Tupe maoni, ushauri, dokezo: Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum

Tupe maoni, ushauri, dokezo: Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum

TUSHINDWE TENA.....TULIMCHOMOA
NA USIKU ULE ULE ALISAFIRISHWA KWA MJOMBA WAKE SONGEA
YAANI PALE MAMLAKA HUSIKA WAKISEMA WAENDE,WAPELEKE KABISA KARANDINGA KUWABEBA WOTE WAWATOE PALE

Ukiongea na baadhi ya watoto pale kila mmoja ana mkasa wake
Sana sana mambo ya kifamilia yamewakimbiza,sjui mama wa kambo,baba wa kambo
Wengine wazaz wote wamekufa familia haiwatazami tena,wengine akili zao ujeuri tu nk

Hivi dogodogo Centre ipo bado ?

Ova
Hiyo dogodogo siipati. ila sababu kuu ulizotaja ni hizo Mkuu
 
Heri ya Pasaka wana JamiiForums,

Mimi ni Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum.

Ninayo furaha kujiunga nanyi katika mtandao huu. Nimekuwepo hapa tangu 2015 kama msomaji zaidi lakini sasa rasmi nitakuwa active member.

Naamini JF itakuwa sehemu nzuri ya kupokea maswali, maoni na mawazo yenu kuhusu namna tunavyoweza kuboresha maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake, na watu wenye makundi maalum nchini Tanzania.

Hivyo, ninawakaribisha nyote kushiriki kwenye majadiliano haya na mimi niko tayari kujibu maswali yenu na kusikiliza maoni yenu na hata kuyafanyia kazi haraka pale inapobidi.

Unaweza kutoa maoni yako kwenye mjadala huu au kupitia ujumbe wa faragha (PM).

Karibuni
Safi Mh. Waziri kwa kutambua kuwa Jamii Forums kama mahali sahihi pa kupata ushauri, naamini humu ndani watu watatoa ushirikiano kwako.
 
Mh. Karibu sana... tunashida ya homosexual kwenye jamii na mashuleni kwa sasa.

Kama wizara mna kauli gani?

Mbili nini tathimini ya mitaala ya elimu ya msingi kwenye nchi yetu mpaka sasa hasa nimejikita kwenye malengo mahususi ni kweli yanafikiwa?

Asante.
Maswali mengine niya Wizara ya Afya sio Maendeleo ya Jamii
 
Maswali mengine niya Wizara ya Afya sio Maendeleo ya Jamii
Fanyeni homework yenu vizuri sio kutupa mpira. Hili linaigusa kwa sehemu kubwa jamii na maadili ni swala linalotishia ustawi wa jamii na maendeleo yao... wizara mnaona hamna cha kusema mpaka wizara ya afya?... huko napo wakisema ni swala la haki ya faragha tulipeleke wizara ya katiba na sheria? Ok nimekuelewa.
 
Maswali mengine niya Wizara ya Afya sio Maendeleo ya Jamii
Avatar Yako haiendani na jibu lako..kuwa kuongezeka Kwa homesexuality mashuleni ni suala la Wizara ya Afya...?! Inawezekana upo hulumo Wizarani lakini hujui majukumu ya Wizara .Kama vipi waachie Wataalamu wajibu!

Homesexuality ni suala mtambuka. Linahusu sekta kadhaa ..hili ni suala la kijamii! Hapo kwenu Kuna Idara ya Ustawi wa Jamii ,ambayo inashughulikia na wellbeing ya binadamu!

Kama Idara hiyo ikipewa nafasi( Waitumie ) Wana jukumu kubwa la kushuhhulikia masuala haya!

Ni bahati mbaya sana ,wahusika aidha, hawaelewi wajibu wao au hawajitambui!

Na majibu Yako wewe ni dalili za hiki nikisemacho!
 
