Turudi kwenye kikao cha chama kati ya Waheshimiwa mawaziri na Mh. Makonda ni nani anakaa viti vya mbele kuwahutubia wenziwe?

Turudi kwenye kikao cha chama kati ya Waheshimiwa mawaziri na Mh. Makonda ni nani anakaa viti vya mbele kuwahutubia wenziwe?

Haupo objective, wewe unaongelea hisia zako sasa. Swali ni kuwa mawaziri wote wanaingia kwenye vikao vyote vya chama? Na wakiingia wanaingia kama nani mawaziri au wanachama ? Na kama wakiingia kama wanachama ukiangalia structure wa CCM kipi ni kipi na nani ni nani?
Siongelei hisia, Sina hisia kabisa na ccm,mawaziri watakaa kwenye bench maana watavaa kofia za ujumbe, main table itakuwa na chairperson, vice chairman, SG,katibu mwenezi, viongozi wakuu wa chama watakua High table maana ndio wenye serikali
 
..tuchukue Mfano wa Makamu Mwenyekiti vs Makamu wa Rais.

..kama ni kikao cha chama basi wakuu wa chama wako juu.

..Makamu wa Mwenyekiti wa chama anakuwa mkubwa kuliko Makamu wa Raisi.

..kwenye vikao au shughuli za serikali wakuu wa serikali wako juu.

..ktk shughuli za serikali Makamu wa Raisi ni mkubwa kuliko Makamu Mwenyekiti wa chama.
 
Hapa tunapoteza muda tuu kulishana upepo….! Chama kina nguvu kuliko waziri na viongozi wa chama hasa katibu mwenezo anayo nguvu kuzidi waziri kwa sababu anakwenda moja kwa moja kwa wananchi na bahati mbaya katibu mwenezi ana msaidia waziri kupata kura…
Hivyo Waziri hata akijitutumua vipi kamwe asijidanganye!
 
..tuchukue Mfano wa Makamu Mwenyekiti vs Makamu wa Rais.

..kama ni kikao cha chama basi wakuu wa chama wako juu.

..Makamu wa Mwenyekiti wa chama anakuwa mkubwa kuliko Makamu wa Raisi.

..kwenye vikao au shughuli za serikali wakuu wa serikali wako juu.

..ktk shughuli za serikali Makamu wa Raisi ni mkubwa kuliko Makamu Mwenyekiti wa chama.
Nikupe ufafanuzi mdogo ndugu yangu kama utanielewa. Ni hivi Chama kinachotawala hasahasa kwenye nchi za mlengwa wa kati na kushoto kinakuwa ndiyo SHAREHOLDER wa nchi na serikali inakuwa Management ya nchi.

Kwa maana hiyo, hata siku moja haitatokea makamu wa rais akiwa anatekeleza majukum yake ya makamu wa rais akakielekeza chama au hata kukishauri hakiwezi kutokea kitu kama hicho.

Makamu wa rais akiwa anatekeleza majukum yake hawez kumwelekezi nini cha kufanya kichama kiongozi yeyote wa CCM hata mwenyekiti wa shina wa CCM.
Lakini kiongozi wa ngazi yoyote ya CCM anaweze kutoa maelekezo kwa kiongozi yeyote wa serikali.

Hakuna kikao chochote cha Kiserikali kikiwa kinaongozwa na kiongozi yeyote ndani ya serikali kinaweza kuhoji utendaji wa chama lakin Kikao cha chama kinaweza kuhoji utendaji na mwenendo wa serikali wakati wowote na kuomba kipatiwe majibu.

Kwa ufupi sana
 
Hii picha itoshe kukupa majibu kuwa uvunjaji wa taratibu ndani ya CCM haujaanza jana wala leo.

Huyu zero brain anawafokea hadi watumishi wa umma walioingia kazini kwa merit wakati yeye huo uongozi kapata kwa kujuana na maslahi.
download (1).jpeg
 
Tokea uzaliwe ulishawahi kuona au kusikia mtu akiingia kwenye kikao cha ccm kwa kofia ya uwaziri?
Mimi niliwahi sikia mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro aliingia akitokea ACT(ccm b)ila baadae ikamlazimu ahamie CCM A
 
Nchhiii ukitumwa na Raisi a.k.a Amiri Jeshi Mkuu,wewe ni boss.

Huyo kijana katumwa ,ni boss wenu mpokeèni.
Katiba ina muongozo lkn kwa nchi hii sio kweli ,upumbavu mwingi.
 
