Black Walker
Senior Member
- Oct 8, 2018
- 119
- 254
Point yako ina utapiamlo, na wewe unaonekana ni wale wa kuvimba mabega bila kitu, miji haina wenyewe ni suala la muda tu.Mshike adabu !Mmekuja mjini mnajifnya wajanja kuliko wenye miji, rudini kwenu mkalime, si mmetelekeza mashamba ya miwa, kahawa,mawese,ndizi mkayafufue acheni miji ya watu ipendeze.
Kinachotupa tofauti ni kipato ila huwa ni suala la muda tu.
Siwaungi mkono machinga kuendelea kukaa kiholela holela hata kidogo kama ambavyo wewe unaonekana kukerwa nao kutokana na kutokufuata taratibu za mipango miji.
Ulichokosea ni kuonyesha ubaguzi kama ukiwa na hoja jitahidi kuifikisha kwenye jamii bila mwelekeo wa kibaguzi. Tukiendelea kukumbatia kauli za kibaguzi kama zako tutakuwa na kizazi cha chuki mwanzo mwisho.
Kila mtu wa chini atakuwa anapambana kujikwamua siku akipata ndo utaona watu kama akina Makonda au Sabaya.
Kila mtanzania ana haki ya kuishi mahali popote anapoona inafaa kwa "mujibu wa sheria."
Waelimishe wafuate utaratibu usiwabague.