Tupate mkataba wa uendeshi wa hospital za Bugando (TEC) na KCMC (KKKT) ili tujadili bandari vizuri

Tupate mkataba wa uendeshi wa hospital za Bugando (TEC) na KCMC (KKKT) ili tujadili bandari vizuri

  • Mkataba baina ya serikali na hosptali/vituo vya afya vya RC unaweza kuvunjwa ikiwa pande unaotaka kuvunja utatoa 'notice' miaka 3 kabla ya tarehe ya kusudio.
  • DP kaokota dodo mbivu: BANDARI ZOTE ZA BAHARI NA MAZIWA, NA SPECIAL ECONOMIC ZONE ni Mali yake milele. Yaani kampuni inamiliki utajiri wote muhimu wa nchi, hata kama isipiendeleza miongo kadhaa.
DP World masharti yake ni kama yanasema "nikija kukaa kwako, itabidi unipe na mke wako, watoto nao surname inabidi wabadilishe watumie ya kwangu. Mali zako uzihamishie kwenye jina langu"
 
;labda tuanze na agakhani kwanini inapewa misamaha ya Kodi wakati huduma zake ni gharama kubwa
 
Kwa hiyo mwanza na Kilimanjaro hapakua na hospital za serikali!?..kichwa kikubwa ka buyu kimejaa mbegu tu
Serikali kule Mwanza na kilimanjaro hawana hospitali ya Rufaa wana za kawaida tu tena za kawaida mno
 
Serikali kule Mwanza na kilimanjaro hawana hospitali ya Rufaa wana za kawaida tu tena za kawaida mno
Wote tunajua hospitali za manispaa zikoje,Wacha uwongo,na hata kipindi hicho watz hawakuwa wakijaa hospital Kama sokoni Kama ilivyo siku hizi,huduma za hospital za mikoa zilitosha kabisa
 
bugando na kcmc zote ni za serikali nyerere mungu amlaani ndio aliyewapa makanisa na serikali inalipa mishahara hapati chochote na haina ubia wala sheya, katika marais walioivuranga tanzania ni nyerere, kataifisha majumba ya waislamu kawapa NHC katuletea bakwata kuuwa uislamu, bakwata ni wakristo walivaa kanzu
Hatimaye sasa mkataba unapandikiza udini, nashauri watanzania tuwe makini sana maana uhakika nilionao ni kuwa udini huishia pabaya
 
Hospital za Bugando na KCMC zinamilikiwa na makanisa na zinaendeshwa kwa ubia na serikali ya JMT. Ninafikiri mikataba yake ingetusaidia sana kwenye mjadala unaoendelea wa bandari
Kwani Serikali ilihusika katika ujenzi
Shida ya nchii hii Vilaza ni wengii Sana.

Unawezaje kufananisha bandari taasisi ya Serikali na taasisi ya Dini flani.

Wakojani bwana sijui vichwa vyenu mnaswith off wakati flanii
 
Hospital za Bugando na KCMC zinamilikiwa na makanisa na zinaendeshwa kwa ubia na serikali ya JMT. Ninafikiri mikataba yake ingetusaidia sana kwenye mjadala unaoendelea wa bandari
kuendeshwa kwa ubia maana yake serikali iliona inahitaji huduma zake hasa kwa ajili ya wananchi na kwa ajili ya kuajiri watumishi ambao wanalipwa na serikali (not sure kama ziko designated kama zingine ), na zinatibu waislam na wakristo. na hii inatokana na kwamba watu wengine ni wavivu na wasiojali elimu na huduma kwa jamii bali kuabudu na hawakuwa na kitu cha kuleta mbele ya serikali ili nao waingie mou. na watu hao hao ndio walalamishi na wakimaliza kulalamika wanaenda kutibiwa kwenye hospitali hizo hizo. aliyewaloga mnatakiwa mumlaumu sana na ana moto wake special.
 
