Tupate mkataba wa uendeshi wa hospital za Bugando (TEC) na KCMC (KKKT) ili tujadili bandari vizuri

Tupate mkataba wa uendeshi wa hospital za Bugando (TEC) na KCMC (KKKT) ili tujadili bandari vizuri

Hakuna tofauti ya Bei kati ya hizo hospital ulizotaja,Tena za kanisa Bei juu, serikalini Bei chini,kwa nini hospital za kanisa zinazopata ruzuki Bei iwe juu!?..na Kwa nini serikali isaidie biashara za kanisa!?..yaani serikali itie ruzuku halafu useme imeshindea zuendesha!?..tumia akili,haijalishi agha Khan kuwa Ismailia au laa,kwa nini hawakupewa mkataba waliopewa kanisa!?
Una ujinga mwingi sana
 
Unaongeaongea togwa gani we mbuzi!!?..yaani kigezo Cha ruzuku iwe kuwahi kutaifishwa!?..huo ni msaada wa serikali kwa kanisa,imekua hivyo tangu mkoloni,padre dokta sivalon aliandika bila msaada wa serikali taasisi za kanisa zingekufa kifo Cha mende siku nyingi
Kama mkristu matusi kwangu mwiko. Kwa sababu umeelekea huko sitakujibu ili niendelee kuwa na amani.

Amandla...
 
Hospital za Bugando na KCMC zinamilikiwa na makanisa na zinaendeshwa kwa ubia na serikali ya JMT. Ninafikiri mikataba yake ingetusaidia sana kwenye mjadala unaoendelea wa bandari
Hapa tayari umemaliza kwa kuleta justification ya DP world sio!! CCM ni CCM walah hata awe mtakatifu.
 
Hizo ruzuku ziende kwenye hizo hospital za serikali vijijini ambazo hazina vifaa tiba na madaktari badala ya kusaidia biashara za kanisa
Hilo neno ruzuku halijakaa vizuri hizo pesa hiwa ni kwa ajili ya wafanyakazi wa serikali waioko.kwenye hizo hospitali na ukumbuke.miundo.mbinu nyote na vifaa tiba huwa mali ya kanisa sio.serikali sababu uwezo wa serikali kujenga miundombinu mikubwa kama hiyo huwa hawana kwa maeneo yote ya nchi

Hivyo sehemu.ambazo uwezo haupo hutumia hizo za kanisa kuhudumia wananchi wake

Inakuwa gharama ndogo kwa serikali pia kuliko kujenga ya kwake eneo husika..Sababu kuna cost sharing.Kanisa linabeba na serikali inabeba kipande chake kuliko.zigo.lote la hospitali hiyo lingekuwa.zigo la serikali pekee
 
Hospital za Bugando na KCMC zinamilikiwa na makanisa na zinaendeshwa kwa ubia na serikali ya JMT. Ninafikiri mikataba yake ingetusaidia sana kwenye mjadala unaoendelea wa bandari
Hizo Hospitali ni mali ya Kanisa ila Mchonga alizipora kwa kile kilochoitwa kutaifisha enzi za giza za Azimio la Arusha. Msitake kuhalalisha uhuni wa mkataba wa kimangungo wa DP World.
 
Hospital za Bugando na KCMC zinamilikiwa na makanisa na zinaendeshwa kwa ubia na serikali ya JMT. Ninafikiri mikataba yake ingetusaidia sana kwenye mjadala unaoendelea wa bandari
WACHATUSEME NA.2

TANZANIA NI YETU SOTE SIO MALI YA WAKRISTO

Hivi karibuni kumezuka mjadala mkali kuhusu Serikali kuingia kwenye makubaliano ya kuendesha Bandari za Tanzania na kampuni ya DP World. Mjadala huu ulianza na sura ya kisiasa wakati Mwenyekiti wa Chadema Bwana Freeman Mbowe alipotoa shutuma kali kuwa Bandari za Tanganyika zinauzwa na Wazanzibari yaani Waziri wa Ujenzi, Mhe Makame Mbarawa na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan.

