Tusipochukua maamuzi magumu Taifa letu la Tanganyika litapotea kabisa

Hiyo ndugu MALCOM LUMUMBA imeniacha solemba...

Ndo kusema kuwa Tundu Lissu anayajua mengi ya Humphrey Polepole kuliko anavyijijua yeye Polepole, au siyo..?

Haya bhana. Hopefully kuwa, Tundu Lissu Jumatatu tarehe 8/9/2025 mahakama itamrudishia haki ya uhuru wake ili tuione hii battle...
 
Hata wewe bwana MALCOM LUMUMBA ukipewa nafasi serikalini sifikirii Kama unaweza kuikataa .

Tanzania hakuna wanaharakati na hawajawaiga kuwepo hao akina Maria , kimambi n.k wote hao wapo kazini for thdir own interests .
That's true...

Aliyekataa nafasi serikalini Tanzania hii ni mmoja tu, Tundu Lissu..

Hawa wengine sijui. Hata MALCOM LUMUMBA sijui...

Huyu Humphrey Polepole na mwenzake Prof. Palamagamba Kabudi walikuwa vocal na waliosimama ktk mstari...

Walipoingizwa serikalini tu, nao wakawa wanamtandao na wakawa mstari wa mbele kuiua Tanganyika...

Leo Humphrey Polepole ndio huyo anarudi alikotoka lakini wakiwa wameshafanya uharibifu mkubwa...

Hata hivyo, ingalau huyu kakumbuka shuka usiku wa manane...
 
Hili sisi Watanganyika hatuna tatizo, tuko tayari hata leo....

Lakini kwa wenzetu Wazanzibari, hawajawahi kuwa tayari...

Kidogo wako tayari kwenye hili unalolikataa, Serikali tatu...
 
Hongera sana, una akili sana za kuweza kung'amua mambo mazito.​
Lazima wagombanishwe hawa ukiangalia humu ndani kuna uzi watu wanalazimisha polepole ataje waliomshambulia Lissu wakati polepole alishaomba msamaha maana ya msamaha nini? Na Lissu ni mtu wa kujaa Upepo na kulipuka akitoka Lissu anatakiwa kushukuru watu wote wanapambania atoke hata wakina polepole bila kujali mambo ya nyuma. Je ilo litawezekana. Polepole ni CCM kwanza mambo ya kupigania mifumo kua huru hataki hapo ndo ungomvi wake utaanzia na Lissu. Polepole yeye anaamini bila CCM hakuna Tanzania kitu ambacho sio kweli mkiwa na mifumo iliyo nyooka Rais hata akitoka vyama vingine still mifumo itamsimamia
 
Hivi kilichomtuma Raisi Magufuli na watu wake kumshambulia Lissu kilikuwa ni MTANDAO au hulka binafsi ??? Vipi kuhusu Ben Saanane, do you think he deserved that ???
Hapa conflicting info. Sijui tushike la nani na tuache la nani!
 
Saa tatu asubuhi mkuu.

Maana yake ipate muda wa kutosha kabisa kujadiliwa faida na hasara zake, bila kusahau sababu za msingi za kuwepo kwake licha ya kumulikwa huko zamani.

Sheria ipi inakuwa imejadiliwa kirefu:

Iliyopita saa 3 asubuhi au iliyopita saa 11 jioni?

Ndo maana aliyetoa hoja hii kaingia mitini.

Kasema sheria mbovu, ilipitishwa saa kumi na moji jioni.

Ilipaswa ipitishwe saa ngapi, wakeshe nayo usiku kucha ?

Bunge la bongo huwa linakesha na jambo ?

Kwa uchungu na uzalendo gani waliokuwa nao wabunge wa hisani wa CCM ?
 

..MIGA ni Multilateral Investment Guarantee Agency.

..Ni chombo kinachowalinda wawekezaji dhidi ya risk / hatari kama utaifishaji wa mali zao na serikali za nchi walipowekeza.

..Tanzania ni mwanachama wa MIGA.

..Uanachama wa Tanzania MIGA ni ahadi / guarantee kwa jumuiya ya kimataifa kwamba mali za wawekezaji zitakuwa salama hapa nchini.

..Kwa hiyo mpaka hapo utaona kwamba Tundu Lissu alikuwa sahihi aliposema kwamba hatua alizochukua Rais Magufuli zilikuwa zinaiweka nchi katika hatari ya kushtakiwa MIGA.

..Accacia walikuwa na uwezo wa kwenda MIGA kudai walipwe. Hatua ambayo ingefuata ni MIGA kujaribu hatua za usuluhishi. Kama usuluhishi ungeshindikana MIGA wangewalipa Accacia, halafu wao wangeanza kushughulika na Tanzania.

