Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 122,494
- 96,074
Inaonekana sana, sema tu huyo uliye muuliza chombo chake pekee cha kupata habari ni tbc
Kwani KTN haionekani Tanzania? Shikamoo mkuu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani KTN haionekani Tanzania? Shikamoo mkuu.
Unadhani amefanya hivyo kwa kupenda ? Subirini na nyie mtakapokuwa wapinzani mtaelewa !
Hata mzee makamba aliuelewa ubatizo wa moto baadae Sana.
KTN wakuu saa 8 kamili ama?
Acha niache shughuli zangu nimsikilize Lissu, sijawahi kuchoka kumsikiliza LISSU.
Jiulize tu...mbona bado wanaendelea kukusanyana?Jamani jamani kama kuna corona kiasi hicho Lissu si angeanza kuvaa barakoa kuanzia siku alipofika hadi alipohudhulia mkutano mkuu wa kumteua kuwa mgombea urais daah.
Chama cha watu wa kasikazi,tunawasubiri
Unajua madhara ya yeye kutoa kauli ile kiuchumi. Hatuwezi kuipigania upinzani kwa kubomoa misingi ya nchi. Hili hapana.
Muda mfupi mh Tundu Lissu atakuwa mbashara kuanzia saa 8: 00 mchana,Vituo vitakavyokuwa live Ni @standardKenya na @KTNNews, hii Ni kwamjibu wa Tumaini Makene
======
Mwandishi: Ulikuwaje mchakato wa kupona ulikuwaje?
Lissu: Asante kwa kushiriki kwenye kipindi chenu na kuongea na wananchi wa Kenya kuhusu mambo ya Tanzania, Nimekaa miezi minne Nairobi, nilipata huduma nzuri sana za kiafya kutoka kwa madaktari wa Kenya, nina damu nyingi ya wakenya inatembea kwenye mishapa yangu ya damu, nawashukuru watu wa Kenya kwa kuniangalia kwa miezi minne na baadae nikaenda Ubelgiji kutibiwa kwa miezi 11.
Mwandishi: Ulipoteza kiti chako bungeni wakati uko kwenye matibabu, ilikuwa halali kisiasa au kisheria?
Lissu: Wanasema sikuwepo bungeni lakini kila mtu anajua sikuwepo bungeni kwa sababu ya jaribio la mauaji September 2017. Wale waliojaribu kuniua kwa bunduki waliposhindwa ndio wakaamua kunipokonya siti yangu bungeni. Haikubaliki kibinadamu na kisheria labda kisiasa kwenye hesabu zao za siasa.
Mwandishi: Upinzani bado haujaungana kukikabili chama tawala cha CCM, kuna uwezekano wowote upinzani kuongea kwenye sauti moja?
Lissu: Nafikiri kwa upinzani umemaanisha chama changu cha CHADEMA na ACT- WAzalendo(Lissu amekatika). Tunafanyia kazi hilo, kuna baadhi ya mambo ya kisheria yanatakiwa kufanyiwa kazi na mitego ya kisheria.(Lissu amekatika).
Mwandishi: Tanzania imekuwa haitoi namba rasmi za Corona toka April 19, wapiga kura wakienda kupiga kura, tunawezaje kuwalinda wakati wa mchakato wa upigaji kura, kitu gani kitakuwa tofauti kwenye mchakato ambacho kitawalinda?
Lissu: Hili ni suala ambalo linatufikirisha, tuko katikati ya gonjwa la mlipuko lakini serikali yetu imesema wazi kwa dunia kwamba hakuna corona hivyo Rais aliposema hakuna shida wananchi wamefata, watu hawaachi nafasi baina ya mtu na mtu, litakuwa tatizo kubwa kutoka sasa mpaka uchaguzi mkuu. Napenda kuwaomba wananchi wa Tanzania kuamika silika zao na wafanye maamuzi yao hasa kutokana na Rais kutolikubali hili gonjwa.
Nawaomba wananchi wapeane nafasi, wavae barakoa, wanawe mikono na kufanya vyote ambavyo wataalam wamewaelekeza kuepuka maambukizi ya korona.
Mwandishi: Tukiongelea Covid19, unaweza kutupa picha gani kutoka nchini kwako?
Ni picha inayohuzunisha, tunasikia taarifa watu wanakufa kwa corona lakini haviongelewi wazi, serikali imerekebisha sheria ya mitandao inayozuia kupeana taarifa kuhusu huu ugonjwa, ukisema unavunja sheria na unaweza kufungwa. Wananchi wafanye maamuzi yao na wasisikilize ushauri mbaya wa watu kutoka serikali kwamba hamna tatizo, corona inaua na ipo Tanzania.
Mwandishi: Unaongeleaje haki za binadamu?
Lissu: Rekodi ya haki za binadabu Tanzania ni janga, hii miaka mitano tumeona historia mbaya zaidi katika historia yetu yote.(Lissu amekatika)
Kama ni mfa maji, mbona wewe mleta Post ,unatapatapa?Best loser anajipya gani? Huyu lissu ni mfa maji,hana atakachoambulia kwenye uchaguzi wa October, akijitahidi sana ni 5% ya kura zote
Kutokuvaa kwao barakoa hakuuzuii Ukweli kuwa Corona bado ipo! Tuache kuwa wajinga kupindukia.Mikutano ya juzi ya Chadema hakuna aliyevaa barakoa wala tahadhari yeyote akiwemo Lissu. Kuna mambo jamii yako ikikubaliana nayo na wewe ni sehemu yake. Swala la uzalendo si issue ya Magufuli hata awe anamchukia kiasi gani. Chuki ikipitiliza inaleta upofu hata kwenye mambo ya msingi.
Huyu Lissu kila siku ana kosa kubwa la kwanza. Kesho asubuhi hatakua na kosa lolote.
Wajinga ni nani hapa!? Nyie mnaoamini Kuna Korona na bado mnalundika na kuandamana au hawa wanaoamini hakuna Korona na maisha yanaendelea!Kutokuvaa kwao barakoa hakuuzuii Ukweli kuwa Corona bado ipo! Tuache kuwa wajinga kupindukia.