Tusiukubali mradi wa Wachina wa Bandari ya Bagamoyo kwa sababu zozote zile. Utakuwa ni mtego utakaotunasa kama nchi

Tusiukubali mradi wa Wachina wa Bandari ya Bagamoyo kwa sababu zozote zile. Utakuwa ni mtego utakaotunasa kama nchi

Ndio ule Mkataba unaowala Djibout, Zambia na Kenya? Ule mkataba nakumbuka Mwendazake aliwahi kuweka baadhi ya masharti pindi tu ilipoibuliwa na Job bungeni. Moja kati ya Masharti alisema ni kutokuendeleza Bandari yoyote ile katika nchi hii na yeye Mchina ndiye angekuwa anasimamia kila kitu kuanzia Ukurugenzi mpaka kibarua hapo ndani kwa miaka 100 arudishe faida yake.
Ndiyo maana mimi kama mwanachama mwaminifu wa Upinzani nilimuunga mkono magu kwenye hilo,ni mwendawazimu tu ndiye angekubali mkataba wa kixenge namna ile,ni kama tu mchina alituamrisha tuue bandari zetu zote, Dar,tanga,mtwara kisha tutumie bandari yake kama vile hii nchi ni mali yao!! Hapa kikwete alitukosea adabu kabisa,kikwete yupo hai,ningetanani nipate nafasi ya kumweleza uso kwa uso kuwa alitudharau to the maximum kutuletea takataka ya namna ile,rest well jpm!! At least for this!
 
Kongole kwako Mkuu,umegonga penyewe,yes pengine Magu alikuwa anapindisha mambo mengine but kwa hii ni Kama aliamua kuweka wazi kile ambacho kilikuwemo katika mkataba kupitia Kakoko,swali jingine la kujiuliza,Kakoko alisema hawajawazuia kujenga bali wamewaambia hayo masharti ndiyo hapana,kama ni umiliki wa ardhi watapewa wa 33yrs pamoja na masharti mengine kuwa reviewed. Ni nini kiliwafanya Wachina kuingia mitini hata baada ya kuandikiwa barua kukumbushwa warudi kwa meza ya makubaliano waweke terms upya kisha waendelee na ujenzi? Huoni ni kama zile terms walizozitaka wao zilipopigwa chini na wao wakaingia mitini. Hapa ndipo point yako inakuja wale wanaotetea huu mradi mbona wanashindwa kutetea hoja zao kwa kuzipinga za Kakoko? Jibu ni simple tu,kile alichosema Kakoko ndiyo uhalisia wenyewe wa huo mkataba.
Sahihi kabisa
 
'
IMG_20210409_214539.jpg
IMG_20210409_214545.jpg
 
Kwani hatuwezi kuendesha movement...#wekenimkatabahadharani.
Kwenye account ya Twitter ya Rais?
Hatuwezi andamana 😳🙄😂😂😂
MIKATABA MIBAYA KAMA ULE WA BAGAMOYO, HUWA NA KIPENGELE CHA KUTOUTOA HADHARANI. KAWAIDA HUBANDIKWA MUHURI "TOP SECRET". MAJADILIANO HUFANYWA SEHEMU AMBAYO HAKUNA MWINGINE KUINGIA/KUFIKA. KUINGIA CHUMBA CHA MAJADIALIANO UNASECHIWA, HAKUNA KUINGIA NA NCHOCHOTE NA HAKUNA KUTOKA NA CHOCHOTE. MINITI HUCHUKULIWA NA KUTUNZWA NA WENYEWE. HIVYO NDIVYO YALIVYOKUWA MAJADILIANO YA BANDARI YA BAGAMOYO.
 
Sasa iyo nguvu unayotumia tukatae huo mkataba basi ielekeze ili tuweze kuuona huo mkataba.

Unakataaje kitu ambacho hukifahamu? Embu jaribu kutafakari na wewe.

Nikukumbushe tu kuwa, hao hao wachina unaowaona na kusema wametaka bandar sijui wapi, ndio waliomsaidia Nyerere kuongoza nchi kwa kipindi chote alichokuwa madarakani.

Kuanzia ndege za jeshi, silaha za kijeshi, mifumo ya utawala n.k
Wachina hawakumsadia Nyerere kuongoza nchi. Alichokataa Nyerere ni marafiki kumchagulia marafiki. Yeye misaada alipata toka Magharibi na Mashaririki. Miradi mikubwa ya China TZ ilikuwa Urafiki Textile Mill, Ubungo Farm Implements, na TAZARA. Mingine yote ilitoka Magharibi. Wakati huo watu walikuwa wanaikimbia China. China walipata mbinu na kuifanya misaada/miradi yao kuwa na masharti nafuu kuliko Ulaya. Hapo ndiyo nchi zikaelekea huko. Sasa hivi China ana nguvu, na mikopo yao mikubwa wana masharti magumu hasa pale wanapoona faida kwenye masharti hayo. Wao wana kipengele cha rehani, na total ownership kabla hujamaliza kulipa. Such conditions can not be sustained.
 