;labda tuanze na agakhani kwanini inapewa misamaha ya Kodi wakati huduma zake ni gharama kubwa
Kuna vitu vingine havisemwi

Nianze kueleza kwanza maana ya kutaifisha ni nini? Kutaifisha sio.kuchukua mali ya mtu binafsi au taasisi ya dini bure la hapana .Ni kuwa unaamua kuinumua mali yake si kwa malipo ya mkupuo bali ya muda mrefu taratibu kila mwaka unamlipa kiasi fulani hadi deni liishe

Sasa nini kilitokea ? Serikali ilitaifisha mashule na mahospitali ya taasisi za dini kibao ikiwemo.taasisi za Agha Khan nk serikali ikafanya Mwanzoni malipo yalikuwa yakienda vizuri baadaye hasa baada ya vita ya Uganda na Tanzania hali ikawa mbaya kifedha madeni hayalipiki.Ndipo baadaye serikali ikaona wakae wajadiliane na taasisi wanazoshindwa kulipa wawalipe.kwa utaratibu upi mbadala? Ndio.mahesabu yakspigwa kuwa serikali kupunguza madeni irudishe baadhi ya shule na Hospitali kwa wenyewe na zikabuniwa njia xongine za kulipa hayo madeni ikiwemo hiyo misanaha ya kodi nk mfano waislamu walipewa bure majengo ya chuo kikuu chao kilichoko Morogoro kilichokuwa chuo cha Tanesco

Gharama za kutaifisha vya watu matokeo yake ndio hayo na mengine yakaja ya ubinafsishaji kuuza mali.zilizotaifoshwa kwa wawekezaji serikali ipate pesa ipunguze mzigo wa madeni na kulipa
 
Kwani Serikali ilihusika katika ujenzi
Shida ya nchii hii Vilaza ni wengii Sana.

Unawezaje kufananisha bandari taasisi ya Serikali na taasisi ya Dini flani.

Wakojani bwana sijui vichwa vyenu mnaswith off wakati flanii
simple, kama serikali haikuhusika na ujenzi, majengo ni ya kanisa, serikali si iondoke ione kama kanisa litashindwa? sisi uwa tunatumia sadaka na huwa tunatoa sana sadaka. tunaweza kujiendesha bila serikali kama mkiona vipi. na ikiwa hivyo sijui mtatafuta hospitali zenu za kwenda kutibiwa? au mtakuja tu kwasababu sisi huwa hatulipizi kisasi tutawapokea tu, Mungu wetu ni wa upendo.
 
  • Mkataba baina ya serikali na hosptali/vituo vya afya vya RC unaweza kuvunjwa ikiwa pande unaotaka kuvunja utatoa 'notice' miaka 3 kabla ya tarehe ya kusudio.
  • DP kaokota dodo mbivu: BANDARI ZOTE ZA BAHARI NA MAZIWA, NA SPECIAL ECONOMIC ZONE ni Mali yake milele. Yaani kampuni inamiliki utajiri wote muhimu wa nchi, hata kama isipiendeleza miongo kadhaa.
DP kaokota dodo hasa, manake amekuta kila kitu kimejengwa, yeye kuendesha tu, na anataka amilikishwe ardhi ambayo tayari imeshajengwa miundombinu. si aseme tu anataka tumpe majengo yote ya mandari bure ili yeye apige pesa? na atuzuie tusishindane na bandari zake za DUBAI.
 
Hospital za Bugando na KCMC zinamilikiwa na makanisa na zinaendeshwa kwa ubia na serikali ya JMT. Ninafikiri mikataba yake ingetusaidia sana kwenye mjadala unaoendelea wa bandari
Mjinga ka wewe sijui unaendeleaje kuishi, better ungekufa. Badala ya kujenda hoja unaharibu kabisa dhamira safi ya rais Samia. Hivi unadhani wanaopona kwa kutibiwa KCMC au Bugando ni wa kristo tu??? Idiot kabisa.
 
