapumbavu wangapi wangependa kwa kiasi gani kujidanganya kuwa ni usiku.

Koleo na liitwe kwa jina lake kwani koleo siyo kijiko!
Hiii ndio kazi mtakayo kua nayo mpaka uchaguzi unaisha kazi yenu itakua kutetea upuuz wa Mgombea wenu
 
Huyu jamaa sidhani hata kama atapata muda wa kunadi ilani ya chama,maaana yeye kila kitu kilichoko nchi mwetu ni kibaya,sasa kama kufanya nini ,si angegombea urais huko ubeligiji amabako hakuna madhaifu

Huyu mtu hafai na watanzania inabidi waambuwe ukweli kuwa hili ni garasa,halifai hata kwa bure,mtu amejaa chuki na ubinafsi wa kutupwa ,

Huyu mtu
 
huyu jamaa janja janja nyingi sana mix na kutufokea ndo anaharibu kabisa
 
Lissu bana!!

Anamchukia Magufuli hadi anachukia nchi inayoongozwa na Magufuli. Swala la kusema hali ya Corona nchini inahuzunisha inadhihirisha hilo.

Hivi ukiwa mwanasiasa huwezi kutenganisha kile kilicho maslahi ya nchi na kile kilicho maslahi ya wanasiasa?

Na je ukiwa mwanasiasa huwezi kukubaliana na mwanasiasa mwenzio wa upande tofauti kwenye maslahi ya nchi?

Katika swala la Corona Magufuli kaongoza nchi vyema. Hili huwezi kumwondolea hata kama unamchukia vipi.
 
Nampenda lakini hamna kitu kipya cha kujivunia kutoka kwake
kwani hakuna tofauti kati ya mwanasiasa na mwanasiasa!!!!!!!...
 
Ndugu yangu Tundu Lissu, tunaomba utambue kuwa pamoja na mivutano ya kisiasa tuliyonayo nchini, linapokuja suala la kimataifa ni lazima tuwe wamoja.

Naomba nikuulize katika wale waliokuja kukupokea uwanja wa ndege hakuna hata mmoja aliyevaa taulo la usoni, je umewahi kusikia kuna mtu kafa kwa korona.

Juzi ulikuwa kwenye mkutano mkuu wa chadema na umati wa wajumbe. .Je umewahi kusikia kuna mtu anaugua korona?

Siku iliyofuata ulikuwa kwenye mkutano mkuu wa ACT. Ulipokelewa vizuri kwa shangwe na kukumbatiwa...je kuna mtu umesikia ana korona?

Ni ukosefu wa uzalendo kuituhumu nchi eti watu wanakufa na korona na takwimu zinafichwa tena kwenye vyombo vya kimataifa na cha jirani yetu ambaye ni hasimu wetu wa kiuchumi....ni ukosefu wa uzalendo kwa nchi, ni uhaini mkubwa.

Tena wewe ilitakiwa ukae karantini siku za kutosha maana umezurura sana nchi zenye korona. Usije ukatuletea korona la kibeberu hapa.

Wewe unayemshukuru Mungu amekuponya na mauti, ndiye huyo huyo aliyetuponya na Korona. Usimdhihaki Mwenyezi Mungu...

Hili limeniuzi sana

Wajumbe oyee
 
Huyo jamaa ni country pumpkin!

Tena boga la kiangazi.


Anawataka watanzania wachukue tahadhari ambazo yeye na chama chake hatuoni wakizichukua.

1.Hajakaa "eda" ya siku 14 inayotakiwa na wataalamu pindi aliporejea.

2.Mapokezi yake hayakuzingatia social distancing wala hakuna barakoa.

3.Vikao vya chama chake hakukua na barakoa wala social distancing and likely hata mikono hawakunawa.

4.Jana kule ACT kaenda wanashikana mikono na kubambiana bila tahadhari yoyote.


Huyo jamaa yenu ilifaa aungane na dereva wake kwenye matibabu ya "saikolojia" pengine moto bado ni mdogo kichwani.
 
Huyu kichwa atakuwa alikiacha ubelgiji. Kweli nchi iwe na corona kwa kiwango anachoongelea halafu wanachadema waendelee kukutana bila tahadhari yoyote!
 
Huu mtego wa Covid 19 amenasa.
Watu wa karibu wangemchomoa chezeni na wapiga kura mbona hamtuelewi? Kweli Lockdown na social distance kwa chinga?

Second mistake
 
Back
Top Bottom