..Mgogoro wa Jpm na Accacia haukufika MIGA kwasababu kulikuwa na negotiations.

..Kama Jpm asingelainika ndio mgogoro huo ungekwenda MIGA.

..Mimi naamini kusema Tundu Lissu alidanganya ni kutokumtendea haki, na kukwepa kujadili kisomi hoja yake.

Cc Nguruvi3
 
Acasia na Barrick ni mtu huyo huyo.


..Magufuli na Kabudi waliwachota akili watu wengi kwa kuwadanganya kuhusu uhalisi baina ya Accacia na Barrick.

..Kifupi ni kwamba Barrick aliuza hisa zake chake, na kubadilisha jina la kampuni kuwa Accacia.
 

..Magufuli alimlaghai au kumchota akili Polepole.

..Polepole aliamini anamtumikia mtu mwema, muadilifu, na mzalendo, wakati alikuwa akitetea jitu fisadi na liuaji.

..Magufuli kabla hajafa aliunda urafiki na Rostam, na akamrudisha Lowassa ndani ya Ccm.

..Kwa kifupi Magufuli na genge lake walikuwa wameshaseti mirija ya kuinyonya nchi kwa kushirikiana na Rostam. Tatizo ni kwamba MUNGU naye alikuwa na mipango yake.

..Polepole katika utawala wa Magufuli alikuwa sawa na mshika mapembe ya ng'ombe huku wenzake wakikamua na kufaidi maziwa.
 
Huyu malcom anajifanya jasusi uchwara mwenye nia njema ya "kuikomboa" Tanganyika lakini nimegundua ana malengo fiche ambayo yako mbali sana na kuikomboa Tanganyika.

Hili ni boksi. Garasa.
Sawa Mchambuzi Bichwa Jasusi mbobezi from KGB
 
Pointi kubwa kwa sasa ni namba 2 hapo juu.

Hata kwa katiba hii, wananchi wangejitambua hakika mambo yangekuwa tofauti.

Katiba ya JMT: Wananchi ndio msingi wa mamlaka yote.

Hilo unalielewaje mkuu?
Hapana! Point kubwa haiwezi kuwa ya kuwapa Wananchi nguvu ya BUNGE
Point kubwa ni kutengeneza Katiba itakayowapa Wananchi nguvu za BUNGE
 
Kuhusu Maria Sarungi huo ni uongo
 
Kwa mtazamo wangu Magufuli alimuamini sana Bahiru A Kakurwa. Kama utakumbuka, kazi ya kwanza ya Bashiru ilikuwa kurudisha vigogo ili kuunganisha Chama. Ni wakati ule alipokumbana na akina Makamba baada ya mwamnaharakati huru kuwananga.

Polepole alimwangalia Magufuli ulivyoeleza (mzalendo) na kufumbia macho ukatili, mauaji na ufisadi
Kwa mantiki, hutamsikia akizungumzia mauaji , ukatili kwa Wafanyabiashara, pesa za Bargaining kinyume na sheria. Sa100 alisema pesa zimepekwa China etc na zile Bilioni 70 zilizopelekwa Mwanza hazijulikani zilikuwa za nini.

Ili repentance iwe haswa! Polepole anatakiwa aeleze yote. That being said kuna 'kamchango' anakokatoa hasa kwa wale waliogoma kuelewa, inasaidia ! Wengi hawakujua hili dudu lililoundwa 1977 lina mauza uza gani. Tunajua mengi kupitia kwake, na hiyo ina encourage wengine ! huo nao ni mwendo mzuri
 
Mkuu kwa yale madudu katika mikataba ya madini, pamoja na udanganyifu mkubwa kuhusu mikataba hiyo, huoni kwamba hatua kali alizochukua JPM zilikuwa na uhalali - LICHA YA?

Juzi hapa pale baharini wanajeshi wa Marekani walidiriki kuwafyatua na kuwaua genge la watu waliosadikika wanasafirisha madawa ya kulevya.

Umejifunza nini?

Kama mwizi ni katili vile, huku wananchi wenu wanataabika na kufa kimaskini, lazima tu mzalendo achukue hatua kali za haraka ili kuwa mfano kwa wengine.

Huu ndio wakati sikuwahi kuelewa TAL anatetea nini haswa, maana alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa.

Huo ndio ulikuwa wakati wa kusimama pamoja kama taifa.

Mm nasimama na Polepole.
Mm nasimama na TAL.
Mm nasimama na Maria Sarungi.
Mm nasimama na Mange.
Nasimama na yeyote anayetetea nchi yake sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…