Avatar Yako haiendani na jibu lako..kuwa kuongezeka Kwa homesexuality mashuleni ni suala la Wizara ya Afya...?! Inawezekana upo hulumo Wizarani lakini hujui majukumu ya Wizara .Kama vipi waachie Wataalamu wajibu!
Homesexuality ni suala mtambuka.Linajusu sekta kadhaa ..hili ni suala la kijamii! Hapo kwenu Kuna Idara ya Ustawi wa Jamii ,ambayo inashughulikia na wellbeing ya binadamu!
Kama Idara hiyo ikipewa nafasi( Waitumie ) Wana jukumu kubwa la kushuhhulikia masuala haya!
Ni bahati mbaya sana ,wahusika aidha ,waelewinwajibu wao ,au hawajitambui! Na majibu Yako wewe ni dalili za hiki nikisemacho!
Unalosema ni kweli kabisa
Huyo hana maarifa ya kutosha kuhusu wizara yake.
Amewekwa kujibu tu!
Kama vipi abadilishwe hatumuelewi.

Dr Dorothy jibu maswali wewe ndio unajua uchugu wa wananchi na sio huyo anaefananishq afya na maendeleo ya jamii
 
Maswali mengine niya Wizara ya Afya sio Maendeleo ya Jamii
Homo sexuality iko ndani ya ustawi wa jamii, jinsiaa na maendeleo, ndani ya kundi maalumu.

Wizara ya Afya haihusiki, japo itaingia pale kuhusu hoja za kisayansi, kupitia hormonal imbalances.
 
Sijasoma kila page ..

Nauliza Kesi za wale Makonda WA magari ya shule waliolawiti watoto zimefika wapi??

Why Kesi nyingi za kulawiti watoto zinafutwa?..

Na kuna mtu sikumbuki wapi alikuwa na kesi ya kulawiti watoto wake nae kaachiwa...wizara inasemaje?
 
Ndugu Waziri,

Naomba kufahamu, kwa nini NSSF wameagiza Sisi Wastaafu tunaochukua Pension Benki ya TCB tusikope tena hadi tumalize mikopo tuliyonayo?

Kulikua na " Top up", lakini Sasa wanasema, NSSF wanazuia!!!

Pensheni ndogo, tusaidieni angalau mikopo tafadhali Kiongozi.
 
Mheshimiwa umetoa namba za simu, je ni za kwako binafsi au za ofisi?!
 
Heri ya Pasaka wana JamiiForums,

Mimi ni Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum.

Ninayo furaha kujiunga nanyi katika mtandao huu. Nimekuwepo hapa tangu 2015 kama msomaji zaidi lakini sasa rasmi nitakuwa active member.

Naamini JF itakuwa sehemu nzuri ya kupokea maswali, maoni na mawazo yenu kuhusu namna tunavyoweza kuboresha maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake, na watu wenye makundi maalum nchini Tanzania.

Hivyo, ninawakaribisha nyote kushiriki kwenye majadiliano haya na mimi niko tayari kujibu maswali yenu na kusikiliza maoni yenu na hata kuyafanyia kazi haraka pale inapobidi.

Unaweza kutoa maoni yako kwenye mjadala huu au kupitia ujumbe wa faragha (PM).

Karibuni
Dokta nakupongeza kwa hatua hii adhimu kabisa ya kufungua mlango wa kupokea ushauri mbalimbali ili kuboresha Wizara hii muhimu


Mimi nikushauri kwenye jina muangalie namna ya kurekebisha ama kuboresha tools za wizara kwenye jina. Jina hili Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum kwanza ni refu na linajicontradict. Naomba ufafanuzi wa hizi terminology kwenye jina la Wizara

Maendeleo ya jamii
Hii inamaanisha jamii kwa mlengo upi? Kwa sababu sehemu kubwa ya maendeleo ya jamii imejikita kwenye maendeleo ya wanawake na girl child. Maendeleo ya jamii nadhani ihusishe na ile mikopo ya asilimia 10 yaani isimamiwe na Wizara hii kwani TAMISEMI imeelemewa mno na ajira, ujenzi wa moundombinu ya shule na health facilities na kusimamia utawala wa mikoa, wilaya, kata na mitaa

Jinsia
Mhe. Ukiondoa matamko ya kuwataka wanaume wanaonyanyaswa na wake zao kujitokeza lakini nguvu kibwa omewekwa kwa wanawake. Hata NGO zinazofanyakazi kwenye jamii zimejikita kutatua kero za mwanamke.

Wanawake
Wapo kwenye kila acronomy ya jina la Wizara. Sijaelewa hii segment kama.inatumika kwa malengo ya kisiasa au kundi fulani ndani ya kundi la wanawake.

