Tundu Lissu: Tunasikia taarifa watu wanakufa kwa Corona lakini haisemwi wazi. Serikali imerekebisha Sheria inayozuia kupeana taarifa

Tundu Lissu: Tunasikia taarifa watu wanakufa kwa Corona lakini haisemwi wazi. Serikali imerekebisha Sheria inayozuia kupeana taarifa

Kwa nini Kenya, Kwa nini Corona, kwa nini wakati huu, Kwa nini Lissu.?
Yote haya ni maswali tafakarishi sana. Kumbuka juzi ndio kumejitokeza sakata la safari za ndege. Tusisahau ukaburu wa yule mbunge wao.
Na maswali aliyo ulizwa mi yale ya uchokonozi.
Kwa maana nyingine Kenya wanawashika mkono wapinzani wa serikali ya JMT.
 
Kama korona ipo Lissu angeshauri uchaguzi mkuu ukahairishwa. Hakuna haja ya kampeni sababu ya corona.
 
Mkuu itakuwa ni aibu kubwa sana kwa taifa letu kumpa urais mtu mwenye ubinafsi,mlopokaji,hana staha wala uvumilivu,kila linalomwijia kwa bichwa lake yeye ni kulopoka tu.

Huyu urais atausikia kwenye bomba tu,na nawaambieni huyu kwa uchu wake wa madaraka anao uwezo wa kuanzisha hata vikundi vya uasi ili tu kuvuruga amani ya nchi

Najua fika hawezi kushinda anachofanya ni kutaka kuvuruga amani yetu,kwa aliyoyafanya ughaibuni yatosha .

Sintoshangaa Lisu akianzisha vikundi vya uasi, na ni lazima atapata watu wa kumuunga mkono. Ila lazima tuangalie chanzo cha hayo yote ni kipi. Kulikuwa na katiba ya wananchi iliyotokana na rasimu ya Warioba, katiba ile ilichezewa sana na wanaccm, na bado hayo maoni yaliyochakuchuliwa kuwa katiba pendekezwa rais huyu aliiogomea katiba ile. Kumbe lengo la rais huyu ni kutaka kuongoza nchi hii kwa kutubuzs atakavyo kwa katiba hii yenye mapungufu. Je unadhani kila mtu anaweza kukubali hilo?

Kama yatatokea machafuko nchi hii, basi hayataletwa na Lisu tu, bali hata Magufuli atakuwa ni sehemu ya machafuko hayo. Fumbieni macho uhayawani, wakati tumeona wazi kuwa toka Magufuli aingie madarakani, box la kura linabakwa kimachomacho.
 
Sass hivi mtatafuta vikosa vya kuongea vya Mtu huyu kila siku Kama Mafarisayo walivyofanya dhidi Ya Yesu.

Kuna majibu mengine yanatokana na Hali halisi.

Kwa mfano unaweza kusema korona ipo kwa sababu hatupimwi hivyo siwezi kuthibitisha Kama haipo.

Ama ukajibu haipo kwa sababu hatupimwi hivyo siwezi kuthibitisha Kama ipo.
Hali halisi.
 
Mikutano ya juzi ya Chadema hakuna aliyevaa barakoa wala tahadhari yeyote akiwemo Lissu. Kuna mambo jamii yako ikikubaliana nayo na wewe ni sehemu yake. Swala la uzalendo si issue ya Magufuli hata awe anamchukia kiasi gani. Chuki ikipitiliza inaleta upofu hata kwenye mambo ya msingi.
 
Jamani jamani kama kuna corona kiasi hicho Lissu si angeanza kuvaa barakoa kuanzia siku alipofika hadi alipohudhulia mkutano mkuu wa kumteua kuwa mgombea urais daah.
Hata kuchukua form wote wataenda bila barakoa. Wakivaa kuanzia sasa ndio tutajua unafiki wa wanasiasa.
 
Alafu mtambue kitu kimoja,
Lissu mmempa attention kubwa kuliko uwezo wake , Hilo tu.
Wewe acha bwana uwezo wa Lissu kutokufa baada ya kumwagiwa magazine nzima ya risasi Ni mkubwa mno.
Huyu Mtu Ni mgumu kufa.
Na hicho ndio kinatufanya tumpe attention.

Bado kuhusu suala suala la uwezo wa kiakili anawashinda wengi mno hata jiwe.
 
