Uchaguzi 2020 Tusemezane: Uhalisia wa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2020

kamwe mifumo ya kisiasa tulorithishwa na mabeberu haiendani na siasa japo tunalazimisha iwe ndo mifumo yetu rasmi, kuna haja ya kuunda mifumo ya kisiasa inayoendana nasi ili tuweze kupiga hatua mbele.
 
Jiandaeni kisaikolojia maana lissu ndiye ataapishwa baada ya October.

Wananchi wa Tanzania tegemeo lao ni mh Lissu.

Hutaki rudi kwenu Burundi.
Si unajua kiitikio chenu cha tumeibiwa×6
 
Nimependa Sana ulivyomuelezea huyu jamaa,inaonesha Ana uelewa mdogo Sana wa mambo
Asante Sana kiongozi.
Una hekima kubwa Sana.
 
mkuu nyani, nakuomba uondoe aya ya mwisho kabisa maana hakuna timamu anayeweza kubishana na wewe katika haya uliyoandika!


nadhani kinachotafutwa ni idadi ya wabunge plus ruzuku, maana wabunge kushinda ni rahisi sana hasa mkikomaa!


shida yetu kelele za hitaji la tume huru huwa linaanza mwaka mmoja kabla ya uchaguzi, kitu ambacho kimsingi haisadii!
 
Kuna siku unachangia kama mtu kabisa. Wakati mwingine unajitoaga ufahamu..., Kwa leo umeongea Jambo la maana.

Kwa mtazamo wangu, Sisi wananchi tuna mahitaji yetu mengi saana, siyo tu kuitoa CCM madarakani bhaaaas, yapo mengi Sana. Kwa hiyo basic need siyo kuitoa CCM madarakani Tu.

Kati ya vitu vya hatari tangu dunia iumbwe ni power, yaan mtu akishakuwa nayo hiyo anafanya kila awezalo isitoke kwake, Kama watu walikuwa wanaua watoto wote wa kiume kuzaliwa kisa Tu kaambiwa kuna mfalme atazaliwa, enzi hizo, itakuwa leo Kwa urais? Kwa maana hiyo, sitegemei kutawahi kuwa na mazingira rahisi and fair ya mtu/chama kujishindia Tu dola kirahisi.

Sasa basi, lazima tushiriki uchaguzi, tuambizane Sera, tukosoane kila mmoja anapokesea, tukosane kosane kutoana madarakani...., Chama kilichopo madarakani kiendelee kujirekebisha wananchi wakipende, kikijisahau watu watakuja kuchagua upinzani 80% Kwa 20% itakuwa ngumu kuchakachua.

Note: kuna maeneo ya ubunge na udiwani, upinzani wanatangazwa na the same system, si Kwa kupenda Bali inawabidi kufanya hivyo.

#HapaKaziTu
#NiYeye
 
Nimependa Sana ulivyomuelezea huyu jamaa,inaonesha Ana uelewa mdogo Sana wa mambo
Asante Sana kiongozi.
Una hekima kubwa Sana.
Kwa ujumla WaTz ni wanafki. Na Nyani Ngabu anauwakilisha unafki huo. Kasoro anaziona kwenye katiba na tume , halafu pa kurushia taka ni kwa wapinzani !!! Ajabu na kweli
 
Kwa sasa busara ni kushiriki. Na kisha kukusanya nguvu ya wananchi kuhakikisha Tume ziziso huru zinalazimishwa kuwa huru. Na wakati wote wa kampeni, wagombea wa vyama vya upinzani wapige kampeni kubwa ya kuwaandaa watu katika kuilazimisha Tume isiyo huru iwe huru, katiba inayolinda chama tawala iwasaliti watawala.

Wajati muda mzuri wa kuwaandaa watu kwa hilo kama wakati wa kipindi cha kampeni.

Tunataka CCM wajutie kwa nini waliamua kuingia kwenye uchaguzi kukiwa na Tume isiyiaminika, na katiba mbaya.

Wapinzani siyo wajinga. CCM watajutia ujinga wao wa kuamini watu ni wajinga wakati wote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kususia uchaguzi inaweza kuwa wazo baya kuliko yote,,ili upate tume huru au hata katiba mpya unahitaji jukwaa la "kupambania" huwezi kudai mambo hayo ukiwa sebuleni kwako.Isitoshe "umma" haujaiva kiasi cha kutosha "kuingia barabararani" kudai haki za kijamii.Kwahiyo nilazima kukubali hali hii iendelee kwa mda hadi hapo "umma" utakapokuwa tayari kubadili hali ya mambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…