Lakini ghafla mjadala ukahama kwenye Siasa na ukatawaliwa na hisia kali za kidini. Sote tumeshuhudia namna viongozi wa dini ya Kikristo hasa wakatoliki wakiongozwa na Kadinali Pengo walivyokuwa wakilipigia kelele suala la Bandari.

Hoja zinazotawala mjadala huu ni mbili. Hoja ya kwanza ni kwamba mkataba ule umesainiwa na Waziri Mzanzibari na Rais Mzanzibari na kwamba Wanzanzibari hawa wawili wanauza mali za Tanganyika. Hoja yao ya pili inadai kuwa mkataba hauna ukomo wa muda, yaani ni mkataba wa milele. Hii hoja hii ya pili inashabikiwa sana na viongozi wa Kanisa.

Jambo la kushangaza ni kuwa mpaka sasa hakuna hata msemaji mmoja, awe mwanasiasa au kiongozi wa Kanisa aliyetoa hoja za kiuchumi na utendaji za kupinga makubaliano hayo.

Badala yake, viongozi wengine kama vile mama Anna Tibaijuka anadiriki kusema uwongo kuhusu sababu za DP World kukataliwa kuendesha Bandari za Marekani. Mama Tibaijuka anajua vyema lakini hakutaka kusema kuwa sababu ya kukataliwa kuongoza Bandari za New York na New Jersey ni Uwarabu wao na wala si utendaji wao.

Ni kweli Bunge la Marekani lilikataa DP World wasipewe Bandari hizo lakini walisema wazi kuwa Marekani haiwezi kuwapa Waarabu kuendesha Bandari zao kwa sababu za kiusalama. Hakuna asiejua msimamo wa Marekani kuhusu Waarabu na Waislamu.

Kwa makusudi kabisa, mama huyu anapotosha watu kwa kufananisha suala la Bandari za Marekani na Bandari za Dar es Salaam. Kwenye suala la Dar es Salaam, DP World haikutaka kununua TPA. Inachopendeza ni kuendesha na si kununua Bandari ya Dar es Salaam.

Suala hili la kuendesha si geni Tanzania. Kampuni ya TICTS imeendesha Bandari ya Dar es Salaam kwa zaidi ya miaka 20. Kampuni ya “Swissport” inaendesha Kiwanja cha Ndege cha Dar es Salaam kwa muda mrefu. Mbona hizi kelele hatukuzisikia?

Wakati wa utawala wa Donald Trump Marekani ilifika hatua ya kupiga marufuku baadhi ya Mataifa ya Arabuni kwa maana Waislamu kuingia Marekani. Kwa hiyo mama Tibaijuka hakutaka kuwa mkweli kuhusu suala hili.

Ametumia kivuli chake cha kuwa mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa kwa wakati ule kuwaaminisha Watanzania kuwa yeye anafahamu zaidi kuhusu ubaya wa DP World.

Mama Tibaijuka amekosa uadilifu (moral authority) wa kuweza kukemea kile alichokiita mkataba mbovu kwa sababu wakati kampuni ya TICTS iliyokuwa inaendesha Bandari ya DSM kwa utendaji wa hovyo huyu mama alikaa kimya hata pale ambapo TICTS walipopewa nyongeza ya mkataba wa miaka 15 bila kufuata sheria za manunuzi.

Lakini jambo la pili, nani asiyejua kuwa mama Anna Tibaijuka alikiri hadharani kuwa alipokea shs 1.6 bilioni ya fedha za rushwa za ESCROW? Huyu mama ambaye alisema kwa majigambo kuwa shs 1.6 bilioni ni pesa ya mboga ana uchungu gani wa kuwatetea Watanzania masikini?

Bado tunarejea kusema tena kwa kinywa kipana, mpaka sasa hakuna mtu hata mmoja aliyesema kwa kuonesha ushahidi kuwa DP World hawana uwezo kifedha au utendaji wao ni mbovu. Hakuna aliyesema kuwa hizo fedha ambazo tunaahidiwa ni ahadi hewa kwa sababu DP World hawana uwezo wa kuvutia mizigo kupitia Bandari ya Dar es Salaam.

