Pre GE2025 Tuseme bila unafiki: Kikwete ni tatizo kwa sasa nchini kuliko wakati wowote

Pre GE2025 Tuseme bila unafiki: Kikwete ni tatizo kwa sasa nchini kuliko wakati wowote

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwa hiyo kujiunga jf siku nyingi ndo kipimo cha kujua maarifa ya mtu?

Nimekuuliza kuna kiongozi iliye asisi mambo ya hovyo ndani nchi hii kama jiwe?
Huyo Rostam si alikaribishwa ikulu na jiwe zaidi ya mara tatu?
JPM hakuhitaji msaada wa machawa kuongoza nchi bali alipendwa na watanzania wengi, unamkumbuka Waziri Kangi aliyempamba jukwaani baada ya kumaliza hotuba yake akamtumbua pale pale.., zilikuwa zama za watu kukimbilia Tv kila ilipofika saa 2 usiku kusikiliza JPM amesema nini ? mpaka leo mamilioni ya Video clip za hotuba zake zipo random mitandaoni iwe You tube,Insta,Fb ama Tiktok zikiwa na mamilioni ya viewers kukiko rais yoyote aliyetawala nchi hii..
 
The man is everywhere but natoa aren't na tahathari hakuna marefu yasiyo na ncha.

Minyororo yako uliyoifunga inaelekea mwisho tubu na omba msamaa kwa Watanzania

Umewakosea Sana Watanzania haiwezekani kabisa kila kitu unahusishwa wewe!!

Why unatumia nguvu nyingi kuhujumu umma kwa maslahi yako binafsi?

Wajukuu wetu warithi nini Kama kila kitu kinauzwa na wewe upo kimya unapata manufaa gani na maslahi gani?.

Rais Mustaafu pekee aliyebaki badala ukemee uhuni na wahujumu uchumi wa nchi wewe kutwa upo na Rais tu kwenye kila Jambo hata Kama anavuruga nchi?

Jk jifunze kwa mwenzako Uhuru Kenyatta pamoja na kwamba ni bosi ni tajiri kweli ila bado serikali ya ruto anaikosoa waziwazi bila kupindisha maneno

Jk unakwama wapi? Nyerere alikemea Sana utawala wa Mwinyi Mkapa why wewe kimya ??

Ulimkosoa Magufuli pale maslahi yako yalivyoguswa lakini sasahivi nchi inaanguka upo tu unashangaa mpaka watu waanze kugawana mbao?

Umeshindwa kusoma upepo kwamba wananchi wa nchi hii hawatamchagua kabisa Samia kwanini ujamshauri apumzike?

Jk wewe ni tatizo kwa Sasa pengine kuliko hata Samia mwenyewe!!

Na mtaanguka wote!!
JK na huyo bibi wana mahusiano ya simu nyingi sana, ya "kibinafsi", naeleweka, na ya kiuchumi, kifisadi
 
Uzuri kwenye Nchi hii hakuna mtu anafahamu siasa, fitina na majungu kama Kikwete. Kama aliwai kumtosa swaiba wa ukweli Lowsssa itakuwa Samia. Twende mdogo mdogo. Ata yeye anafahamu baada yake hakuna msitahafu atasema Asikilizewe kama yeye. Tulienia atawaacha sehemu nzuri mnayo itaka nyinyi wala msiwe na shaka. Kikwete ni mtu ambaye anaweza kuona Ccm hakuna kada aliyepikwa akaiva akahamua nchi ichukuliwe na wapinzani. Binafsi bado namuamini Kikwete.
utasubiri sana !
La kuvunda halina ubani !
Ngoja Tusubiri tuone !
 
Unataka aendelee kufanya kazi ya Urais?

Hujui kuwa Jiwe alitaka kumtengenezea kesi feki ya kutaka kupindua serikali ili ammalize?, Nenda kasome kitabu cha Kabendera utaikuta hiyo!
Sasa ndio aunge mkono ujinga wa kumpitisha huyu Mama agombee tena uraisi?
 
Hazina yetu pekee iliyo baki nchini ni Rais Mstaafu JK, Watanzania wote wenye vyama na wasio na vyama tunamuombea Mungu azidi kumpa maisha marefu yenye afya na maarifa tele.
Taifa linamtegemea na Afrika pia.

