Tundu Lissu: Wakati mnajadili kujiuzulu kwa Spika Ndugai, mwenzenu He's laughing all the way to the Bank. Anaondoka akiwa tajiri

Tundu Lissu: Wakati mnajadili kujiuzulu kwa Spika Ndugai, mwenzenu He's laughing all the way to the Bank. Anaondoka akiwa tajiri

Hiyo calculation ya kiinua mgongo (gratuity) ni kwa mujibu wa sheria ipi maana naona kama vile upotoshaji umezidi kushika kasi.
 
Hiyo calculation ya kiinua mgongo (gratuity) ni kwa mujibu wa sheria ipi maana naona kama vile upotoshaji umezidi kushika kasi.
Hivi Stroke hata hoja huioni hapo. Ni lazima uonekane uko against Lissu ?!.

Wa Tanganyika tumerogwa somewhere. Sijui tatizo ni kuchukulia siasa kama yanga & simba !!
 
Hivi Stroke hata hoja huioni hapo. Ni lazima uonekane uko against Lissu ?!.

Wa Tanganyika tumerogwa somewhere. Sijui tatizo ni kuchukulia siasa kama yanga & simba !!
Kwahiyo unataka nikae kimya hata kama anapotosha kuhusiana na kiinua mgongo.

Hakuna mahali hapa Duniani Kiinua mgongo kinalipwa namna hiyo.
 
Kwahiyo unataka nikae kimya hata kama anapotosha kuhusiana na kiinua mgongo.

Hakuna mahali hapa Duniani Kiinua mgongo kinalipwa namna hiyo.
Tupe ufafanuzi wako mkuu. Ni vizuri tukaskia kutoka kwako pia.
 
Ndio baba yako, kaka yako au ww mwenyew in reality umeshindiliwa bullets za kutosha ili ufe. Then kibinadam kbs ni ngumu sana kutoumia kila ukikumbuka. Sometimes huez mlaumu kwa madhira aliyopitia still hata hakuna aliejali kuchukua hatua, Tafakari mkuu!!!
I know this, but kwa nafasi yake kama kiongozi wa chama na kwa future plan za chama sioni sababu kwake kuendelea na kauli za aina hiyo.

Hizi lugha akiendelea nazo wapo watakaomshangaa, na siamini kama jibu sahihi kwa hao watakaomshangaa wakiuliza kwa nini anatumia lugha hizo tuwajibu kwasababu alipigwa risasi.

Kwanza yule mtuhumiwa namba moja hayupo tena, sasa kuendelea kutumia hizo kauli kwa hawa waliopo binafsi sioni maana yake.
 
Upotoshaji....

Upotoshaji katika hicho kiinua mgongo "gratuity"....
 
Kwa mujibu wa Sheria ya Mafao ya Watumishi wa Kisiasa [Political Service Benefit Act] iliyotungwa wakati wa serikali ya awamu ya tatu chini ya Rais Hayati Benjamin W. Mkapa, mstaafu huyu wa "kujiuzuru kwa kulazimishwa" yuko entitled kupata mafao yafuatayo;

1. Kiinua Mgongo [Gratuity] cha 50% ya pesa zote alizowahi kulipwa kama mshahara wakati wote akiwa Spika [2015 - January, 2022]...

2. Malipo ya pensheni 80% ya mshahara wa Spika kwa wakati huo/wa sasa...

3. Winding up Allowance: Ambayo ni malipo ya mkupuo ya mishahara yake ya miaka miwili [miezi 24] - February 2022 hadi February 2024..!

4. Gari mpya [brand new] moja ya chaguo lake [obviously itakuwa Toyota Land Cruiser V8]....

5. Personal Driver: Huyu ni mwajiriwa wa serikali na atakuwa analipwa na serikali maisha yake yote hadi boss atakapokufa...

6. Lita 70 za mafuta ya gari kila wiki sawa na lita 280 kila mwezi: Hii ni kwa ajili ya Gari yake aliyonunuliwa na serikali...

7. Fedha taslimu 40% ya thamani ya bei ya mafuta anayopata kila mwezi i.e Lita 280: Hii inaitwa vehicle maintenance allowance kila mwezi...

8. Diplomatic Passport for him & his Spouse: Kwa maisha yao yote hadi watakapokufa...

9. Atapewa/kujengewa nyumba ya thamani ya chaguo lake....!

NOTE:
1. Sheria hii inawataja hawa "Viongozi walio katika Utumishi wa kisiasa" kuwa ni: Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, mawaziri, makatibu wakuu, manaibu mawaziri, wabunge, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya nk

2. Kinachowatofautisha hawa wote ni AINA na VIWANGO vya mafao [benefits]. Wanaofaidika na kulundikiwa mafao mazuri na ya kufuru zaidi ni Rais, VP, PM, Mawaziri...