Kwa kuwa mjadala umetawaliwa na CHUKI za kidini na wasemaji wakubwa wamekuwa viongozi wa Kanisa. Tukumbuke kuwa ni Wakristo hao hao ambao mmoja kati ya viongozi wao waliosema kuwa Rais Samia anafanana na muuza vitumbua! Makanisa hawakukemea kauli hii ya kumkosea adabu Rais.

Kwa kuwa mjadala wa Bandari una chuki za udini, naomba tujikumbushe nafasi ya Makanisa katika nchi hii.

TUKUMBUKE MWAKA 1992

Mwaka 1992, Serikali iliingia Mkataba na Makanisa kupitia Taasisi zao za TEC na CCT. Chini ya Makubaliano yale, hospitali za Makanisa zitatumika kwa wananchi wote pale ambapo Serikali haina hospitali.

Kwa kufanya hivyo, Serikali itakuwa na wajibu wa kuyapa Makanisa fedha za kuendesha hospitali hizo ingawa umiliki wa hospitali utabaki kuwa wa Makanisa.

Ifahamike kuwa fedha hizo zinatokana na kodI za Watanzania wote; Waislamu, Wakristo, Mabaniani, Magoha, Makadiani, na hata wale wasio na dini.

Nini athari za Mkataba huu ? Mkataba huu wa kibaguzi una athari nyingi. Kwanza:

Serikali inatumia kodi za wananchi kuyapa Makanisa kuendesha shughuli zake za kuimarisha Ukristo.

Tunasema hivyo kwa sababu utaratibu unaotumika ni kuwa Serikali inatoa fedha kwa Makanisa ambayo wao ndio wanapanga matumizi ya fedha zile na sio Serikali.

Pili, kwenye Jamii, Makanisa yanaonekana ndio yanatoa huduma za Jamii na hivyo kujenga saikolojia kwa wananchi kuwa Ukristo ndio unajali wananchi.

Athari ya tatu ni kuwa Makanisa yananyonya wananchi kwa sababu pamoja ya kuwa hospitali zile zinapata fedha kutoka Serikalini, bado wananchi wanalipia huduma.

Nne, Mkataba hauna ukomo, yaani ni wa milele. (Wakristo wataendelea kupewa hayo mabilioni na Waislamu watanyimwa milele).

Kwa tafsiri nyingine ni kuwa Serikali imejivua kwenye wajibu wa kutoa huduma za Jamii na kuchagua Makanisa kuwa ndio wakala wake.

Tunapenda kuwakumbusha Watanzania kuwa wakati Mkataba huo unasainiwa aliyesaini Mkataba ni Bwana Edward Lowassa aliyekuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu. Huyu ni Mkristo

Kwa utaratibu wa Serikali, Lowassa alikuwa Waziri wa Nchi, hivyo basi Waziri mwenye dhamana ni yule mwenye ofisi yake kwa maana ni Waziri Mkuu.

Wakati unatiwa saini Mkataba, huo Waziri Mkuu alikuwa John Samwel Malecela ambaye ni Mkristo.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ndie aliyeishauri Serikali isaini Mkataba ule ambao kwanza hauna ukomo (mkataba wa maisha) na pili unatumia kodi za wananchi kuimarisha Ukristo alikuwa Damian Lubuva ambaye ni Mkristo.

Kwa upande wa Kanisa mwanasheria wao alikuwa Prof Balozi Costa Mahalu, Mkristo.
Kwa maana hiyo, upande wa Serikali, Mkataba ule umeasisiwa na kusimamimwa na Wakristo watupu. Waziri wa Nchi Mkristo, Waziri Mkuu Mkristo, Mwanasheria Mkuu Mkristo.

Ni Wakristo! Wakristo! Wakristo!

Kama kwenye hoja ya makubaliano ya Bandari ni Wazanzibari wawili (ambao ni Waislamu) wamesaini makubaliano ya kuiuza Tanganyika, Mbona Waislamu hawakulalamika pale Wakristo 3 wazito Serikalini walipobuni mbinu za kutumia kodi za wananchi kuimarisha dini yao Ukristo Tanzania?

