Tunduma ni mji wa kipekee. Mapigo yake ni kama Kariakoo

Tunduma ni mji wa kipekee. Mapigo yake ni kama Kariakoo

Zile deal za Black market upande wapili nyuma ya frame za Viatu ule upande unazalisha sana Madoni Kila mwezi kwenye deal za:-
Vipodozi.
Vitenge.
Mafuta ya Kula.
Sukari.
Sigara .
Mbegu za Mahindi / Zamsed.
Mafazeti used kutoka Zimbabwe, South Africa.
USD ;- zinatoka Congo na unazipata upande wapili, Pombe za Viroba, na Pombe za vichupa vidogo wanauza Bei ya Tshs 1000/= na Viroba vinaanzia 250-500 maeneo ya Black na Iboya.
Kuna matajiri wanspiga Hela kwenye Biashara ya kubadilisha Fedha, yeye ana Supply fedha Kwa Vijana jioni anarudishiwa na Faida , Hao wanaitwa wenye Visima , mtu ana Supply hata billioni Moja Kwa Vijana wake 30 wanaokwenda kutafuta Dolla Hadi Congo.
Kuna Wababe kwenye Biashara ya Mafuta ya Petroleum kupeleka upande wa Zambia Kuna Yule Msomali wa Petroafrica mwenye upara aliwakamata sana wa Zambia.
Kuna Yule Tajiri wa Valentine Bar ya Pale Boarder na Valentine night club Jamaa anajimbiza sana kaanzia kwenye Bar Hadi kushika soko la Viatu Hadi Kumiliki Kusoma pale Kisimani.
Yupo Dubai Tyre Jamaa anakimbiza sana kwenye biashara ya Tyre Sasa amehamia kwenye Mafuta Bei zake za Tyre ni kama Dar es salaam. Yupo yule Manyanya ameshika biashara za maduka balaa pale Boarder piya yeye ndie amehamia kwenye vituo vya Mafuta, Wapo Hawa Jamaa wa Olympic petroleum anauza Mafuta Kwa wholesale Kwa Bei ya Depot'.
Mjii wa Tunduma una Bank zaidi ya Sita, Petrol Station zaidi ya Hamsini, lodge na Bar zimetapaka Kila baada ya nyumba mbili or tatu,
Hakuna ma mwamba ambao huwa nawakubali kama huyu mwamba. Yaani wakiishi mahali wanafuatilia kujua mishe na info zote za mji. Mimi nimewahi ishi mji mmoja zaidi ya miaka 5 ila ukiniuliza taja matajiri watatu katika mji huo siwezi
 
Huu uzi ilikuwa niuandike muda mrefu kwa mambo niliyojionea kwenye mji wa Tunduma. Kwa ambao hajawahi fika Tunduma wanaweza kudhani ni ka-mji kadogo ambacho kipokipo tu. Kwa sisi wa Arusha tulikuwa tunaamini Namanga ndo mji mkubwa zaidi wa mpakani kwa Tanzania kumbe kuna Tunduma.

Kinachonifanya niandike ni biashara kubwa iliyoko Tunduma. Ule mji wa mpakani kwa mjasiriamali mdogo ni sehemu sahihi ya kwenda kusoma ramani. Uchangamfu wake unaendana sana na Kkoo tofauti ikiwa ni ukubwa tu. Ila wafanyabiashara wa nguo Tunduma wanawezaje kuuza nguo za jumla kwa bei sawa na ya Kariakoo? Baadhi ya wafanyabiashara huuza bei chini hata kuliko Kariakoo. Kimahesabu imekaaje hii? Hata vitu vingine jamaa wako fair.

Kimsingi Tunduma ni boda kubwa zaido bongo yenye fursa nyingi sana.
Mkuu bila picha huu uzi huutendei haki walah!!!


🤓🤓🤓🤓
 
Naifahamu sana border ya Tunduma. Nimewahi kupiga kambi pale kwa miezi mitatu na ndio mahali nilipopata ujanja wa kujitafutia na kusimamia hatma ya maisha yangu.
Tunduma nenda na akili tu ya kujituma na uaminifu, Kisha uwe na nidhamu kwenye matumizi ya pesa unayopata, baada ya mwaka utagundua siri ya mafanikio.