3. TUNDU LISSU alimaliza kutoa maelezo ya elimu na ufafanuzi wake akijibu swali hili kwa wasikiliizaji na wachangiaji wa mjadala huo kwa kusema...

"....Wakati nyie mkishangilia na kulumbana mitandao oh amejiuzuru, mwenzenu IS LAUGHING ALL THE WAY TO THE BANK . Hili lijamaa limeondoka lakini likiwa litajiri kwelikweli...!!"

Akauliza, mnadhani ni kwanini CCM wanang'ang'ani madaraka, hawataki kuondoka madarakani kwa njia za Amani hata kutupiga risasi sisi wengine (yeye TL)...?

Alijijibu kwa kusema: Ni kwa sababu hii....ULAJI..!!
Kama hizo ndiyo stahili za viongozi wa kisiasa,kwa nini mnatarajia kuwa CCM wakubali mabadiliko ya aidha Katiba?
Ni dhahiri hawawezi kukuba kwa hiari yao aslani.Maovu,akili,nguvu na raslimali yoyote itakayowabakiza madarakani itatumika mpende msipende hata mkifa njaa ama ukali wa tozo/maisha wao hawajali na haiwahusu.
Bila Katiba mpya,sisi Watanzania na nchi yetu tupo mnadani na tushauzwa tayari-tunakaangwa kwa mafuta yetu wenyewe na tunaangamia kwa kunyimwa maarifa.
 
Ifike mahala hata ninyi wanachama muyaelewe hayo maneno kwamba yanafaa kutumika ili kutia msisitizo wa hoja maana hata hao ambao wako against na nyie kuna wakati wanatumia maneno kama hayo hayo.

Sikiliza ule wimbo wa CCM mbele kwa mbele kuna maneno kama “waache waandamane wajinga wale” nikusema jambo ambalo kikatiba linajulikana watu timamu wakilifanya ni wajinga?

Mimi naona yupo sawa asimtukane tu mtu matusi ya nguoni.
Sasa mjinga hapa kwa mtazamo wangu ni yule anayeona wanaoandamana ndio wajinga, kwasababu ni haki yao kisheria, hawa ni kama kichaa anayekimbia na nguo yako bora usimkimbize ili kutunza heshima yako.
 
Kumbe ndo maana wanaenda kwa waganga maporini huko[emoji848][emoji848]
 
I know this, but kwa nafasi yake kama kiongozi wa chama na kwa future plan za chama sioni sababu kwake kuendelea na kauli za aina hiyo.

Hizi lugha akiendelea nazo wapo watakaomshangaa, na siamini kama jibu sahihi kwa hao watakaomshangaa wakiuliza kwa nini anatumia lugha hizo tuwajibu kwasababu alipigwa risasi. Kwanza yule mtuhumiwa namba moja hayupo tena, sasa kuendelea kutumia hizo kauli kwa hawa waliopo binafsi sioni maana yake.
Mkuu mbona kama unateseka bure!

Lissu ndivyo alivyo amekuwa na maneno makali hata kabla ya kupigwa risasi, fuatilia matamshi yake utaona maneno kama Dikteta uchwara n.k...

Nafikiri ukiwa unataka abadilike unataka asiwe Lissu labda awe Ndugai!

Maneno makali viongozi wengi wazuri wanayo, kumbuka Mwl Nyerere alivyokuwa anatumia maneno makali kwa watu wasioelewa, wajinga, wapumbavu, malayamalaya, walevi nakumbuka aliwahi kumwita Regan rais wa Marekani mjinga n.k
 
Duh!, Hapa nikuomba Ndugai atengue arudi tu kwenye uspika, inamaana huyo mwingine atalipwa kama Ndugai, mzigo kwa taifa huu
 
Labda hasira ya kunyimwa pesa ya matibabu
Amekuwa mvumilivu mno.CCM mkiambiwa mabaya yenu mnapenda sana kuhurumiwa,eti maneno makali:Ni makali kuliko risasi?Hivi Lissu hana moyo/mwili wa nyama!Ndugai aliposema ukweli wa kuuzwa kwetu mlivyomshukia kama mwewe je,ni sahihi?
Uwasilishaji wa hoja wa Mh.Lissu ni sahihi.
Alinyimwa matibabu ya majeraha ya risasi alizomiminiwa akiwa kazini na siyo ugonjwa wa kusendeka ili lengo la muuaji wake litimie,mlitaka awasujudie?
Mkuki kwa nguruwe?
 
Back
Top Bottom