Tundu Lissu uongozi ni hekima wewe huna karama hiyo ,,,

Tuleteee matusi ya Lissu otherwise hizi ni chuki zako tu dhidi yake
 
Tundu lisu na magufuli wanafanana kitabia kabisa sema mmoja alikuwa Rais na huyo upinzani, Tundu lisu huwa hana break ya mdomo wala busara, anahitaji mtu juu yake wa kumpa amri, hivi hivi lazima aharibu, pia ni mubishi flani hivi
Nakuunga mkono. Nashangaa kwanini Magufuri hakuliona Hilo. Magufuri angejenga urafiki na Lissu na sio uadui.
 
Umesema ni gaidi,sawa.Sasa gaidi gani katika dunia hii ambaye ni mtu hatari wa kuweza kuharibu,kuleta taharuki,kuua na kusumbua jamii akikamatwa anaambiwa aombe msamaha tu(aombe Pooh) ili aachiwe huru?Je,akileta madhara baada ya kuachiwa huru?Msitucheze shere.Muwe wa kweli.Aachiwe kwa haki au afungwe kwa hila.Baaasiii!
 
Tundu lisu na magufuli wanafanana kitabia kabisa sema mmoja alikuwa Rais na huyo upinzani, Tundu lisu huwa hana break ya mdomo wala busara, anahitaji mtu juu yake wa kumpa amri, hivi hivi lazima aharibu, pia ni mubishi flani hivi
Ukiwa na akili ndogo hautaweza kumuelewa tundu lisu, Magufuli hata darasa la pili F walikuwa wanamuelewa, kumfanisha Tundu lisu na Magufuli ni kushindwa kutumia akili yako vizuri
 
Lissu hana maana kabisa tena hafai. Nakumbuka alitoa siri kuwa jiwe hakuwa na cheti cha kuzaliwa Lissu hafai. Lissu akaja akatoa siri kuwa Jiwe alikwibia Machinga kupitia vitambulisho feki Lissu hafai. Akaja akasema kuwa Jiwe ni Dikteta uchwara.
[emoji23][emoji23] kweli kabisa acha tuwaunge mkono Lisu Hana maana kabisa
 
Ukiwa na akili ndogo hautaweza kumuelewa tundu lisu, Magufuli hata darasa la pili F walikuwa wanamuelewa, kumfanisha Tundu lisu na Magufuli ni kushindwa kutumia akili yako vizuri
Wote tu Wana factors nyingi za kufanana sema Tundu lisu alikuwa anajua sana sheria na kingereza mkuu, ila mengine karibia wafanane
 
Wote tu Wana factors nyingi za kufanana sema Tundu lisu alikuwa anajua sana sheria na kingereza mkuu, ila mengine karibia wafanane
Sidhani kama wanafanana.Sidhani.Bado nachunguza hilo.Ila akili inaniambia hapana,hawafanani.
 
WANAOFAA KUWA VIONGOZI NI HAWA HAPA: Yule aliyeagiza Wakurugenzi kukimbia ofisi pindi Wapinzani wanarejesha fomu za kugombea. Yule aliyetamka uchaguzi wa serikali za mitaa uwe kijani tu nchi yote. Wale waliosema tutamlazimisha awe Rais wa Maisha atake asitake. Yule aliyewaweka bungeni wabunge 19 wasiokuwa na Chama. Yule aliyenunua ndege 11 bila bajeti kupita bungeni. Yule aliyejenga uwanja wa ndege bila bajeti kupita bungeni. Hawa ndio viongozi wanaofaa.
 
Lissu hana maana kabisa tena hafai. Nakumbuka alitoa siri kuwa jiwe hakuwa na cheti cha kuzaliwa Lissu hafai. Lissu akaja akatoa siri kuwa Jiwe alikwibia Machinga kupitia vitambulisho feki Lissu hafai. Akaja akasema kuwa Jiwe ni Dikteta uchwara.
Hawa jamaa wanamuogopa Lisu
Lissu hana maana kabisa tena hafai. Nakumbuka alitoa siri kuwa jiwe hakuwa na cheti cha kuzaliwa Lissu hafai. Lissu akaja akatoa siri kuwa Jiwe alikwibia Machinga kupitia vitambulisho feki Lissu hafai. Akaja akasema kuwa Jiwe ni Dikteta uchwara.
Wananzengo mnavyomuogopa Lissu ngoja atangazwe na Tume kwa Raisi wa 7 mtalala na viatu
 
Lissu hana busara za uongozi na ni kama mtu mwenye shida ya afya ya akili! Na huwa haambiwi ukweli anakera sana. Ndiyo maana hata Mzee Mtei aliwahi kumsema alivyothubutu kuzungumza upuuzi kuhusu Baba wa Taifa.

Katika akili ya kawaida, huwezi kutaka muafaka wa mazungumzo kwa mashariti ya nje ya meza ya mazungumzo. Wajifunze kwa Mwalimu Nyerere na TANU wakati uchaguzi wa kura tatu na Mandela hata baada ya kutoka gerezani alivyounda Tume ya Askofu Tutu. Nimejiuliza hivi kama Lissu ndiyo angekuwa Mzee Mandela au Mwalimu Nyerere si wangenyonga wazungu wote baada ya Uhuru? Lakini busara na hekima Wazee hawa walisisitiza umoja, upendo na mshikamano wa kitaifa na walikataa misimamo ya wahafidhina kutaka kulipiza kisasi.

Leo, Lissu wao ndiyo kutwa wanaichafua nchi na viongozi halafu eti waombwe radhi na kubembelezwa! Childish! CHADEMA lazima ionyeshe political maturity!
 
mbwa hawa wanabambika watu kesi halafu wanataka hekima. Wewe mbona hukutumia hekima wakati unabambikiza kesi

Punguza ukali wa maneno...

Ile kauli imetoka Ikulu kwa kiongozi wa dola.
Baadala yakuichukua tu kauli yenyewe, zama ndani zaidi uelewe msingi wa kauli ile ya kimamlaka, Dola inamengi kuliko mimi na wewe tunavyofahamu...

Kuna kauli ilitoka kwa mkuu wa mamlaka juu ya mtu fulani kuomba documents kwa mtu fulani huku akijua Dola inakabiliana na watu fulani kwa maslahi ya Taifa.... hatujui maamuzi ya dola juu ya mhusika lakini mhusika aliyeombwa documents ni mbunge sasa wa chama tena baada ya kutoka mahabusu... ( Tafsiri yangu hapa sio kuunga mkono juu ya unyama fulani kwa fulani hapana ni kuonyesha tu namna tunavyopaswa kutofautisha dola, maslahi ya Taifa na siasa zetu hizi)...

Rais anaposema au kuzungumzia suala la heshima maana yake ni utii kwa mamlaka na utii wa sheria....
 
Lissu kakurupuka kumjibu Zitto,kumbe wenzake walienda na file kumuangukia Mangula!
Yaan Katibu hajamtaarifu kaimu mwenyekiti wake kwamba anakwenda kwa makamu mwenyekiti wa ccm kuomba msamaha,ili mbowe aachiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…