Tunduma ni mji wa kipekee. Mapigo yake ni kama Kariakoo

Hakuna ma mwamba ambao huwa nawakubali kama huyu mwamba. Yaani wakiishi mahali wanafuatilia kujua mishe na info zote za mji. Mimi nimewahi ishi mji mmoja zaidi ya miaka 5 ila ukiniuliza taja matajiri watatu katika mji huo siwezi
 
Mkuu bila picha huu uzi huutendei haki walah!!!


🤓🤓🤓🤓
 
Hapana, unaingia tu hata na gari yako yenye plate number za Tz, sema kuna distance ya kutoka mpakani mpaka km kadhaa mbele ndio utatakiwa docs.
Mfano natoka hapo tunduma natumia usafiri gani kwenda nakonde
 

Mkuu nikifika hapo na 1.5m naweza kujitafuta nikajipata?
 
Wewe naona unapitaga ndani ya gari tu watu wenye mpo ndani ya gari lazima mpigwe bei iyo ipo sehemu yote.

Tunduma Kuna machaka ugari maharage na mboga za majani jero tu [emoji16] unapewa na advantage ya kachumbari ya free.
Kunaitwa magurueni........
 
Mkuu nikifika hapo na 1.5m naweza kujitafuta nikajipata?
Mkuu, hiyo pesa inatosha sana kuanza pale Tunduma, kile ni chuo cha maisha mwana. Hiyo laki tano ipangie kujikimu na hiyo millioni hakikisha inakuwa mtaji wako. Fungua milango yote ya fahamu ujifunze, jenga mahusiano na hustlers waliopo pale ikiwezekana omba kibarua kwa wafanyabiashara wakubwa pale. 1.5m unatoka tu!
 
Nimewahi kufika mara 5 ila sijawahi upenda huo mji umekaa hovyo afu kukame sana.
Mkuu, mara ya kwanza nilipita Tunduma mwaka 1995 na treni ya TAZARA kuelekea Kapirimposhi. Kimji kile kilionekana kama vibanda kwenye kambi ya wakimbizi, Ukweli ni kuwa pale sio mahali pa kutumia, pale kila unayemuona amekuja kutafuta, na mawazo ya utafutaji ndio pale utasikia hadi mtoto mdogo..... Pesa inasakwa shambani kwenye kilimo na mtaani kwenye biashara. Pale ng'ambo upande wa Zambia ni hivyo hivyo.
 

Naweza kuja pm unishauri kitu mkuu?
 
Bila shaka!.. Lakini ingependeza sana kama na wengine humu wangepata uzoefu wa Tunduma.

Ok plan yangu nataka niende week inayoanza, but nilitaka nianze na biashara ya mtaji mdogo kama laki tatu hivi ili nikiyumba niwe na backup naogopa kuinvest yote kwa pamoja, nataka nipange chumba cha bei rahisi tuu kwasababu ndio naanza mishe huko. Kwa uzoefu wako biashara gani naweza kuanza kwa pesa hiyo na sehemu gani naweza kupata chumba cha bei rahisi penye usalama pia. Yeyote mwenye uzoefu na huko anaweza kunishauri chochote kile. Thanks in advance great thinkers.
 
Naweza kuja pm unishauri kitu mkuu?
Bila shaka!.. Lakini ingependeza sana kama na wengine humu wangepata uzoefu wa Tunduma.
Ni biashara gani uanze nayo?... Hiyo ni ngumu kukushauri, inategemea wewe unatamani kufanya biashara ya aina gani. Anza kwanza kutafuta chumba cha bei rahisi tu, viko vingi sana. Ukiishapata chumba na pesa ya kianzio ipo anza kutoa huduma kwa kubadilisha pesa au vuka mpaka ukajumue vipodozi Nakonde uje uuze kwenye mabasi. Wakati huo yasome mazingira kwa haraka sana, ndani ya mwezi utakuwa umeona njia ya kutokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…