Tundu Lissu: Tunasikia taarifa watu wanakufa kwa Corona lakini haisemwi wazi. Serikali imerekebisha Sheria inayozuia kupeana taarifa

Tundu Lissu: Tunasikia taarifa watu wanakufa kwa Corona lakini haisemwi wazi. Serikali imerekebisha Sheria inayozuia kupeana taarifa

ndio maana mnakufa kwa ukimwi kwa maana hata condom kuvaa pia ni shida...tutakufa kama kuku
 
Muda mfupi mh Tundu Lissu atakuwa mbashara kuanzia saa 8: 00 mchana,Vituo vitakavyokuwa live Ni @standardKenya na @KTNNews, hii Ni kwamjibu wa Tumaini Makene

======
Mwandishi: Ulikuwaje mchakato wa kupona ulikuwaje?

Lissu: Asante kwa kushiriki kwenye kipindi chenu na kuongea na wananchi wa Kenya kuhusu mambo ya Tanzania, Nimekaa miezi minne Nairobi, nilipata huduma nzuri sana za kiafya kutoka kwa madaktari wa Kenya, nina damu nyingi ya wakenya inatembea kwenye mishapa yangu ya damu, nawashukuru watu wa Kenya kwa kuniangalia kwa miezi minne na baadae nikaenda Ubelgiji kutibiwa kwa miezi 11.

Mwandishi: Ulipoteza kiti chako bungeni wakati uko kwenye matibabu, ilikuwa halali kisiasa au kisheria?

Lissu: Wanasema sikuwepo bungeni lakini kila mtu anajua sikuwepo bungeni kwa sababu ya jaribio la mauaji September 2017. Wale waliojaribu kuniua kwa bunduki waliposhindwa ndio wakaamua kunipokonya siti yangu bungeni. Haikubaliki kibinadamu na kisheria labda kisiasa kwenye hesabu zao za siasa.

Mwandishi: Upinzani bado haujaungana kukikabili chama tawala cha CCM, kuna uwezekano wowote upinzani kuongea kwenye sauti moja?

Lissu: Nafikiri kwa upinzani umemaanisha chama changu cha CHADEMA na ACT- WAzalendo(Lissu amekatika). Tunafanyia kazi hilo, kuna baadhi ya mambo ya kisheria yanatakiwa kufanyiwa kazi na mitego ya kisheria.(Lissu amekatika).

Mwandishi: Tanzania imekuwa haitoi namba rasmi za Corona toka April 19, wapiga kura wakienda kupiga kura, tunawezaje kuwalinda wakati wa mchakato wa upigaji kura, kitu gani kitakuwa tofauti kwenye mchakato ambacho kitawalinda?

Lissu: Hili ni suala ambalo linatufikirisha, tuko katikati ya gonjwa la mlipuko lakini serikali yetu imesema wazi kwa dunia kwamba hakuna corona hivyo Rais aliposema hakuna shida wananchi wamefata, watu hawaachi nafasi baina ya mtu na mtu, litakuwa tatizo kubwa kutoka sasa mpaka uchaguzi mkuu. Napenda kuwaomba wananchi wa Tanzania kuamika silika zao na wafanye maamuzi yao hasa kutokana na Rais kutolikubali hili gonjwa.

Nawaomba wananchi wapeane nafasi, wavae barakoa, wanawe mikono na kufanya vyote ambavyo wataalam wamewaelekeza kuepuka maambukizi ya korona.

Mwandishi: Tukiongelea Covid19, unaweza kutupa picha gani kutoka nchini kwako?

Ni picha inayohuzunisha, tunasikia taarifa watu wanakufa kwa corona lakini haviongelewi wazi, serikali imerekebisha sheria ya mitandao inayozuia kupeana taarifa kuhusu huu ugonjwa, ukisema unavunja sheria na unaweza kufungwa. Wananchi wafanye maamuzi yao na wasisikilize ushauri mbaya wa watu kutoka serikali kwamba hamna tatizo, corona inaua na ipo Tanzania.

Mwandishi: Unaongeleaje haki za binadamu?

Lissu: Rekodi ya haki za binadabu Tanzania ni janga, hii miaka mitano tumeona historia mbaya zaidi katika historia yetu yote.(Lissu amekatika)



Ameongea ukweli, na ukweli mtupu.
 
Huko ni kuwacheza shere na kuwadhihaki waliokufa au kufiwa na ndugu au jamaa kwenye janga hili.

Kauli yako ni yenye kuashiria dharau kwao ambapo kwa hakika ni ujinga uliopitiliza. Samahani lakini sikuweza kupata namna nyingine ya kukuelezea zaidi ya hiyo.

Pole lakini.
Acheni sound. Huenda ipo ila sio kwa kiwango mnachotaka kuwa aminisha wakenya. Endeleeni kuwa na ajenda moja na wakenya siku moja mtayaona majibu ya watanzania
 
Matusi na kashifa hazijengi mkuu, but siwezi kuwalaumu maana mgombea wenu break mdomoni kwake,chochote kikija kwake ni kuropoka tu


Turudi kwenye hoja,lissu hafai kuwa rais na hata kuwa kwa vyovyote vile iwavyo,huyu mtu no mbinafsi na mlafi wa madaraka na ataigawa nchi yetu na huenda hata ikaingia kwenye machafuko sababu ya huyu lissu

Watanzania hawapendi promo,wanapendA rais mchapa kazi kama ilivyo kwa JPM,

Harafu itakuwa ni maajabu kwa chama ambacho hakina uhakika wa kupata japo five MPs kutegemea kutoa rais wa kuiongoza nchi
Safari hii mmekwisha , Wanafiki wakubwa nyie !
 
