Hata wasingeunga mkono walipaswa kutekeleza agizo la serikali, sidhani kama viongozi wana nia mbaya na machinga la hasha!
Kinachofanywa ni kuweka mazingira ya miji katika utaratibu wake kwa mujibu wa miongozo ya mipango miji japo bado kasoro zipo nyingi.
Miji ilionekana kuwa michafu muda wote kila mahali, fujo tupu na kuzalisha vibaka, piga picha pale viwanja vya mnazi mmoja yaani ilifikia hatua kupishana ilikuwa shida ni mwendo wa kupigana vikumbo.
Sehemu nyingi zilianza kuwa makazi ya mateja. Mara nyingi unakutana nao wanazurura na kicheni kimoja au betri mbovu kumbe anakula timing ukikosea tu imekula kwako.
Natoa hongera kwa viongozi wetu zoezi hili litapunguza na kuondoa kero hii.