Kama hoja ni ukomo wa mkataba, mbona Mkataba huu wa Serikali na Makanisa hauna ukomo? Ni mkataba wa milele na ndio maana mpaka leo (miaka 30 sasa) bado unaendelea kutumika.

Bado Serikali inaendelea kutekeleza Mkataba wa kibaguzi ambapo inatumia kodi za wananchi wote kuimarisha shughuli za Kanisa.

USHAHIDI

Tarehe 23 Januari 2019, Rais Magufuli alikutana na viongozi wa dini zote IKULU. Kwenye Mkutano ule Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Tanga Bwana Maimo Mndolwa alilalamika kwa Rais Magufuli kuwa Serikali inavunja Mkataba kwa kujenga hospitali kwenye maeneo ambayo Kanisa imeachiwa kuwa na hosptali ambazo zinapewa fedha na Serikali.
Amelalamika hivyo kwa sababu Mkataba wa Makanisa na Serikali hauna ukomo. Kila penye hospitali ya Kanisa, Serikali haikutakiwa kujenga hospitali yake. Badala yake, Serikali inatakiwa kuendelea kutoa fedha za kodi kuwapa Makanisa ili ziendeshe hospitali zao na kuimarisha Ukristo kwa kutumia jasho la Watanzania.

Katika kusisitiza madai yake, Askofu Mkuu alitoa ushahidi wa hospitali zilizojengwa na Serikali katika Wilaya ya Ifakara, Ngara na Muheza ambazo kwa mujibu wa Mkataba wa 1993, Serikali haikutakiwa kujenga hospitali hizo za Wilaya.

Kitendo cha Serikali kujenga hospitali hizo kinatafsiriwa na Kanisa kuwa Serikali imevunja Mkataba kwa sababu sasa inatoa huduma hiyo muhumu kwa wananchi.

Askofu Mkuu alifafanua kua matatizo haya yapo kwenye ngazi ya Wilaya kwa sababu kwenye ngazi za juu, hakuna tatizo kwa kuwa kuna Msimamizi anaesimamia Mkataba huo.

Hapa Askofu Mkuu alikuwa ana maana kuwa hospitali za KCMC ya Moshi, Bugando ya Mwanza na CCBRT ya Dar es Salaam ambazo zote ni mali ya Kanisa bado zinaendelea kupata fedha za kodi huku zikiendelea kuwalipisha wananchi kwa huduma wanazopewa kwenye hospitali hizo.

Rais Samia Suluhu Hassan alifanya Mkutano na Baraza la Maaskofu la Kanisa Katoliki Tanzania uliofanyika Kurasini tarehe 25 Juni 2021. Katika risala yao, Baraza la Maaskofu limeilaumu Serikali kwa kujenga hospitali zake kinyume cha Mkataba wa 1992, na Makanisa.

Kwenye risala hiyo, Baraza la Maaskofu limeshangaa kuona Serikali inajenga hospitali kwenye Wilaya ambazo Makanisa tayari yana hospitali zao. Wamehoji kwa nini kuwepo na ushindani wa kutoa huduma hizo?

Kwa maana nyepesi, kwa nini Makanisa yasiachiwe kuendesha hospitali maisha (milele) na kuendelea kupewa ruzuku zinazotokana na kodi za wananchi?

Risala hiyo ni ya chombo cha juu kabisa katika Kanisa Katoliki ambao leo viongozi hao hao wanaohoji na kulalamika kuhusu makubaliano ya Serikali na DP World kuwa hayana ukomo!

Kanisa hilo hilo ambalo linapiga kelele kuhusu mkataba wa Serikali na DP World, ndilo ambalo kiongozi wake Askofu Method Kilaini alipewa shs. 80.9 milioni, Askofu Eusebius Nzigirwa alipewa shs. 40.4 milioni na Mchungaji Alphonce Twimanye Simon alipewa shs 40.4 milioni fedha za Rushwa zilizotokana na kashfa ya akaunti ya Tegeta ESCROW.

