Kuna machinga alikuwa anakaa hapa mtaani .kahama anasema kodi kubwa
 
Walikua wanaweka uchafu tu
Kule Arusha nilipita juzi.Wala hawajui kinachoendelea.Bado wamejazana kila mahali.Mtaa wa Congo (Majengo) ndo kumekucha.Nadhani kwa vile mji wa kitalii, hawahusiki.Ila likiisha hili lifuate la bodaboda.Nao wajipange.Vinginevyo waanze kusoma PGO.
 

Muhimu sana serikali kuhakikisha matajiri, wenye maduka makubwa hawaweki meza zao au kujenga vibanda vyao safi.

Sheria ile ile iliyowatoa wamachinga itumike kwa watu wote bila kujali status zao, upendeleo, rushwa.

Njia za wanaotembea zibaki wazi kwa wanaotembea kwa miguu.
 
Mnaotembea kwa miguu mnasababisha foleni road
 

Mazingira ya biashara, kilimo, exports, kodi, tozo muhimu yawe rafiki kwa wafanyabiashara na wakulima wote wakubwa na wadogo.

Hizi sera zinabidi ziwe strategic pia kuwe na join-up thinking.

Wakati wamachinga wanaondolewa barabarani, lazima kuwe na sera za uhakika, endelevu kuhakikisha taifa halizalishi wamachinga wengine wengi.

Kuongeza tozo kunapunguza ajira/kipato kwa wakala wa miamala, bei za mbolea inaongeza vikwazo kwa wakulima.

Hizi sera inabidi ziende kwa pamoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…