Hizi hospitali zilijengwa na makanisa lakini zilitaifishwa na serikali ikazichukua 100%. Serikali ilipoona zinawashinda ndio zikaomba waliozijenga wazichukue tena kwa makubaliano kuwa zitatumika kama hospitali za rufaa. Hizi hospitali zinamilikiwa 100% na makanisa, hela zinazotoka hospitali ni kuziwesha ziendelee kutoa huduma kwa gharama ambayo wewe na mimi tunaweza kumudu. Hii ni tofauti na hospitali ya Aga Khan inayomilikiwa na taasisi ya Kiislamu ya kiismailia ambayo hawana ushirikiano na serikali. Wote tunajua gharama za Aga Khan au ile ya wahindu ya Hindu Mandal. Mnatakiwa kuwashukuru wakatoliki na walutheri kukubali hospitali zitumike kama hospitali za rufaa. Msijidanganye kuwa haziwezi kujiendesha bila ushiriki wa serikali. Ushirikiano huo ukifa kama mnavyotaka watapandisha gharama zao na zitakuwa kama za Aga Khan.

Amandla...
Fact! Na tunataka bandari zetu zibaki kuwa mali yetu daima.
 
Hizi hospitali zilijengwa na makanisa lakini zilitaifishwa na serikali ikazichukua 100%. Serikali ilipoona zinawashinda ndio zikaomba waliozijenga wazichukue tena kwa makubaliano kuwa zitatumika kama hospitali za rufaa. Hizi hospitali zinamilikiwa 100% na makanisa, hela zinazotoka hospitali ni kuziwesha ziendelee kutoa huduma kwa gharama ambayo wewe na mimi tunaweza kumudu. Hii ni tofauti na hospitali ya Aga Khan inayomilikiwa na taasisi ya Kiislamu ya kiismailia ambayo hawana ushirikiano na serikali. Wote tunajua gharama za Aga Khan au ile ya wahindu ya Hindu Mandal. Mnatakiwa kuwashukuru wakatoliki na walutheri kukubali hospitali zitumike kama hospitali za rufaa. Msijidanganye kuwa haziwezi kujiendesha bila ushiriki wa serikali. Ushirikiano huo ukifa kama mnavyotaka watapandisha gharama zao na zitakuwa kama za Aga Khan.

Amandla...
Weka mkataba acha maelezo
 
Ni pale wadau wanapogombana na kurushiana maneno kwa Imani zilizokuja na Merikebu ili ku-justify kumilikishwa mali zao nyingine kwa mgeni....

Makes you wonder...., "How did we Get Here"!!!!!!!!!
 
WACHATUSEME NA.2

TANZANIA NI YETU SOTE SIO MALI YA WAKRISTO

Hivi karibuni kumezuka mjadala mkali kuhusu Serikali kuingia kwenye makubaliano ya kuendesha Bandari za Tanzania na kampuni ya DP World. Mjadala huu ulianza na sura ya kisiasa wakati Mwenyekiti wa Chadema Bwana Freeman Mbowe alipotoa shutuma kali kuwa Bandari za Tanganyika zinauzwa na Wazanzibari yaani Waziri wa Ujenzi, Mhe Makame Mbarawa na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan.

Lakini ghafla mjadala ukahama kwenye Siasa na ukatawaliwa na hisia kali za kidini. Sote tumeshuhudia namna viongozi wa dini ya Kikristo hasa wakatoliki wakiongozwa na Kadinali Pengo walivyokuwa wakilipigia kelele suala la Bandari.

Hoja zinazotawala mjadala huu ni mbili. Hoja ya kwanza ni kwamba mkataba ule umesainiwa na Waziri Mzanzibari na Rais Mzanzibari na kwamba Wanzanzibari hawa wawili wanauza mali za Tanganyika. Hoja yao ya pili inadai kuwa mkataba hauna ukomo wa muda, yaani ni mkataba wa milele. Hii hoja hii ya pili inashabikiwa sana na viongozi wa Kanisa.

Jambo la kushangaza ni kuwa mpaka sasa hakuna hata msemaji mmoja, awe mwanasiasa au kiongozi wa Kanisa aliyetoa hoja za kiuchumi na utendaji za kupinga makubaliano hayo.

Badala yake, viongozi wengine kama vile mama Anna Tibaijuka anadiriki kusema uwongo kuhusu sababu za DP World kukataliwa kuendesha Bandari za Marekani. Mama Tibaijuka anajua vyema lakini hakutaka kusema kuwa sababu ya kukataliwa kuongoza Bandari za New York na New Jersey ni Uwarabu wao na wala si utendaji wao.

