Tundu Lissu: Tunasikia taarifa watu wanakufa kwa Corona lakini haisemwi wazi. Serikali imerekebisha Sheria inayozuia kupeana taarifa

Tundu Lissu: Tunasikia taarifa watu wanakufa kwa Corona lakini haisemwi wazi. Serikali imerekebisha Sheria inayozuia kupeana taarifa

Salaam ziwafikie wote walio furahia kushambuliwa kwa mh Lissu.
Unadhani amefanya hivyo kwa kupenda ? Subirini na nyie mtakapokuwa wapinzani mtaelewa !

Hata mzee makamba aliuelewa ubatizo wa moto baadae Sana.
 
Jamani jamani kama kuna corona kiasi hicho Lissu si angeanza kuvaa barakoa kuanzia siku alipofika hadi alipohudhulia mkutano mkuu wa kumteua kuwa mgombea urais daah.
Jiulize tu...mbona bado wanaendelea kukusanyana?
 
Unajua madhara ya yeye kutoa kauli ile kiuchumi. Hatuwezi kuipigania upinzani kwa kubomoa misingi ya nchi. Hili hapana.

Je haya malalamiko yako umemnukuu vizuri alichosema? Isije ikawa unaleta maelezo yako kwa uelewa wako na maneno uliyobeba humu mitandaoni. Kama kweli kasema hiki unacholalamikia ni kweli atakuwa hakufanya sawa, kwani angeweza kutoa jibu ambalo halina madhara kwa nchi.

Ninadhani katika hilo hata vyombo vya habari vya humu ndani haviko huru, ndio maana toka amefika hapa nchini hakuna chombo chochote cha habari kimemuhoji, kibaya zaidi kila akiongea sauti yake inakatwa. Sasa kama vyombo vya habari vinakuwa biased, acha wengine wamuhoji, na yeye atakachofanya ni kuchomoa battery.
 
Muda mfupi mh Tundu Lissu atakuwa mbashara kuanzia saa 8: 00 mchana,Vituo vitakavyokuwa live Ni @standardKenya na @KTNNews, hii Ni kwamjibu wa Tumaini Makene

======
Mwandishi: Ulikuwaje mchakato wa kupona ulikuwaje?

Lissu: Asante kwa kushiriki kwenye kipindi chenu na kuongea na wananchi wa Kenya kuhusu mambo ya Tanzania, Nimekaa miezi minne Nairobi, nilipata huduma nzuri sana za kiafya kutoka kwa madaktari wa Kenya, nina damu nyingi ya wakenya inatembea kwenye mishapa yangu ya damu, nawashukuru watu wa Kenya kwa kuniangalia kwa miezi minne na baadae nikaenda Ubelgiji kutibiwa kwa miezi 11.

Mwandishi: Ulipoteza kiti chako bungeni wakati uko kwenye matibabu, ilikuwa halali kisiasa au kisheria?

Lissu: Wanasema sikuwepo bungeni lakini kila mtu anajua sikuwepo bungeni kwa sababu ya jaribio la mauaji September 2017. Wale waliojaribu kuniua kwa bunduki waliposhindwa ndio wakaamua kunipokonya siti yangu bungeni. Haikubaliki kibinadamu na kisheria labda kisiasa kwenye hesabu zao za siasa.

Mwandishi: Upinzani bado haujaungana kukikabili chama tawala cha CCM, kuna uwezekano wowote upinzani kuongea kwenye sauti moja?

Lissu: Nafikiri kwa upinzani umemaanisha chama changu cha CHADEMA na ACT- WAzalendo(Lissu amekatika). Tunafanyia kazi hilo, kuna baadhi ya mambo ya kisheria yanatakiwa kufanyiwa kazi na mitego ya kisheria.(Lissu amekatika).

Mwandishi: Tanzania imekuwa haitoi namba rasmi za Corona toka April 19, wapiga kura wakienda kupiga kura, tunawezaje kuwalinda wakati wa mchakato wa upigaji kura, kitu gani kitakuwa tofauti kwenye mchakato ambacho kitawalinda?

Lissu: Hili ni suala ambalo linatufikirisha, tuko katikati ya gonjwa la mlipuko lakini serikali yetu imesema wazi kwa dunia kwamba hakuna corona hivyo Rais aliposema hakuna shida wananchi wamefata, watu hawaachi nafasi baina ya mtu na mtu, litakuwa tatizo kubwa kutoka sasa mpaka uchaguzi mkuu. Napenda kuwaomba wananchi wa Tanzania kuamika silika zao na wafanye maamuzi yao hasa kutokana na Rais kutolikubali hili gonjwa.