Kwa hiyo kesho akifa kwa corona, Tanzania ndo basi tena siyo?
Mkuu watakuwepo, Ila si huyo anayehubiri uwepo wa Corona nchini na vifo viingi Sana,

Kila mtu ana kipaji chake, huyu mwenzetu, Mungu kampa kipaji cha uongeaji usio na mpangilio bila kujali lipi linafaa kusemwa Kwa Wakati gani na lipi Kwa muda upi,

Watanzania tumepata mgombea Uraisi wa ajabu Kwa mara ya Kwanza tangu uhuru wa nchi yetu

Huyu ni wa kupingwa na kila mtu mwenye akiri timamu
 
Safari hii mmekwisha , Wanafiki wakubwa nyie !
Mmekwisha ninyi mkuu,CCM chama dola,tutawanyoa kwa chupa mwaka huu na huyo mgonjwa wenu atawakimbieni tena,

Urais sio matako kwa kila mtu lazima awe nayo liambieni dubwana lenu limekwama
 
Mkuu watakuwepo, Ila si huyo anayehubiri uwepo wa Corona nchini na vifo viingi Sana,

Kila mtu ana kipaji chake, huyu mwenzetu, Mungu kampa kipaji cha uongeaji usio na mpangilio bila kujali lipi linafaa kusemwa Kwa Wakati gani na lipi Kwa muda upi,

Watanzania tumepata mgombea Uraisi wa ajabu Kwa mara ya Kwanza tangu uhuru wa nchi yetu

Huyu ni wa kupingwa na kila mtu mwenye akiri timamu
Kwa hiyo na wewe umejitoa ufahamu kwamba Tanzania hakuna corona na hakuna wanaokufa si ndiyo?
 
anatatizo kubwa na kisaikolojia ambalo huwapata watu wa aina kama yake kibaya zaidi hata watu wake wa karb hawamwambii....

fikria tu kesho tuamke tunarais anaitwa tl.. unadhani nn kitatokea???
Haiwezi tokea, kwahiyo sitaki nichoshe akili yangu kifikiria
 
Mmekwisha ninyi mkuu,CCM chama dola,tutawanyoa kwa chupa mwaka huu na huyo mgonjwa wenu atawakimbieni tena,

Urais sio matako kwa kila mtu lazima awe nayo liambieni dubwana lenu limekwama
Kila siku siyo Jumapili
 
Sasa Kama haipo tunajihadhari nayo kwa kipi? Hata hivyo issue yangu haikuwa corona bali mtu anajejifanya kwamba bila yeye hakuna Tanzania
Hapo alijilinganisha na wagombea wengine
 
Petty issue_Maendeleo is increased productivity ya watu, universal and improved health systems,Quality and inclusive education system and not petty issue like taa za barabarani au kununua ndege kwa keshi
Kwani kwenye hivyo ulivyotaja wewe kipi hakifanyiwi ongezeko la uzalishaji
 
Kutokuvaa kwao barakoa hakuuzuii Ukweli kuwa Corona bado ipo! Tuache kuwa wajinga kupindukia.
Naona umekubali kimya kimya kwamba korona ni ugonjwa wa kawaida tu inabidi tuzoee kuishi nao.
 
Hata kama corona bado ipo hakutakiwa kukiri wazi. Hii kauli itampa wakati mgumu kwenye kampeni. Atafanyaje kampeni kama kuna corona? Halafu anatakiwa asome upepo, watanzania kwa sasa wanafurahia maisha ya kuishi bila hofu ya corona. Watu hatupendi kuvaa mibarakoa hivyo kutuambia bado corona ipo ni kutukosesha furaha. Nashauri aachane kabisa na habari za korona zitamshushia umaarufu.
Hiki kweli kizazi cha nyoka!
TL sio mjinga kama wajinga unaowafahamu na unaowaelewa wewe!
TL nyeupe nyeupe, hawezisema nyeusi wakati ni nyeupe. Heri akose hiyo kura yako kwa kukataa kusema uwongo lakini atapata kura za watu kama sisi tusiopenda uwongo hata kama tutakuwa 100 tu!
 
Lissu anajua anachosema, Sidhani kwa nafasi yake anaweza kuongea tu alimradi ameongea, Ana ushahidi wa anachoongea, kumbuka Lissu ni kiongozi anaetafuta ridhaa ya raia kuongoza nchi, Inawezekanaje adanganye na anajua walio upande mwingine wanasubiri akosee kidogo tu wamshambulie kisiasa?
Ndio ivyo, akili imeshamruka, kutoka nusu kifo sio mchezo mzee nati haziwezi kuwa sawa Kama Mwanzo. Lissu is going insane. Sio Jambo zuri kumtokea binadamu lakini huo ndio ukweli.
 
Back
Top Bottom