Ni kweli Bunge la Marekani lilikataa DP World wasipewe Bandari hizo lakini walisema wazi kuwa Marekani haiwezi kuwapa Waarabu kuendesha Bandari zao kwa sababu za kiusalama. Hakuna asiejua msimamo wa Marekani kuhusu Waarabu na Waislamu.

Kwa makusudi kabisa, mama huyu anapotosha watu kwa kufananisha suala la Bandari za Marekani na Bandari za Dar es Salaam. Kwenye suala la Dar es Salaam, DP World haikutaka kununua TPA. Inachopendeza ni kuendesha na si kununua Bandari ya Dar es Salaam.

Suala hili la kuendesha si geni Tanzania. Kampuni ya TICTS imeendesha Bandari ya Dar es Salaam kwa zaidi ya miaka 20. Kampuni ya “Swissport” inaendesha Kiwanja cha Ndege cha Dar es Salaam kwa muda mrefu. Mbona hizi kelele hatukuzisikia?

Wakati wa utawala wa Donald Trump Marekani ilifika hatua ya kupiga marufuku baadhi ya Mataifa ya Arabuni kwa maana Waislamu kuingia Marekani. Kwa hiyo mama Tibaijuka hakutaka kuwa mkweli kuhusu suala hili.

Ametumia kivuli chake cha kuwa mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa kwa wakati ule kuwaaminisha Watanzania kuwa yeye anafahamu zaidi kuhusu ubaya wa DP World.

Mama Tibaijuka amekosa uadilifu (moral authority) wa kuweza kukemea kile alichokiita mkataba mbovu kwa sababu wakati kampuni ya TICTS iliyokuwa inaendesha Bandari ya DSM kwa utendaji wa hovyo huyu mama alikaa kimya hata pale ambapo TICTS walipopewa nyongeza ya mkataba wa miaka 15 bila kufuata sheria za manunuzi.

Lakini jambo la pili, nani asiyejua kuwa mama Anna Tibaijuka alikiri hadharani kuwa alipokea shs 1.6 bilioni ya fedha za rushwa za ESCROW? Huyu mama ambaye alisema kwa majigambo kuwa shs 1.6 bilioni ni pesa ya mboga ana uchungu gani wa kuwatetea Watanzania masikini?

Bado tunarejea kusema tena kwa kinywa kipana, mpaka sasa hakuna mtu hata mmoja aliyesema kwa kuonesha ushahidi kuwa DP World hawana uwezo kifedha au utendaji wao ni mbovu. Hakuna aliyesema kuwa hizo fedha ambazo tunaahidiwa ni ahadi hewa kwa sababu DP World hawana uwezo wa kuvutia mizigo kupitia Bandari ya Dar es Salaam.

Kwa kuwa mjadala umetawaliwa na CHUKI za kidini na wasemaji wakubwa wamekuwa viongozi wa Kanisa. Tukumbuke kuwa ni Wakristo hao hao ambao mmoja kati ya viongozi wao waliosema kuwa Rais Samia anafanana na muuza vitumbua! Makanisa hawakukemea kauli hii ya kumkosea adabu Rais.

Kwa kuwa mjadala wa Bandari una chuki za udini, naomba tujikumbushe nafasi ya Makanisa katika nchi hii.

TUKUMBUKE MWAKA 1992

Mwaka 1992, Serikali iliingia Mkataba na Makanisa kupitia Taasisi zao za TEC na CCT. Chini ya Makubaliano yale, hospitali za Makanisa zitatumika kwa wananchi wote pale ambapo Serikali haina hospitali.

Kwa kufanya hivyo, Serikali itakuwa na wajibu wa kuyapa Makanisa fedha za kuendesha hospitali hizo ingawa umiliki wa hospitali utabaki kuwa wa Makanisa.

Ifahamike kuwa fedha hizo zinatokana na kodI za Watanzania wote; Waislamu, Wakristo, Mabaniani, Magoha, Makadiani, na hata wale wasio na dini.