Hadi leo Kanisa halijatangaza hadharani hatua za kinidhamu iliyowachukulia viongozi hao. Ukimya huu tuutafsiri vipi? Kwa ukimya huu, Kanisa linapata wapi “moral authority” ya kupinga mkataba wa DP World.

Watanzania hawajasau wakati wa utawala wa Magufuli wameshuhudia mauwaji kule Kibiti na Rufiji ambayo ni Wilaya zenye Waislamu wengi. Watanzania bado wanakumbuka viroba vyenye miili ya watu vilivyokuwa vinaokotwa Coco Beach kila uchao.

Kanisa lilikuwa wapi wakati Magufuli anatoa roho za watu wasio na hatia? Masheikh wangapi wamepotea ambao mpaka leo hawajulikani walipo wakati wa utawala wa Magufuli?

Hao waliobahatika wametoka jela wakiwa vilema kama alivyo Sheikh Abdallah Maginga Wambura ambaye kakatwa mguu kutokana na vipigo vya Polisi?

Yuko wapi mwanasiasa Ben Saanane ambaye “kosa” lake ni kuandika kuwa PhD ya Magufuli ni feki? Yuko wapi Mwandishi Azory Gwanda ambaye “kosa” lake lilikuwa kuandika ukweli kuhusu mauwaji ya Kibiti?

Wakati wa utawala wa Magufuli, Mbunge wa Kilwa Kusini Mhe Selemani Bungara maarfu “Bwege” aliwahi kusema Bungeni kuwa raia wake walichukuliwa na askari msikitini na wamepotea mpaka leo hawajulikani walipo. Kanisa halikuyaona haya?

Kama Kanisa ilifumbia macho udhalimu na ukatili huu, leo wanapata wapi mdomo wa kukemea hicho wanachokiita mkataba usio na maslahi kwa wananchi?

Ni wananchi gani hao ambao leo Kanisa linajifanya kuwatetea?

Saa Watanzania wanakumbuka kuwa pamoja na ukatili wote wa Magufuli, ni viongozi hao hao wa Kanisa waliokuwa wakimkaribisha kila Jumapili kwenye Makanisa yao na kumpa nafasi ya kuzungumza. Leo Kanisa linataka kuwadanganya Watanzania kuwa lina maslahi na wananchi?

Kuna kitu kikubwa zaidi ya uhai? Wakati watu wanatolewa roho zao na Magufuli Kanisa lilikuwa wapi?

KWANINI WAKRISTO WANAPINGA MKATABA WA BANDARI

Mpaka sasa si Makanisa wala Wanasiasa ambao wametoa hoja ya kiuchumi. Tofauti na Wamarekani ambao walisema hadharani kuwa hawawezi kuwapa Waarabu kuendesha Bandari zao, hapa Tanzania sababu haswa ya kupinga Mkataba haisemwi hadharani.

Vinatafutwa visingizio tu. Ukweli ni kuwa Mkataba wa Bandari unapingwa na kuwepo kwa fikra potofu za Kanisa kuwa:

Iwapo DP World watapewa zabuni ya kuendesha Bandari, uwepo wao Tanzania utawanufaisha Waislam kwa namna moja au nyingine.

Kuna wanaohofia kuwa iwapo Bandari itafanikiwa, na endapo itatokea fursa ya miradi mingine mikubwa ya kiuchumi, Dubai watakuwa na nafasi nzuri ya kupewa miradi hiyo. Kwa hiyo kuwepo kwao kutaimarisha Uislamu.

Ikiwa DP World watapata tenda ya Bandari, nchi itapata mafanikio makubwa ya kiuchumi ambayo kwa fikra zao potofu yatakuwa yameletwa na Rais Mwislamu. Kwa maana hiyo, Waislamu wanaweza kuongoza nchi kwa ufanisi. Tayari kuna watu wanaosema kuwa Samia awe Rais wa mwisho Mwislamu Tanzania

Kuna wanaosema Bandari ikipata mafanikio itaonekana kuwa kumbe Wanawake wanaweza kuongoza nchi vizuri
Kuna wasemao kuwa Bandari ikifanikiwa itaonekana Wanzanzibari nao wana uwezo sawa na wa Bara katika kuliongoza taifa letu.