Wapi kwenye katiba psmeandikwa chama kitakuwa juu ya Serikali?
Acha kujifanya chizi wakati uko na akili timamu, wapi pameandikwa kuwa kutakuwa na mhimili iliyojichimbia chini zaidi lakini si ulikuwepo kipindi cha yule muovu. Kuamini kuwa tunaongozwa na katiba ni ujinga mkuu, Rais anaweza ikanyaga itakavyo kwani wengi wa kuilinda ni wateule wake
 
TAIFA halina umeme n sukari.mnawaza nani akae mbele ya wengine.takataka tu
Swala la umeme ni janga na hakuna cha kufanya wankwambi subiri mwezi wa tatu swala la kukatika umeme litakua historia.yaan unamwmbia mgonjwa we kufa tu kwasasa matibabu yatapatikana mwezi wa tatu.poor CCM
 
Makonda ni msemaji wa chama nje ya chama siyi ndani.
Kama serikali ilivyo na msemaji, anapokea maelekezo ya nini aje atuambie. Aache kujitwika madataka yasiyo yake, ajifunze kazi yake.
Yeye anapaswa kuzungumza na vyombo vya habari, kuhusu mambo ya chama tu, siyo ya serikali.
Ni mtoa taarifa, tena anazopewa na vikao vya ndani siyo kubuni nini cha kusema.
 
Haupo objective, wewe unaongelea hisia zako sasa. Swali ni kuwa mawaziri wote wanaingia kwenye vikao vyote vya chama? Na wakiingia wanaingia kama nani mawaziri au wanachama ? Na kama wakiingia kama wanachama ukiangalia structure wa CCM kipi ni kipi na nani ni nani?
Nachojua mimi wabunge wote wa CCM wanaingia kwenye kikao kinachoitwa MKUTANO MKUU WA CCM TAIFA.

Kikao hicho ndio cha mwisho kupitisha viongozi wa chama kitaifa pia wagombea nafasi za kiserikali kama Rais kwa kupiga kura.

Kwenye hicho kikao hakuna cheo cha uwaziri bali wote hao ni wajumbe.

Katibu mwenezi hakai mbele anakaa kwenye viti vya sekretarieti. Anaingia kwa cheo chake.
 
Tulikua tunabishana hapa mtaani kuhusu mgawanyo wa madaraka ndani ya chama na serikali.

Mimi bado nilikua nimeshikiria kwamba viongozi wa chama wakiamua wanaweza kuwa na nguvu kuliko mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya.

Nimerudi hapa jukwaani nataka kupata majibu juu ya swali langu hili:

Turudi kwenye vikao vya chama kati ya Waheshimiwa mawaziri na Mh. Makonda ni nani anakaa viti vya mbele kuwahutubia wenziwe?
Kikao pekee cha chama ambacho kinamkutanisha Mwenezi na Mawaziri wote ni Mkutano Mkuu wa CCM ambapo Mawaziri huingia kwa nafasi zao za Ubunge.Katika kikao hicho Meza Kuu wanakuwepo Mwenyekiti,Makamu Mwenyekiti wote wawili (Bara na Zanzibar),na Katibu Mkuu.Wajumbe wengine wote wanakuwa na hadhi sawa.
 
Nachojua mimi wabunge wote wa CCM wanaingia kwenye kikao kinachoitwa MKUTANO MKUU WA CCM TAIFA.

Kikao hicho ndio cha mwisho kupitisha viongozi wa chama kitaifa pia wagombea nafasi za kiserikali kama Rais kwa kupiga kura.

Kwenye hicho kikao hakuna cheo cha uwaziri bali wote hao ni wajumbe.

Katibu mwenezi hakai mbele anakaa kwenye viti vya sekretarieti. Anaingia kwa cheo chake.
Kwa maana hiyo hicho kinachoitwa waziri halipo ndani ya vikao vya ccm automatically
 
Siongelei hisia, Sina hisia kabisa na ccm,mawaziri watakaa kwenye bench maana watavaa kofia za ujumbe, main table itakuwa na chairperson, vice chairman, SG,katibu mwenezi, viongozi wakuu wa chama watakua High table maana ndio wenye serikali
Hapana...Itifaki ya vikao vya Chama haiko hivyo..Meza Kuu ni
1.Mwenyekiti
2.Makamu wa Mwenyekiti
3.Katibu Mkuu
Wengine wote kukaa kama wajumbe wenye hadhi sawa akiwemo huyo Mwenezi.
 
Mkuu serikali si ndio chama na chama si ndio serikali! Mfumo mzima ni mbovu
Ndio maana unaona kipepe yupo kila mahali.
Katiba ndio shida
Hatujaweza kutofautisha chama na serikali
Wapi imeandikwa Serikali ndo chama?
 
Back
Top Bottom