Nini athari za Mkataba huu ? Mkataba huu wa kibaguzi una athari nyingi. Kwanza:

Serikali inatumia kodi za wananchi kuyapa Makanisa kuendesha shughuli zake za kuimarisha Ukristo.

Tunasema hivyo kwa sababu utaratibu unaotumika ni kuwa Serikali inatoa fedha kwa Makanisa ambayo wao ndio wanapanga matumizi ya fedha zile na sio Serikali.

Pili, kwenye Jamii, Makanisa yanaonekana ndio yanatoa huduma za Jamii na hivyo kujenga saikolojia kwa wananchi kuwa Ukristo ndio unajali wananchi.

Athari ya tatu ni kuwa Makanisa yananyonya wananchi kwa sababu pamoja ya kuwa hospitali zile zinapata fedha kutoka Serikalini, bado wananchi wanalipia huduma.

Nne, Mkataba hauna ukomo, yaani ni wa milele. (Wakristo wataendelea kupewa hayo mabilioni na Waislamu watanyimwa milele).

Kwa tafsiri nyingine ni kuwa Serikali imejivua kwenye wajibu wa kutoa huduma za Jamii na kuchagua Makanisa kuwa ndio wakala wake.

Tunapenda kuwakumbusha Watanzania kuwa wakati Mkataba huo unasainiwa aliyesaini Mkataba ni Bwana Edward Lowassa aliyekuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu. Huyu ni Mkristo

Kwa utaratibu wa Serikali, Lowassa alikuwa Waziri wa Nchi, hivyo basi Waziri mwenye dhamana ni yule mwenye ofisi yake kwa maana ni Waziri Mkuu.

Wakati unatiwa saini Mkataba, huo Waziri Mkuu alikuwa John Samwel Malecela ambaye ni Mkristo.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ndie aliyeishauri Serikali isaini Mkataba ule ambao kwanza hauna ukomo (mkataba wa maisha) na pili unatumia kodi za wananchi kuimarisha Ukristo alikuwa Damian Lubuva ambaye ni Mkristo.

Kwa upande wa Kanisa mwanasheria wao alikuwa Prof Balozi Costa Mahalu, Mkristo.
Kwa maana hiyo, upande wa Serikali, Mkataba ule umeasisiwa na kusimamimwa na Wakristo watupu. Waziri wa Nchi Mkristo, Waziri Mkuu Mkristo, Mwanasheria Mkuu Mkristo.

Ni Wakristo! Wakristo! Wakristo!

Kama kwenye hoja ya makubaliano ya Bandari ni Wazanzibari wawili (ambao ni Waislamu) wamesaini makubaliano ya kuiuza Tanganyika, Mbona Waislamu hawakulalamika pale Wakristo 3 wazito Serikalini walipobuni mbinu za kutumia kodi za wananchi kuimarisha dini yao Ukristo Tanzania?

Kama hoja ni ukomo wa mkataba, mbona Mkataba huu wa Serikali na Makanisa hauna ukomo? Ni mkataba wa milele na ndio maana mpaka leo (miaka 30 sasa) bado unaendelea kutumika.

Bado Serikali inaendelea kutekeleza Mkataba wa kibaguzi ambapo inatumia kodi za wananchi wote kuimarisha shughuli za Kanisa.

USHAHIDI

Tarehe 23 Januari 2019, Rais Magufuli alikutana na viongozi wa dini zote IKULU. Kwenye Mkutano ule Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Tanga Bwana Maimo Mndolwa alilalamika kwa Rais Magufuli kuwa Serikali inavunja Mkataba kwa kujenga hospitali kwenye maeneo ambayo Kanisa imeachiwa kuwa na hosptali ambazo zinapewa fedha na Serikali.
Amelalamika hivyo kwa sababu Mkataba wa Makanisa na Serikali hauna ukomo. Kila penye hospitali ya Kanisa, Serikali haikutakiwa kujenga hospitali yake. Badala yake, Serikali inatakiwa kuendelea kutoa fedha za kodi kuwapa Makanisa ili ziendeshe hospitali zao na kuimarisha Ukristo kwa kutumia jasho la Watanzania.