Hoja zote hizo ni za kipuuzi. Mafanikio yakiletwa na Rais Mwislamu au mwanamke au Mzanzibari wataonufaika ni wananchi wote.

Fedha za Bandari zitawanufaisha WOTE kwani anaepanga matumizi ya fedha ni Bunge letu ambalo lina Wabunge Waislamu, Wakristo na wasiokuwa na dini.

MWISHO

Nchi hii Waislamu wamekuwa wakidai kuwa Tanzania ni NCHI YETU SOTE

Waislamu wamekuwa wakidai kuwa idadi yao ni kubwa

Waislamu wanajigamba kuwa wamesoma lakini hawapewi fursa sawa

Kinachoshangaza ni kuwa tokea Mjadala wa Bandari uanze na hata mijadala mingine inayohusu UDINI huwasikii Waislamu kusema lolote. Wao ni kimyaaaaaaaaaa.

Mjadala wa Bandari umetawaliwa na viongozi wa dini ya Kikristo, Wasomi Wakristo, Taasisi za Kikristo na hata wanasheria waliofungua kesi Mahakamani ni Wakristo.

Kwenye mjadala wa Bandari kuna mafunzo kwa Waislamu.

MWENYEZIMUNGU ASHUHUDIE TUMEFIKISHA
 
Huo mkataba uletwe hadharani tuchambue vipengere vyake kwanini kanisa aneficha huo mkataba kama uko fair........kuna kilichofichwa nyuma ya pazia wananchi tunapigwa na kinisa iwe je serikali iendeshe hospitali zote za kanisa na shule wakati huo wanatoza ada kubwa kwa ajiri ya matibabu.
Kwani pale Muhimbili mnatibiwa bure? Mnadhihirisha upumbavu wenu kwa kutaka kuuelekeza mjadala wa DP World kuchukua sura ya udini.
 
Basi na misikiti ijenge yao ili pasiwe na wivu
Basi kila dini ijenge Hospitali zake kwa kutibia waumini wake na sisi tusioamini katika hizo dini za mashariki ya kati tutapiga nyungu kama jadi yatu inavyotuelekeza.
 
Kwa hiyo mnalipiza kisasi kwa mfano dhaifu kama huo!!! Hivi unafahamu hata muhimbili ilikuwa ya kanisa? Hizo hospitali zinatoa huduma sawa kwa watu wote, na huwa haziulizi dini yako ili kupewa upendeleo wa huduma.
Hata hivyo seriously umekaa ukafikiri ukaona hii hoja ya hospitali inafanana na kuuzwa kwa bandari? Kazi tunayo kwa hasara ya fikra tulizonazo.
Ndiyo wanazidi kujivua nguo
 
Mnahangaika tu, mkataba wa hovyo wa bandari na waarabu lazima uvunjwe.
 
Hilo neno ruzuku halijakaa vizuri hizo pesa hiwa ni kwa ajili ya wafanyakazi wa serikali waioko.kwenye hizo hospitali na ukumbuke.miundo.mbinu nyote na vifaa tiba huwa mali ya kanisa sio.serikali sababu uwezo wa serikali kujenga miundombinu mikubwa kama hiyo huwa hawana kwa maeneo yote ya nchi

Hivyo sehemu.ambazo uwezo haupo hutumia hizo za kanisa kuhudumia wananchi wake

Inakuwa gharama ndogo kwa serikali pia kuliko kujenga ya kwake eneo husika..Sababu kuna cost sharing.Kanisa linabeba na serikali inabeba kipande chake kuliko.zigo.lote la hospitali hiyo lingekuwa.zigo la serikali pekee
Ni ruzuku,acha ujinga
 
Zote hizo ni hospital za kanisa ziliporwa na Serikali,sawa na majengo ya NHC Serikali iliwapora kibabe wahindi.
Ni wakati Sasa Serikali iwarudishie wahindi nyumba zao.
 