Naisubiria kwa hamu hio siku,hawa watu hawapo serious kabisa. Halafu suala lacorona wangeachana nalo kabisaa ni ishu kubwa
Hata kuchukua form wote wataenda bila barakoa. Wakivaa kuanzia sasa ndio tutajua unafiki wa wanasiasa.
 
Hiii ndio kazi mtakayo kua nayo mpaka uchaguzi unaisha kazi yenu itakua kutetea upuuz wa Mgombea wenu

Hatutetei upuuzi ila hadi uchaguzi unaisha tutakuwa tunamtetea mgombea yeyote:

IMG_20200804_210728_515.jpg


Kwamba ni Magufuli, Membe, Lissu, Lipumba n.k, hapendwi mtu hapa!

Tunataka taifa lenye kuzingatia kweli, haki na uhuru kamili wa watu wake.

Kwa hakika ni wapuuzi kama nyie peke yenu mnaoendekeza njaa mnaoweza kuwa na ujasiri wa kujidanganya kuwa hata ukweli huo eti hamuuoni.

Mwelekezeni mgombea wenu nini watu wanataka na atapata uungwaji mkono wote.

Kuukimbia ukweli, udikteta uchwara, janja janja, uongo uongo, ficha ficha, fitina fitina, hadaa hadaa na vyote vya namna hiyo havitakaa vimsaidie.
 
Ndugu yangu Tundu Lissu, tunaomba utambue kuwa pamoja na mivutano ya kisiasa tuliyonayo nchini, linapokuja suala la kimataifa ni lazima tuwe wamoja.

Naomba nikuulize katika wale waliokuja kukupokea uwanja wa ndege hakuna hata mmoja aliyevaa taulo la usoni, je umewahi kusikia kuna mtu kafa kwa korona.

Juzi ulikuwa kwenye mkutano mkuu wa chadema na umati wa wajumbe. .Je umewahi kusikia kuna mtu anaugua korona?

Siku iliyofuata ulikuwa kwenye mkutano mkuu wa ACT. Ulipokelewa vizuri kwa shangwe na kukumbatiwa...je kuna mtu umesikia ana korona?

Ni ukosefu wa uzalendo kuituhumu nchi eti watu wanakufa na korona na takwimu zinafichwa tena kwenye vyombo vya kimataifa na cha jirani yetu ambaye ni hasimu wetu wa kiuchumi....ni ukosefu wa uzalendo kwa nchi, ni uhaini mkubwa.

Tena wewe ilitakiwa ukae karantini siku za kutosha maana umezurura sana nchi zenye korona. Usije ukatuletea korona la kibeberu hapa.

Wewe unayemshukuru Mungu amekuponya na mauti, ndiye huyo huyo aliyetuponya na Korona. Usimdhihaki Mwenyezi Mungu...

Hili limeniuzi sana

Wajumbe oyee
Yeye amesema amesikia sikia huko kuna watu wanakufa.
Mbona unatka kulisha watu maneno kuwa yeye ndio kasema?
 
Huyu lisu ni mpuuzi wakenya wanavyotupiga vita yeye ndio ameona wazuri was kuungana nao.
Shenzi kabisa
 
Huyu kichwa atakuwa alikiacha ubelgiji. Kweli nchi iwe na corona kwa kiwango anachoongelea halafu wanachadema waendelee kukutana bila tahadhari yoyote!
Huenda sio Tundulisu yule mtanzania wetu labda mabeberu wamembadilisha [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Lisu hayupo sawa ana overconfidence, jazba na hasira sana, kiasi zina affect huwezo wake wa kufikiri vizuri kabla ajaongea, na mpka uchaguzi unaisha jamaa anaweza kuja kugeuka bonge la kituko.
 
Huenda sio Tundulisu yule mtanzania wetu labda mabeberu wamembadilisha [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kweli kabisa mi mwenyewe naanza kuliona hili maana kuna mambo anaongea yanatia mashaka juu ya afya yake ya akili
 
Unajua madhara ya yeye kutoa kauli ile kiuchumi. Hatuwezi kuipigania upinzani kwa kubomoa misingi ya nchi. Hili hapana.

..na unajua madhara ya kuwaambia wananchi covid19 imekwisha wakati hujui kama imekwisha?
 
Back
Top Bottom