Mzunguko wa pesa Tunduma ni hatari, pale ndio njiapanda ya minyororo ya pesa... Hata jirani zetu wa Zambia pale Nakonde wanaufahamu mziki wa Tunduma......
Sidhani kama Tanzania hii iko border iliyochangamka kama Tunduma. [emoji848]

Mkuu nikifika hapo na 1.5m naweza kujitafuta nikajipata?
 
Wewe naona unapitaga ndani ya gari tu watu wenye mpo ndani ya gari lazima mpigwe bei iyo ipo sehemu yote.

Tunduma Kuna machaka ugari maharage na mboga za majani jero tu [emoji16] unapewa na advantage ya kachumbari ya free.
Kunaitwa magurueni........
 
Mkuu nikifika hapo na 1.5m naweza kujitafuta nikajipata?
Mkuu, hiyo pesa inatosha sana kuanza pale Tunduma, kile ni chuo cha maisha mwana. Hiyo laki tano ipangie kujikimu na hiyo millioni hakikisha inakuwa mtaji wako. Fungua milango yote ya fahamu ujifunze, jenga mahusiano na hustlers waliopo pale ikiwezekana omba kibarua kwa wafanyabiashara wakubwa pale. 1.5m unatoka tu!
 
Nimewahi kufika mara 5 ila sijawahi upenda huo mji umekaa hovyo afu kukame sana.
Mkuu, mara ya kwanza nilipita Tunduma mwaka 1995 na treni ya TAZARA kuelekea Kapirimposhi. Kimji kile kilionekana kama vibanda kwenye kambi ya wakimbizi, Ukweli ni kuwa pale sio mahali pa kutumia, pale kila unayemuona amekuja kutafuta, na mawazo ya utafutaji ndio pale utasikia hadi mtoto mdogo..... Pesa inasakwa shambani kwenye kilimo na mtaani kwenye biashara. Pale ng'ambo upande wa Zambia ni hivyo hivyo.
 
Mkuu, hiyo pesa inatosha sana kuanza pale Tunduma, kile ni chuo cha maisha mwana. Hiyo laki ipangie kujikimu na hiyo millioni hakikisha inakuwa mtaji wako. Fungua milango yote ya fahamu ujifunze, jenga mahusiano na hustlers waliopo pale ikiwezekana omba kibarua kwa wafanyabiashara wakubwa pale. 1.5m unatoka tu!

Naweza kuja pm unishauri kitu mkuu?
 
Bila shaka!.. Lakini ingependeza sana kama na wengine humu wangepata uzoefu wa Tunduma.

Ok plan yangu nataka niende week inayoanza, but nilitaka nianze na biashara ya mtaji mdogo kama laki tatu hivi ili nikiyumba niwe na backup naogopa kuinvest yote kwa pamoja, nataka nipange chumba cha bei rahisi tuu kwasababu ndio naanza mishe huko. Kwa uzoefu wako biashara gani naweza kuanza kwa pesa hiyo na sehemu gani naweza kupata chumba cha bei rahisi penye usalama pia. Yeyote mwenye uzoefu na huko anaweza kunishauri chochote kile. Thanks in advance great thinkers.
 
Naweza kuja pm unishauri kitu mkuu?
Bila shaka!.. Lakini ingependeza sana kama na wengine humu wangepata uzoefu wa Tunduma.
Ok plan yangu nataka niende week inayoanza, but nilitaka nianze na biashara ya mtaji mdogo kama laki tatu hivi ili nikiyumba niwe na backup naogopa kuinvest yote kwa pamoja, nataka nipange chumba cha bei rahisi tuu kwasababu ndio naanza mishe huko. Kwa uzoefu wako biashara gani naweza kuanza kwa pesa hiyo na sehemu gani naweza kupata chumba cha bei rahisi penye usalama pia. Yeyote mwenye uzoefu na huko anaweza kunishauri chochote kile. Thanks in advance great thinkers.
Ni biashara gani uanze nayo?... Hiyo ni ngumu kukushauri, inategemea wewe unatamani kufanya biashara ya aina gani. Anza kwanza kutafuta chumba cha bei rahisi tu, viko vingi sana. Ukiishapata chumba na pesa ya kianzio ipo anza kutoa huduma kwa kubadilisha pesa au vuka mpaka ukajumue vipodozi Nakonde uje uuze kwenye mabasi. Wakati huo yasome mazingira kwa haraka sana, ndani ya mwezi utakuwa umeona njia ya kutokea.
 
Back
Top Bottom