Tupeana updates za kuhama kwa Wamachinga
Mnazalisha majobless.
Huyo mama 2025 mtampa shida sana
Yaani kuwekewa utaratibu wa biashara ni tatizo?!😲

Btw uongozi wa Machinga mkoa wa Dar umeunga mkono zoezi hilo na wenyewe walikwenda pale Karume kusafisha.....na greda waliomba ofisi ya Mkurugenzi.....

FYI : Ofisi za Wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wanatoa maeneo ya kufanyia biashara....hakuna anyimwaye!

UKWELI UTATUWEKA HURU

#Siempre JMT
 
Pamoja na Nia njema kabisa iliyonayo Serikali yetu., wasiwasi wetu ni kuongezeka kwa vibaka mitaani.
Wasiwasi ni akili....

Ila....

Hakuna aliyezuiwa kufanya biashara....

Maeneo yametengwa na maelekezo kutolewa kila mmoja apate eneo la kufanyia biashara....

Btw mazoea tu huwa yana tabu ila mapambano ya RIZIKI HALALI hayakomi na huendelea....
 
Kwahiyo unaona wamachinga ndo vibaka acha dharau. Graduate wangapi wako mtaani na hawajaitwa vibaka.
Pole sana kama nimekukwaza. Sikuwa na dhamira hiyo uliyo ifikiria.

Jana nikiwa natokea ubungo kuja kimara ndani ya daladala, kulikuwa na jamaa (vijana) waliyobomolewa vibanda vyao

Moja ya tahadhari katika maelezo yao ilikuwa juu ya uwezekano wa kuongezeka kwa vitendo vya ukabaji, kwakuwa vijana wengi hawatakuwa na kazi kipindi hiki Serikali ikiwa bado inafanya utaratibu wa maeneo.

Kiufupi ni kuwa tunajijua watanzania, unaweza kupinga lakini ukweli ukabaki nao ndani ya moyo wako.
 
Yaani kuwekewa utaratibu wa biashara ni tatizo?![emoji44]

Btw uongozi wa Machinga mkoa wa Dar umeunga mkono zoezi hilo na wenyewe walikwenda pale Karume kusafisha.....na greda waliomba ofisi ya Mkurugenzi.....

FYI : Ofisi za Wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wanatoa maeneo ya kufanyia biashara....hakuna anyimwaye!

UKWELI UTATUWEKA HURU

#Siempre JMT
Hata wasingeunga mkono walipaswa kutekeleza agizo la serikali, sidhani kama viongozi wana nia mbaya na machinga la hasha!

Kinachofanywa ni kuweka mazingira ya miji katika utaratibu wake kwa mujibu wa miongozo ya mipango miji japo bado kasoro zipo nyingi.

Miji ilionekana kuwa michafu muda wote kila mahali, fujo tupu na kuzalisha vibaka, piga picha pale viwanja vya mnazi mmoja yaani ilifikia hatua kupishana ilikuwa shida ni mwendo wa kupigana vikumbo.

Sehemu nyingi zilianza kuwa makazi ya mateja. Mara nyingi unakutana nao wanazurura na kicheni kimoja au betri mbovu kumbe anakula timing ukikosea tu imekula kwako.

Natoa hongera kwa viongozi wetu zoezi hili litapunguza na kuondoa kero hii.
 
KUMEKUCHA, Nasikia dar imefanyiwa usafi ndani ya usiku mmoja na hawa vijana, watu wameamka asubuhi hawaamini wanachokiona ,sehemu ambayo ilikua haipitiki saivi unapita bila kugusana.

vibanda vyote vimevunjwa hivi vya service road sasa ufanyike usafi wa kwenda jiji liwe safi zaidi

kumbe inawezekana aisee khaa Suma jkt sio wa mchezo mchezo, waendelee kupewa tenda hawa vijana
Picha
 
Mataga utaweweseka sana.
Wanabomoa vibanda vyenu wanaweka vibanda vyao. Mtetezi wenu ndio kashaondoka pambaneni na Hali zenu. Wajanja wameangalia wamejua mnapiga hela maeneo fulani fulani. Wametafuta njia ya kuingia hapo na ndio hio kwamba vibanda vyenu vichafu havifai kuwa hapo ILA vibanda vyao visafi ndio vinastahili! Wewe mlalahoi kibanda chako peleka kijijini kwenu huku tunataka vibanda vya akini tipisi, fishifishi na wajanja wengine wa mjini
 
Mataga pia mfuate sheria bila shurti
Pumzika kwa amani Jemedari chuma JPM, mzalendo na kiongozi madhubuti.

Mabeberu na Mafisi yamekuondoa mapema sana ingali taifa linahitaji uchapa-kazi wako.

Kila siku naikumbuka ile sauti yako yenye mngurumo wa radi. Kiongozi mwenye kinywa kilichojaa mamlaka na AMRI.

You have gone too soon John!
 
Muhimu waelekeze juhudi kubwa kusafisha masoko kama Tandika, Tandale,ilala Boma, Mwenge, Temeke fukwe zote kama magogoni, kawe, oysterbay.

Masoko inabidi yapangwe upya na yawe na miundombinu ya kutosha ya vyoo na visafi, sehemu za kuweka uchafu, (Dustbins) miundombinu ya kuchukua maji taka na maji ya mvua, meza, nafasi za kutosha kwenye njia za kupita watembea miguu ndani ya soko, roof, sakafu za cement / zege, parking za kutosha, na taa/mwanga wa kutosha etc.

Muhimu sana wahakikishe wafanyabiashara wote wanaendelea kupata sehemu zao za kuuza zilizo safi, salama kwa kila mtu anayetembelea soko.

Wawekeze pia kuwa na bustani njingi mjini, na kupanda miti, majani, maua katikati ya barabara kubwa na pembezoni ya barabara zote.
 
Huo ndio ukweriii ndugu zangu.
Hata huyo mnaodai ni mtetezi wenu alikuwa akiwatumia tu kwa maslahi yake sio kwamba alikuwa akiwapenda kutoka moyoni. Aliamua kuwakumbatia nyie ili kubalance lakini baadae angewaondoa tu.
 
Back
Top Bottom