Watesi wa nchi hii ni nyinyi wenyewe msio kuwa na akili, kikwete kaingia madarakani kakuta nchi ina miaka 45 imepata uhuru na bado akaikuta inanuka umasikini kila sehemu, akatawala miaka 10 akaondoka akaiacha nchi inanuka umasikini mpaka ana miaka 10 ameondoka madakani nchi bado inanuka umasikini.
Sema uwezavyo,tuite majina utakayo ila mwisho wa yote utafika. Na atawajibika Kwa yote aliyo na anayotenda.
 
Mkuu kwa ungwana ungeanza kutaja kama nilivyo kuomba halafu ndio unitake nikutajie.

Ila kwa kukufundisha ungwana nakutajia kama ifuatavyo:

Baadhi ya mawaziri waliohudumu kwenye serikali ya Ali Hassan Mwinyi (1985–1995) na baadaye wakateuliwa tena kwenye serikali ya Benjamin Mkapa (1995–2005) ni hawa:

1. Mheshimiwa Jakaya Kikwete

  • Serikali ya Mwinyi: Waziri wa Maji, Nishati na Madini (1990–1995).
  • Serikali ya Mkapa: Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (1995–2005).

2. Marehemu Edward Lowassa

  • Serikali ya Mwinyi: Naibu Waziri wa Maji, Nishati na Madini (1990–1995).
  • Serikali ya Mkapa: Waziri wa Nishati na Madini (2000–2005).

3. Hayati John Pombe Magufuli

  • Serikali ya Mwinyi: Naibu Waziri wa Ujenzi (1995).
  • Serikali ya Mkapa: Waziri wa Ujenzi (2000–2005).

4. Marehemu Joseph Mungai

  • Serikali ya Mwinyi: Waziri wa Elimu na Utamaduni.
  • Serikali ya Mkapa: Waziri wa Kilimo na Chakula.

5. Mheshimiwa Anna Abdallah

  • Serikali ya Mwinyi: Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.
  • Serikali ya Mkapa: Waziri wa Afya (2000–2005).

6. Marehemu Basil Mramba

  • Serikali ya Mwinyi: Naibu Waziri wa Fedha.
  • Serikali ya Mkapa: Waziri wa Fedha (2000–2005).

7. Marehemu Iddi Simba

  • Serikali ya Mwinyi: Waziri wa Viwanda na Biashara.
  • Serikali ya Mkapa: Waziri wa Viwanda na Biashara (1995–2000).
Umempa dozi kubwa kuliko uzito wake.
 
Samia hamuitaji mtu yeyote kubaki madarakani nguvu yake ya urais aliyo nayo inamtosha kufanya chochote anacho jisikia na asiwepo mtu atakayebweka ndani nchi hii.
Nguvu ya kimamlaka aliyo nayo Samia kwa sasa anaweza kuitumia kumpoteza hata huyo Kikwete.
😂😂😂😂
 
Mkuu usisahau pia Kuwa Rais fisadi hudhibiti mafisadi ili abaki yeye mwenyewe kwenye kufisidi nchi!!! Zingatia 1.5T ya 2017.
1.5T 2017 na sasa tupo 2025 wahuni wanashindana kufisadi na sio kudhibiti ufisadi....

Unajua kuna tirioni ngapi kutoka 2oo5 hadi 2925 zimedhibitiwa ili kumfanya rais fisadi afisidi nchi?

Najua hujui ila nikuambie tu rais fisadi hawezi kudhibiti mafisadi...

Nyongeza ni hii "wachawi walishakufa".
 
Umempa dozi kubwa kuliko uzito wake.
Ametoa ufafanuzi huu kupitia usaidizi wa AI hata hivyo Magu hakuwahi kuhudumu katika serikali ya Mwinyi.. ni meeneo mengi imekosewa bora angetumia Analyisis anayoijua yeye..
 
Nguvu ya kimamlaka aliyo nayo Samia kwa sasa anaweza kuitumia kumpoteza hata huyo Kikwete.
Bibie mwenye nyege zake nchini ampoteze mwanaume rijali anayemfanya atabasamu?

Hebu tafuta uongo mwingine wa kujifurahisha
 
Back
Top Bottom