Tundu Lissu: Walionipiga risasi ni Kikosi Kazi cha Ofisi ya Rais chini ya Mkuu wa TISS, Balozi Kipilimba

Tundu Lissu: Walionipiga risasi ni Kikosi Kazi cha Ofisi ya Rais chini ya Mkuu wa TISS, Balozi Kipilimba

Nimefuatilia mjadala huu wa kisiasa nimegundua Watanzania tuna roho mbaya sana hasa mhanga anapokuwa si wa itikadi sawa na yetu,kisiasa au kiimani huwa tunaona kama si binadamu mwenzetu anayesitahili kuishi au haki nyingine yoyote na tunakoelekea kama taifa ni kubaya mno.
 
Ameomba commitment hakikisho la usalama na sio minimum risk

Yote hii ni kuendelea kuwatafutia uhalali wale wauwaji kwenye yao?

1. Alitoa taarifa ya kuwa hatarini mkapuuza.
2. Akashambuliwa, upelelezi haujafanyika kuwapata wauwaji.
3. Yuko tayari kurudi, kumhakikishia usalama hamtaki.

Kumhakikishia usalama si ni kumpa ulinzi na kuwakabili wote waliotaka kumdhuru?

Au hasa hasa nyie mnataka nini?

Au mbwa mtakuwa mmekula mbwa?
 
Nimefuatilia mjadala huu wa kisiasa nimegundua Watanzania tuna roho mbaya sana hasa mhanga anapokuwa si wa itikadi sawa na yetu,kisiasa au kiimani huwa tunaona kama si binadamu mwenzetu anayesitahili kuishi au haki nyingine yoyote na tunakoelekea kama taifa ni kubaya mno.

Ila rekebisha kidogo yule mwingine alikuwa mwuaji unprovoked.

Huyu mwingine ni mhanga wa wauwaji mithili ya majambazi tu.

Hii ni purely CCM dhidi ya wengine.
 
kama ni kweli, case closed,,amiri jeshi was nchi yeyote Dunia,ananguvu sana,
cheki Trump alitoa amri TU,watu wakapotea,,
huu ukweli watu wanajifanya hawautambui,,bush aliamuru jeshi liingie iraq ,matokeo take watu milioni kadhaa walikufa,,,
mfalme Daud,aliaamuru kamanda wake mkuu auWe ili tu yeye arithi Mke,,
kama anavyodai ni kweli Lisu awe mpole tu,hakuna kitu sisi tutaweza msaidia
Trump au Bush walitoa amri ya kuuwawa Mmarekani gani?
 
Hili na mimi ndio nilikua nataka kulisema haya yote anazuga tu pesa ya ukimbizi ya bure keshaiona tamu kuliko kurudi bongo. Asiwasingizie watu ubaya kikosi cha kujumuisha TISS, JWTZ na polisi kingemtaka kisingetumia risasi 36 na atoke mzima. Hao jamaa wa kazi risasi mbili tu angekua sasa hivi jina lake linatanguliwa na marehemu. waliompiga risasi hawajui anabahatisha ila watakua ni wahuni tu waliotaka kuivuruga nchi. Lisu anatafuta scapegoat ya kutorudi bongo mjanja sana huyu wakili msomi😀😀😀😀[emoji23][emoji23][emoji23]
Bila shaka utakuwa mmoja wa wahuni hao
 
Wanaumkebehi Lissu ni wendawazimu...huyu mtu alitaka kuuliwa na mwili wake umeumizwa. Amekuja kushiriki uchaguzi kila chombo cha habari kilipigwa marufuku kutangaza habari zake. Alitaka kuuliwa akakimbilia ubalozi wa Ujerumani ameondoka chini ya usimamizi wa mataifa ya nje, sasa hapa analalamika kuhusu hao watu waliotaka kumdhuru kuna mbuzi mawe humu zinakebehi. Huyo Mama Samia mwenyewe pamoja na kwenda kumtembelea Nairobi mbona alishindwa kusimamia alivyotaka kuuliwa tena. Magufuli alikuwa na kikosi katili sana.
Wanao mkebehi ndio hao hao wahusika mkuu. Usishangae
 
Back
Top Bottom