Tushaurini sisi wateja wa Halotel tuhamie mtandao gani?

Tushaurini sisi wateja wa Halotel tuhamie mtandao gani?

Ninatumia line ya chuo, Sasa nilipigiwa simu na texts kutoka halo kwamba niende kubadilisha wanipe line ya 4G. yenye data Gb4. Sijafanya hivyo kwa makusudi kuhofia kupoteza line ya chuo yenye bundle nafuu.
Hata ukibadili line inabaki ya chuo ila mbona line ya chuo halotel haina cha zaidi.
 
TTCL NAKO MAMBO NI[emoji3063][emoji3063][emoji3063][emoji3063]
Screenshot_20211019-133702_Phone.jpg
 
Tupambane na halotel yetu si tuliipenda wenyewe ama!!
 
Vodacom kwa 1000 unapata mb 350

Kwahiyo bado halotel wana nafuu
 
Kazi iendelee mko bize kutukana watu mitandaoni
 
Nina hasira hapaaa.
Yaani mega bando ya gb 1 kwa wiki wameweka mb 600.mimi kila siku nanunua bando la 1,000 .kumiliki smart phone ni kujitia umasikini[emoji2959][emoji2959][emoji2959][emoji2959][emoji2959]
 
Hapa niripo nina kazi ya zima simu,,,mwishoe litakufa *****. Halotel ❌ tigo❌
 
Jamani nimekandika bando via halopesa nashangaa napata bando njiwa napitia hapa viwango inasikitisha jamani lile bando pendwa la usiku la 1500 liililokuwaga 10gb likashuka hadi 5gb tukavumilia kwa sasa ni mb 1160

Nimenyoosha mikono, iam done
Daah..nimeumia sana mkuu
 
Back
Top Bottom