Katika kusisitiza madai yake, Askofu Mkuu alitoa ushahidi wa hospitali zilizojengwa na Serikali katika Wilaya ya Ifakara, Ngara na Muheza ambazo kwa mujibu wa Mkataba wa 1993, Serikali haikutakiwa kujenga hospitali hizo za Wilaya.

Kitendo cha Serikali kujenga hospitali hizo kinatafsiriwa na Kanisa kuwa Serikali imevunja Mkataba kwa sababu sasa inatoa huduma hiyo muhumu kwa wananchi.

Askofu Mkuu alifafanua kua matatizo haya yapo kwenye ngazi ya Wilaya kwa sababu kwenye ngazi za juu, hakuna tatizo kwa kuwa kuna Msimamizi anaesimamia Mkataba huo.

Hapa Askofu Mkuu alikuwa ana maana kuwa hospitali za KCMC ya Moshi, Bugando ya Mwanza na CCBRT ya Dar es Salaam ambazo zote ni mali ya Kanisa bado zinaendelea kupata fedha za kodi huku zikiendelea kuwalipisha wananchi kwa huduma wanazopewa kwenye hospitali hizo.

Rais Samia Suluhu Hassan alifanya Mkutano na Baraza la Maaskofu la Kanisa Katoliki Tanzania uliofanyika Kurasini tarehe 25 Juni 2021. Katika risala yao, Baraza la Maaskofu limeilaumu Serikali kwa kujenga hospitali zake kinyume cha Mkataba wa 1992, na Makanisa.

Kwenye risala hiyo, Baraza la Maaskofu limeshangaa kuona Serikali inajenga hospitali kwenye Wilaya ambazo Makanisa tayari yana hospitali zao. Wamehoji kwa nini kuwepo na ushindani wa kutoa huduma hizo?

Kwa maana nyepesi, kwa nini Makanisa yasiachiwe kuendesha hospitali maisha (milele) na kuendelea kupewa ruzuku zinazotokana na kodi za wananchi?

Risala hiyo ni ya chombo cha juu kabisa katika Kanisa Katoliki ambao leo viongozi hao hao wanaohoji na kulalamika kuhusu makubaliano ya Serikali na DP World kuwa hayana ukomo!

Kanisa hilo hilo ambalo linapiga kelele kuhusu mkataba wa Serikali na DP World, ndilo ambalo kiongozi wake Askofu Method Kilaini alipewa shs. 80.9 milioni, Askofu Eusebius Nzigirwa alipewa shs. 40.4 milioni na Mchungaji Alphonce Twimanye Simon alipewa shs 40.4 milioni fedha za Rushwa zilizotokana na kashfa ya akaunti ya Tegeta ESCROW.

Hadi leo Kanisa halijatangaza hadharani hatua za kinidhamu iliyowachukulia viongozi hao. Ukimya huu tuutafsiri vipi? Kwa ukimya huu, Kanisa linapata wapi “moral authority” ya kupinga mkataba wa DP World.

Watanzania hawajasau wakati wa utawala wa Magufuli wameshuhudia mauwaji kule Kibiti na Rufiji ambayo ni Wilaya zenye Waislamu wengi. Watanzania bado wanakumbuka viroba vyenye miili ya watu vilivyokuwa vinaokotwa Coco Beach kila uchao.

Kanisa lilikuwa wapi wakati Magufuli anatoa roho za watu wasio na hatia? Masheikh wangapi wamepotea ambao mpaka leo hawajulikani walipo wakati wa utawala wa Magufuli?

Hao waliobahatika wametoka jela wakiwa vilema kama alivyo Sheikh Abdallah Maginga Wambura ambaye kakatwa mguu kutokana na vipigo vya Polisi?

Yuko wapi mwanasiasa Ben Saanane ambaye “kosa” lake ni kuandika kuwa PhD ya Magufuli ni feki? Yuko wapi Mwandishi Azory Gwanda ambaye “kosa” lake lilikuwa kuandika ukweli kuhusu mauwaji ya Kibiti?