Unaota wewe

Waislamu na nyie Jengeni hospitali kubwa zenye hadhi kubwa mahali ambako serikali haina hospitali Serikali itaingia ubia na nyie

Na sio.ubia hasa serikali huwa inapanga kutumia majengo ya hizo hospitali.kwa kutoa baadhi ya huduma.za afya kwa wote zilizo.kwenye mipango yake.Kwa kupeleka wafanyakazi wake,nk .Hivyo hizo hospitali huwa na vitengo viwili cha kanisa na cha serikali. Hicho kinaitwa pesa inalipwa hospitali ya kanisa ni gharama za mishahara ya wafanyakazi wa serikali waliopo hapo na uendeshaji wa shughuli zao na kodi serikali inalipa kutumia miundombinu ya kanisa iliyoko kwenye hiyo hospitali

Si kuwa serikali inamiliki hizo hospitali au ina hisa hapana.Na serikali ikiamua hata kesho kuondoa wafanyakazi wake Hospitali itaendelea na wa kwake bila shida.
Kwa hiyo mwanza na Kilimanjaro hapakua na hospital za serikali!?..kichwa kikubwa ka buyu kimejaa mbegu tu
 
Unaota wewe

Waislamu na nyie Jengeni hospitali kubwa zenye hadhi kubwa mahali ambako serikali haina hospitali Serikali itaingia ubia na nyie

Na sio.ubia hasa serikali huwa inapanga kutumia majengo ya hizo hospitali.kwa kutoa baadhi ya huduma.za afya kwa wote zilizo.kwenye mipango yake.Kwa kupeleka wafanyakazi wake,nk .Hivyo hizo hospitali huwa na vitengo viwili cha kanisa na cha serikali. Hicho kinaitwa pesa inalipwa hospitali ya kanisa ni gharama za mishahara ya wafanyakazi wa serikali waliopo hapo na uendeshaji wa shughuli zao na kodi serikali inalipa kutumia miundombinu ya kanisa iliyoko kwenye hiyo hospitali

Si kuwa serikali inamiliki hizo hospitali au ina hisa hapana.Na serikali ikiamua hata kesho kuondoa wafanyakazi wake Hospitali itaendelea na wa kwake bila shida.
Kwa hiyo mwanza na Kilimanjaro hapakua na hospital za serikali!?..kichwa kikubwa ka buyu kimejaa mbegu tu
Kwani vilijengwa na waislamu? Ni wazungu ndio walijenga
 
Kila kitu kina pande mbili positive na negative. Sasa tukijadili hayo swali ni je serikali yetu inauwezo wakuhudumia hao wagonjwa?
Nikukumbushe jambo moja dogo kwa usalama wa nchi?

1. Tulikuwa na viongozi wakubwa wa nchi hii ambao umauti uliwakuta wakiwa nchi jirani ( hospitali za wenzetu ). Hivi kama viongozi hao wanaumwa na wanapelekwa nje? unadhani ndani ya nchi kutakuwa na huduma yeyote ya afya hata yakuweza kuwahudumia raia wake wakiwa wagonjwa?
Nadhani ni wakati wa kuwa na sheria ya kuwataka viongozi wote wa umma wawe wadau wa kwanza wa huduma zote za kijamii zinazotolewa na umma. Watoto wao wasome shule za umma, watumie usafiri wa umma, hospitali za umma nakadhalika.. sina uhakika kama kuna Mheshimiwa mbunge hata mmoja anayesomesha mtoto kwenye shule ya umma.. inasikitisha.
 
Kabla ya kujadili mkataba tambua baada ya kupata uhuru shule na hospital za dini nyingi zilitaifishwa baadae wakati wa utawala wa awamu ya pili walitaka kurudishiwa Mali zao ila ikaonekana kutakuwa na pengo kubwa kati ya dini mbili kubwa badala yake serikali ikaingia mkataba wa mou kuwa haitataifisha Mali za taasisi za dini na pia serikali italipia baadhi ya wahudumu kama madaktari , manesi na wataalamu wengine.
Hovyo vitu vipo wazi nimeeleza kwa kifupi
 
Back
Top Bottom