Mimi siyo mwanasheria wala mwanasiasa, lakini nina foundation nzuri sana kuhusu sheria kwa vile ninaishi mazingira ambayo ujuzi wa sheria ni wa muhimu sana. Kwa mfano polisi akikuwashia taa za rangi barabarani huwezi kukimbia ukidai kuwa hujaambiwa kosa lako; ukikimbia unakuwa umetenda kosa, na anaweza kukurushia risasa au kutafuta polisi wengine wakuzingire na hata kuangusha gari lako mtaloni kwani wakti huo tayari unakuwa ni mhalifu hata kama sababu waliyokuwa wanataka kukuuliza haikuwa inahusianiana na makosa yako binafsi. Simama umsikilize kwa nini kakuwashia taa za rangi, baada ya hapo ndipo uulizea uhalali wake kukusimamisha.
Polisi siyo mahakama, hawahukumu bali kazi yao ni kutafuta ushahidi, na raia anakuwa anavunja sheria kuwazuia polisi kutafuta ushahidi huo. Ukishashaingiza mambo ya sheria kwenye siasa basi unakuwa unapoteza watu wako, na pia kuvuruga jamii. hakuna uhusiano wowote kati ya sheria na siasa kwenye jamii timamu.