Tundu Lissu: Walionipiga risasi ni Kikosi Kazi cha Ofisi ya Rais chini ya Mkuu wa TISS, Balozi Kipilimba

Tundu Lissu: Walionipiga risasi ni Kikosi Kazi cha Ofisi ya Rais chini ya Mkuu wa TISS, Balozi Kipilimba

Hili na mimi ndio nilikua nataka kulisema haya yote anazuga tu pesa ya ukimbizi ya bure keshaiona tamu kuliko kurudi bongo. Asiwasingizie watu ubaya kikosi cha kujumuisha TISS, JWTZ na polisi kingemtaka kisingetumia risasi 36 na atoke mzima. Hao jamaa wa kazi risasi mbili tu angekua sasa hivi jina lake linatanguliwa na marehemu. waliompiga risasi hawajui anabahatisha ila watakua ni wahuni tu waliotaka kuivuruga nchi. Lisu anatafuta scapegoat ya kutorudi bongo mjanja sana huyu wakili msomi😀😀😀😀[emoji23][emoji23][emoji23]
Ungekuwa wewe ndiyo lissu,ungerudi[emoji15][emoji15] hebu karibu kuvaa viatu vyake kwanza
 
Huyu bwana ni mlalamikaji wa kiwango cha PHD. Kama Rais kafunga safari mpaka Belgium na akataka waonane, ni lazima nia yake iwe ni njema.

Akumbuke kuwa rais ni taasisi yenye watu wengi nyuma wenye majukumu mbalimbali. Hivyo aondoe wasiwasi aliokuwa nao.

Kufariki kwa JPM kumaifanya taasisi ya urais iwe na mabadiliko makubwa. Aondoe shaka.
Lakini kwa maelezo yake lile jarada lililofunguliwa na Kipilimba bado halijafungwa .... Hivyo linaweza kufunguliwa siku yeyote na wakamalizia pale walipoishia!!
 
Mh. Tundu Lissu awataja waliohusika kumshambulia.

Tundu Lissu amesema Walionipiga risasi ni Kikosi kazi kilichopo chini ya Rais kikisimasimaiwa na Mkuu wa TISS Kipilimba. Kikosi kazi kimeua watanzania wengi sana.

Kimeua watu wengi sana, Kilijumuisha watu wa Usalam wa taifa, Watu wa Jeshi la Wananchi, Jeshi la Polisi. Kinaitwa kikosi kazi cha kupambana na Ugaidi na madawa ya kulevya.

Watu wote waliouawa Maeneo ya Mkuranga, Kibiti Kilwa Rufiji zaidi ya watu 400. Wale waliokuwa wanatupwa mtoni maiti zinaokotwa kwenye beach, wote ni Wahanga wa Kikosi hicho.

Ndio waliomteka Ben Saanane, Azory Gwanda Mdude, Mo Dewji. Yote yalitekelezwa na hicho kikosi kazi hichi chiini ya Kipilimba ammbaye sasa ni Balozi.

Sawa maana Balozi kipilimba yupo na atasema naye
 
Hajaweka wazi nini haswa hoja yake. Ni kama mtu mwenye wasiwasi usiokwisha kwa vigezo vya mwanzoni mwa maongezi haya.

Inaweza kuwa ni muendelezo wa siasa za mitandaoni, hataki kutoka midomoni mwa watu kirahisi hivyo inambidi aongee hata kama anachokiongea ukikipima hakina undani sana.
Tundu lisu Muongo TU ,wala hakupigwa risasi,Yale makovu ni ya ugonjwa wa tetekuwanga
 
Yaani huyu poyoyo anabwabwaja kama vile anapigwa risasi Kila siku.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Wewe ungepigwa risasi moja TU ya mguu,sidhani kama ungekua na akili timamu Hadi Leo.
Usiombe kusikia milio ya risasi na risasi zikiingia mwilini mwako.
Sikia kwa watu TU.
Eti Unamwita poyoyo.
Vijitu vingine bana.
 
Mlio karibu na Lissu mkanyeni Amshukuru Mungu wake, na uongizi wa Sasa SSH kumpa Mkono wa heri inatosha.
Kutaja hovyo majina ya taasisi nyeti na majina viongozi kumtafuta mchawi haina maana.
Taasisi Ni kubwa kuliko uhai wa yeyote. Zinafanya mengi makubwa yasiyopimika kwa amani na salama ya taifa letu.
Japo binafsi nasikitika kwa yote ila katika maisha Kuna "DO "and " DON'T"
 
Tundu lisu Muongo TU ,wala hakupigwa risasi,Yale makovu ni ya ugonjwa wa tetekuwanga

Tetekuwanga na Risasi zote ni dhahama kikubwa unarecover vipi kutoka na madhara yake/yatokanayo. TL kwa jinsi alivyo kuwa akiongea alikuwa mtu mwenye furaha na bashasha tele baada ya JPM kufa. Kulikoni mbona bado anahangaika na kulalala lalama? Ama hakujua anaye kufa ni mtu si mfumo?
 
Back
Top Bottom