Wakati wa utawala wa Magufuli, Mbunge wa Kilwa Kusini Mhe Selemani Bungara maarfu “Bwege” aliwahi kusema Bungeni kuwa raia wake walichukuliwa na askari msikitini na wamepotea mpaka leo hawajulikani walipo. Kanisa halikuyaona haya?

Kama Kanisa ilifumbia macho udhalimu na ukatili huu, leo wanapata wapi mdomo wa kukemea hicho wanachokiita mkataba usio na maslahi kwa wananchi?

Ni wananchi gani hao ambao leo Kanisa linajifanya kuwatetea?

Saa Watanzania wanakumbuka kuwa pamoja na ukatili wote wa Magufuli, ni viongozi hao hao wa Kanisa waliokuwa wakimkaribisha kila Jumapili kwenye Makanisa yao na kumpa nafasi ya kuzungumza. Leo Kanisa linataka kuwadanganya Watanzania kuwa lina maslahi na wananchi?

Kuna kitu kikubwa zaidi ya uhai? Wakati watu wanatolewa roho zao na Magufuli Kanisa lilikuwa wapi?

KWANINI WAKRISTO WANAPINGA MKATABA WA BANDARI

Mpaka sasa si Makanisa wala Wanasiasa ambao wametoa hoja ya kiuchumi. Tofauti na Wamarekani ambao walisema hadharani kuwa hawawezi kuwapa Waarabu kuendesha Bandari zao, hapa Tanzania sababu haswa ya kupinga Mkataba haisemwi hadharani.

Vinatafutwa visingizio tu. Ukweli ni kuwa Mkataba wa Bandari unapingwa na kuwepo kwa fikra potofu za Kanisa kuwa:

Iwapo DP World watapewa zabuni ya kuendesha Bandari, uwepo wao Tanzania utawanufaisha Waislam kwa namna moja au nyingine.

Kuna wanaohofia kuwa iwapo Bandari itafanikiwa, na endapo itatokea fursa ya miradi mingine mikubwa ya kiuchumi, Dubai watakuwa na nafasi nzuri ya kupewa miradi hiyo. Kwa hiyo kuwepo kwao kutaimarisha Uislamu.

Ikiwa DP World watapata tenda ya Bandari, nchi itapata mafanikio makubwa ya kiuchumi ambayo kwa fikra zao potofu yatakuwa yameletwa na Rais Mwislamu. Kwa maana hiyo, Waislamu wanaweza kuongoza nchi kwa ufanisi. Tayari kuna watu wanaosema kuwa Samia awe Rais wa mwisho Mwislamu Tanzania

Kuna wanaosema Bandari ikipata mafanikio itaonekana kuwa kumbe Wanawake wanaweza kuongoza nchi vizuri
Kuna wasemao kuwa Bandari ikifanikiwa itaonekana Wanzanzibari nao wana uwezo sawa na wa Bara katika kuliongoza taifa letu.

Hoja zote hizo ni za kipuuzi. Mafanikio yakiletwa na Rais Mwislamu au mwanamke au Mzanzibari wataonufaika ni wananchi wote.

Fedha za Bandari zitawanufaisha WOTE kwani anaepanga matumizi ya fedha ni Bunge letu ambalo lina Wabunge Waislamu, Wakristo na wasiokuwa na dini.

MWISHO

Nchi hii Waislamu wamekuwa wakidai kuwa Tanzania ni NCHI YETU SOTE

Waislamu wamekuwa wakidai kuwa idadi yao ni kubwa

Waislamu wanajigamba kuwa wamesoma lakini hawapewi fursa sawa

Kinachoshangaza ni kuwa tokea Mjadala wa Bandari uanze na hata mijadala mingine inayohusu UDINI huwasikii Waislamu kusema lolote. Wao ni kimyaaaaaaaaaa.

Mjadala wa Bandari umetawaliwa na viongozi wa dini ya Kikristo, Wasomi Wakristo, Taasisi za Kikristo na hata wanasheria waliofungua kesi Mahakamani ni Wakristo.

Kwenye mjadala wa Bandari kuna mafunzo kwa Waislamu.

MWENYEZIMUNGU ASHUHUDIE TUMEFIKISHA
ASANTE NA KWELI UMESAMA
 
Back
Top Bottom