Nawaomba wananchi wapeane nafasi, wavae barakoa, wanawe mikono na kufanya vyote ambavyo wataalam wamewaelekeza kuepuka maambukizi ya korona.

Mwandishi: Tukiongelea Covid19, unaweza kutupa picha gani kutoka nchini kwako?

Ni picha inayohuzunisha, tunasikia taarifa watu wanakufa kwa corona lakini haviongelewi wazi, serikali imerekebisha sheria ya mitandao inayozuia kupeana taarifa kuhusu huu ugonjwa, ukisema unavunja sheria na unaweza kufungwa. Wananchi wafanye maamuzi yao na wasisikilize ushauri mbaya wa watu kutoka serikali kwamba hamna tatizo, corona inaua na ipo Tanzania.

Mwandishi: Unaongeleaje haki za binadamu?

Lissu: Rekodi ya haki za binadabu Tanzania ni janga, hii miaka mitano tumeona historia mbaya zaidi katika historia yetu yote.(Lissu amekatika)



Mbona ume - upload video ambayo ni irrelevant na maudhui ya mada?

Please, Fanya marekebisho ikibidi iondoe kabisa hii
 
Best loser anajipya gani? Huyu lissu ni mfa maji,hana atakachoambulia kwenye uchaguzi wa October, akijitahidi sana ni 5% ya kura zote
Kama ni mfa maji, mbona wewe mleta Post ,unatapatapa?
 
Mikutano ya juzi ya Chadema hakuna aliyevaa barakoa wala tahadhari yeyote akiwemo Lissu. Kuna mambo jamii yako ikikubaliana nayo na wewe ni sehemu yake. Swala la uzalendo si issue ya Magufuli hata awe anamchukia kiasi gani. Chuki ikipitiliza inaleta upofu hata kwenye mambo ya msingi.
Kutokuvaa kwao barakoa hakuuzuii Ukweli kuwa Corona bado ipo! Tuache kuwa wajinga kupindukia.
 
Namfuatilia kwa karibu sana Lissu, kwa hoja zake, hulka zake, na matamshi yake. Huwa namfuatilia kwenye YouTube Lissu kabla na baada ya kupata misukosuko nawaona ni watu wawili tofauti sana.

Yule wa mwanzo alikuwa mwenye subira na mtulivu na aliyeweza kujenga hoja za kushawishi na si mwepesi wa kupanic na kupoteza focus.

Huyu wa sasa amepata tabia za kuropoka na kukosa subira, na asiyekuwa makini katika kuhakikisha havunji sheria kwa makusudi.

Nafahamu majanga makubwa yaliyompata ndugu yetu, na nampa pole sana na tunamshukuru Mungu kwa kumuokoa ndugu yetu Lissu.

Wasiwasi wangu. Je mgombea wetu Lissu ana utimamu wa akili baada ya kupitia hii misukosuko? Maana hili ni takwa la kikatiba...


Wajumbe oyee
 
Lissu anajua anachosema, Sidhani kwa nafasi yake anaweza kuongea tu alimradi ameongea, Ana ushahidi wa anachoongea, kumbuka Lissu ni kiongozi anaetafuta ridhaa ya raia kuongoza nchi, Inawezekanaje adanganye na anajua walio upande mwingine wanasubiri akosee kidogo tu wamshambulie kisiasa?
 
tatizo Tundu Lisu ni muongo sana mpaka yeye mwenyewe anajichanganya. Hili ni janga kwa taifa viongozi wengi wa upinzani wanaishi kwa siasa za matukio na maigizo.
 
Hivi mabilioni ya pesa yaliyochangwa na watu mbalimbali zimefanya nini???

Hii serikali kwa kula michango na rambirambi haichoki......

Takukuru ni wepesi kuchunguza michango ya chadema lkn hawatachunguza huu ufisadi wa ccm na serikali yake
 
Huyu Lissu kila siku ana kosa kubwa la kwanza. Kesho asubuhi hatakua na kosa lolote.


Mfunzeni mdomo wake uwe tofauti na msiempenda.

Maana yeye kila kitu lazima akitolee povu. 🙏
 
U
Kutokuvaa kwao barakoa hakuuzuii Ukweli kuwa Corona bado ipo! Tuache kuwa wajinga kupindukia.
Wajinga ni nani hapa!? Nyie mnaoamini Kuna Korona na bado mnalundika na kuandamana au hawa wanaoamini hakuna Korona na maisha yanaendelea!
 
Back
Top Bottom