DALALI MKUU
JF-Expert Member
- May 7, 2022
- 2,011
- 4,705
Hiyo dogodogo siipati. ila sababu kuu ulizotaja ni hizo MkuuTUSHINDWE TENA.....TULIMCHOMOA
NA USIKU ULE ULE ALISAFIRISHWA KWA MJOMBA WAKE SONGEA
YAANI PALE MAMLAKA HUSIKA WAKISEMA WAENDE,WAPELEKE KABISA KARANDINGA KUWABEBA WOTE WAWATOE PALE
Ukiongea na baadhi ya watoto pale kila mmoja ana mkasa wake
Sana sana mambo ya kifamilia yamewakimbiza,sjui mama wa kambo,baba wa kambo
Wengine wazaz wote wamekufa familia haiwatazami tena,wengine akili zao ujeuri tu nk
Hivi dogodogo Centre ipo bado ?
Ova
Khaaaaah!! We sema kweliSana,ile ni dunia nyingine ujue
Na pale wana mpaka utawala wao
Ova
Safi Mh. Waziri kwa kutambua kuwa Jamii Forums kama mahali sahihi pa kupata ushauri, naamini humu ndani watu watatoa ushirikiano kwako.Heri ya Pasaka wana JamiiForums,
Mimi ni Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum.
Ninayo furaha kujiunga nanyi katika mtandao huu. Nimekuwepo hapa tangu 2015 kama msomaji zaidi lakini sasa rasmi nitakuwa active member.
Naamini JF itakuwa sehemu nzuri ya kupokea maswali, maoni na mawazo yenu kuhusu namna tunavyoweza kuboresha maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake, na watu wenye makundi maalum nchini Tanzania.
Hivyo, ninawakaribisha nyote kushiriki kwenye majadiliano haya na mimi niko tayari kujibu maswali yenu na kusikiliza maoni yenu na hata kuyafanyia kazi haraka pale inapobidi.
Unaweza kutoa maoni yako kwenye mjadala huu au kupitia ujumbe wa faragha (PM).
Karibuni
IpoNi jambo jema lonalopaswa kuigwa na wizara nyingine, lakini pia kama ingewezekana ingekuwa mungefungua official account ya wizara itapendeza zaidi
Maswali mengine niya Wizara ya Afya sio Maendeleo ya JamiiMh. Karibu sana... tunashida ya homosexual kwenye jamii na mashuleni kwa sasa.
Kama wizara mna kauli gani?
Mbili nini tathimini ya mitaala ya elimu ya msingi kwenye nchi yetu mpaka sasa hasa nimejikita kwenye malengo mahususi ni kweli yanafikiwa?
Asante.
Fanyeni homework yenu vizuri sio kutupa mpira. Hili linaigusa kwa sehemu kubwa jamii na maadili ni swala linalotishia ustawi wa jamii na maendeleo yao... wizara mnaona hamna cha kusema mpaka wizara ya afya?... huko napo wakisema ni swala la haki ya faragha tulipeleke wizara ya katiba na sheria? Ok nimekuelewa.Maswali mengine niya Wizara ya Afya sio Maendeleo ya Jamii
Avatar Yako haiendani na jibu lako..kuwa kuongezeka Kwa homesexuality mashuleni ni suala la Wizara ya Afya...?! Inawezekana upo hulumo Wizarani lakini hujui majukumu ya Wizara .Kama vipi waachie Wataalamu wajibu!Maswali mengine niya Wizara ya Afya sio Maendeleo ya Jamii
Mkuu hilo swali sio la wizara ya afya ni wizara ya jinsia na maendeleo ya jamii!Maswali mengine niya Wizara ya Afya sio Maendeleo ya Jamii
Unalosema ni kweli kabisaAvatar Yako haiendani na jibu lako..kuwa kuongezeka Kwa homesexuality mashuleni ni suala la Wizara ya Afya...?! Inawezekana upo hulumo Wizarani lakini hujui majukumu ya Wizara .Kama vipi waachie Wataalamu wajibu!
Homesexuality ni suala mtambuka.Linajusu sekta kadhaa ..hili ni suala la kijamii! Hapo kwenu Kuna Idara ya Ustawi wa Jamii ,ambayo inashughulikia na wellbeing ya binadamu!
Kama Idara hiyo ikipewa nafasi( Waitumie ) Wana jukumu kubwa la kushuhhulikia masuala haya!
Ni bahati mbaya sana ,wahusika aidha ,waelewinwajibu wao ,au hawajitambui! Na majibu Yako wewe ni dalili za hiki nikisemacho!
Homo sexuality iko ndani ya ustawi wa jamii, jinsiaa na maendeleo, ndani ya kundi maalumu.Maswali mengine niya Wizara ya Afya sio Maendeleo ya Jamii
Dokta nakupongeza kwa hatua hii adhimu kabisa ya kufungua mlango wa kupokea ushauri mbalimbali ili kuboresha Wizara hii muhimuHeri ya Pasaka wana JamiiForums,
Mimi ni Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum.
Ninayo furaha kujiunga nanyi katika mtandao huu. Nimekuwepo hapa tangu 2015 kama msomaji zaidi lakini sasa rasmi nitakuwa active member.
Naamini JF itakuwa sehemu nzuri ya kupokea maswali, maoni na mawazo yenu kuhusu namna tunavyoweza kuboresha maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake, na watu wenye makundi maalum nchini Tanzania.
Hivyo, ninawakaribisha nyote kushiriki kwenye majadiliano haya na mimi niko tayari kujibu maswali yenu na kusikiliza maoni yenu na hata kuyafanyia kazi haraka pale inapobidi.
Unaweza kutoa maoni yako kwenye mjadala huu au kupitia ujumbe wa faragha (PM).
Karibuni
Huyu sio WA kwanza ...yupo mwamba mwigulu nchembaKaribu Mh. Waziri, nakushukuru kwa kuwepo hapa JF kupata maoni mbalimbali na nikupongeze kwani huenda ndie Waziri wa kwanza wa serikali hii ya Mheshimiwa Mama Samia kujumuika na jamii hii ya wana JF.
Mimi naomba niwasilishe changamoto kuhusu ustawi wa watoto wetu katika jamii zetu. Watoto yatima na wazee wasiojiweza wamekuwa na shida kubwa wanapohitaji misaada ya matibabu ya afya.
Sera na miongozo ya matibabu ya kina mama wajawazito, watoto wadogo na wazee ipo lakini haisimamiwi ipasavyo katika ngazi za chini za huduma za afya kama vile zahanati na vituo vya kutolea huduma za afya.
Watoto, wazee na yatima wanataabika sana na kupelekea kua omba omba. Maafisa Ustawi wa Jamii na wasimamizi wa huduma za afya hawajali kabisa. Wameingiza siasa na matokea yake, utendaji wao umekua hafifu.
Naomba uwepo mfumo wa ufatiliaji wa huduma za afya kwa makundi maalumu ya jamii, na mfumo huu uishirikishe jamii moja kwa moja, yaani viongozi wa kidini, viongozi wa kisiasa na wengineo wapewe nguvu ya kuwasimamia watoa huduma wa msingi katika vituo vya afya na hospitali zetu.
Ahsante.