Makundi Maalumu
Hapa ndipo watu kadhaa wanainyooshea vidole Serikali kuwa inaficha uhalisia wa kuenea kwa antisocial behavior nchini. Unaonaje ikasomea wenye ulemavu? Kuwa mlemavu siyo kosa wala kumuita mtu mlemavu siyo tusi.

Kwa leo yangu ni hayo
 
Karibu Mh. Waziri, nakushukuru kwa kuwepo hapa JF kupata maoni mbalimbali na nikupongeze kwani huenda ndie Waziri wa kwanza wa serikali hii ya Mheshimiwa Mama Samia kujumuika na jamii hii ya wana JF.

Mimi naomba niwasilishe changamoto kuhusu ustawi wa watoto wetu katika jamii zetu. Watoto yatima na wazee wasiojiweza wamekuwa na shida kubwa wanapohitaji misaada ya matibabu ya afya.

Sera na miongozo ya matibabu ya kina mama wajawazito, watoto wadogo na wazee ipo lakini haisimamiwi ipasavyo katika ngazi za chini za huduma za afya kama vile zahanati na vituo vya kutolea huduma za afya.

Watoto, wazee na yatima wanataabika sana na kupelekea kua omba omba. Maafisa Ustawi wa Jamii na wasimamizi wa huduma za afya hawajali kabisa. Wameingiza siasa na matokea yake, utendaji wao umekua hafifu.

Naomba uwepo mfumo wa ufatiliaji wa huduma za afya kwa makundi maalumu ya jamii, na mfumo huu uishirikishe jamii moja kwa moja, yaani viongozi wa kidini, viongozi wa kisiasa na wengineo wapewe nguvu ya kuwasimamia watoa huduma wa msingi katika vituo vya afya na hospitali zetu.

Ahsante.
Huyu sio WA kwanza ...yupo mwamba mwigulu nchemba
 
Wasalaam, Dr. Gwajima,

Hongera kwa majukumu makubwa ufanyayo kwa mustakabali wa maendeleo ya jamii ya kitanzania.

Mimi nina hoja moja juu ya jamii wa watoto au watu wazima wenye mtindio wa ubongo au usonji kama inavyofahamika na wengi.

Mhe.Waziri,kundi hili ni kama vile limetengwa hakuna taasisi chini ya wizara yako inayo deal na watu wa aina hii specifically kutokana na mwanya huo kumeibuka wajasiriamali mbalimbali wanaochampion kutoa awareness pamoja na kuhudumia watu wenye changamoto hizi ili hali hao watu wanakusanya fedha, wanaitisha matamasha wakijidai kuwasaidia hawa ndugu zetu kumbe hizi fedha zinakwenda kwenye matumbo yao. Wizara yako inawajibika vipi kwa watu wa aina hii ya ulemavu?.

Wizara yako inavikagua vipi hizi foundations za kipigaji ambazo hutumia watu wenye huo ugonjwa kama mitaji mfano wa asasi hizo ni Lukiza na Li-tafo.Tena huyo Li-tafo hata huko bungeni anakuja kutembeza bakuli akidai anataka kujenga centre ya watoto wenye usonji kumbe ni uongo mtupu.

Watu wenye hizo changamoto wanaelekezeka na kufundishika, je serikali kupitia wizara yako inayo statistics za idadi yao pamoja na training centers wanapoweza kupata angalau specialized skills au knowledge?.

Asante.
 
Itifaki imezingatiwa.

Ikiwa kama njia za kuwawezesha kina mama zitaendelea kama ilivyo sasa - bila ya kuangalia na kusisitiza tamaduni zilizo njema na kuvumiliana - mnaandaa jamii yenye 'uhasama' baina ya wanawake na wanaume.

Ni jambo lenye kutia hofu kusikia idadi ya wanawake, tena wasomi, wanaotaka talaka ikiongezeka. Mafanikio yakianza kupatikana katika familia, mwanamke anaazisha visa ili wagawane mali na mwanaume. Je ustawi na haki za watoto kupata malezi bora utakuwa juu ya nani? No one care!

Naamini sheria kali na miongozo lukuki si suluhu ya ndoa na jamii imara, ikiwa kama malezi katika familia yamevurugwa. Wazazi wanapaswa kusisitiza kuwafunza na kusimamia mienendo ya vijana wao kabla na baada ya ndoa.
 
Back
Top Bottom