Ndio ule Mkataba unaowala Djibout, Zambia na Kenya? Ule mkataba nakumbuka Mwendazake aliwahi kuweka baadhi ya masharti pindi tu ilipoibuliwa na Job bungeni. Moja kati ya Masharti alisema ni kutokuendeleza Bandari yoyote ile katika nchi hii na yeye Mchina ndiye angekuwa anasimamia kila kitu kuanzia Ukurugenzi mpaka kibarua hapo ndani kwa miaka 100 arudishe faida yake.
TUKUMBUKE!,Sisi Tanzania tunapaswa kuwa na bandari nyingi kuliko nchi ya Afrika Kusini.
Tanzania tunazo bandari muhimu(Tanga,Kilwa,Lindi,Mtwara)! Tena kuna zile bandari za Ziwa victoria,Tanganyika na ziwa Nyasa).
 
Magu na timu yake hawakuwa watu wa kuaminika sana hasa pale walipotaka mambo yao yaonekane yako sawa na wako sahihi siku zote ila upande wa wale wanaopigia chapuo bandari ya Bagamoyo kupewa Wachina waijenge wameshindwa kabisa kwa miaka sasa kukanusha hata dai moja la yale yaliyosemwa na Kakoko alipozungumza na waandishi wa habari sababu za huo mkataba kukataliwa!

Wale wanaopigia chapuo hiyo bandari kujengwa na Wachina wamekwepa kabisa kuzungumzia hivyo vipengele vinavyodaiwa vilikuwa kwenye huo mkataba, wamebaki kutuimbia wimbo mkataba ni mzuri sana, kuna uwekezaji mkubwa, ni fursa adimu tusiipoteze, wachina ndugu zetu na blah blah nyingine nyingi.
Nia kubwa ya Fulani kutembelea China ilikuwa na kupokea chake ili autetee mradi. Alipokuta Magu ana mawazo tofauti akaufyata. Sasa Magu kaondoka, ndiyo anaupigia chapuo. Maana Wachina wamemkaba koo baada ya kula chao bila kuwasaidia.
 
Usiukubali wewe na Nani? Pambana utafute pesa, ripoti za CAG zimekuwepo miaka na miaka hakuna jipya. Wanyonge tuzidi kusaka noti. 2015 tulipigwa
Akubali ama asikubali, bado serikali itaamua yenyewe bila yeye kuwepo.
Raia ni apambane tu, tutafute pepa, hutoletewa unga! 😂 😂 😂
 
Akubali ama asikubali, bado serikali itaamua yenyewe bila yeye kuwepo.
Raia ni apambane tu, tutafute pepa, hutoletewa unga! [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Bila intervention ya serikali hata hiyo pesa unayoitafuta hutaipata,na ukiipata haitakuwa na maana!! Fikiri tena.
 
JF inaweka kumbukumbu katika mijadala yetu, hapo chini nimekuta kuna mchangiaji ameweza kuweka mawazo yake na mchango.
C&P.

Moja ya maoni ya wadau[emoji116]

Najua topic imepita, lakini ninajua kidogo kuhusu mradi wa Bandari ya Bagamoyo na napenda kumuunga mkono Mhe Spika kwa hoja zifuatazo. Na naamini Serikali yetu itazichukulia kama ushauri wa Mbunge kwa Serikali, ambao ndio wajibu wetu wa msingi kama Wabunge.

Muhimu kujua background ya mradi wa Bandari ya Bagamoyo. Kwanza, mradi huu ulibuniwa na Serikali yetu kama Bagamoyo Special Economic Zone mwaka 2004 chini ya Mpango Kabambe wa Ujenzi wa Sekta Mpya ya Viwanda. Serikali ya Japan ndio ilitusaidia kwenye hili. Mradi huu uliitwa “Tanzania-Mini Tiger 2020” na ulikuwa chini ya Wizara ya Viwanda.

Mamlaka ya Bandari nayo ilibuni Mpango Kabambe wa Miaka 20 wa Uendelezwaji wa Bandari za Tanzania (The Tanzania Port Development Master Plan 2009-2028) ambao ulipendekeza Bandari ya Bagamoyo ijengwe katika miaka ya 2021/2022 ili iwe tayari kujaza nafasi baada ya Bandari ya Dar es Salaam kufikia ukomo wa kuweza kuongezewa uwezo. Kwahiyo mambo mawili ya msingi hapa ni kwamba: (a) Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo tuliubuni sisi wenyewe, ulikuwa sehemu ya mipango yetu ya muda mrefu na haukujengwa kwa msukumo wa Wachina; (b) mradi wa Bandari ya Bagamoyo sio ni mradi wa Bandari, bali ni mradi wa Ukanda wa Kiuchumi ambao unaendana na mji wa viwanda.

Mwaka 2009 Mamlaka ya Bandari, kupitia kampuni ya Hamburg Port Counsulting ya Ujerumani, ilifanya upembuzi yakinifu wa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo na
kuona una manufaa kutekelezwa. Mwaka 2011, Wizara ya Viwanda na Biashara, kupitia CowiConsult, nayo ilifanya upembuzi yakinifu wa Mradi wa Bagamoyo Special Economic Zone (BSEZ), kwa kufungamanishwa na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.

Mipango yote hii ilikuwa ni yetu wenyewe, na tulijiridhisha kama nchi kwamba Bandari ya Bagamoyo tunaihitaji na tukaiweka kwenye Mpango wa Pili wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Taifa kama Mradi wa Taifa wa Kielelezo.

Mwaka 2013 na 2014, Kampuni ya China Merchants Ports Limited, ikiungana na Mamlaka/Mfuko wa Uwekezaji wa Oman (OIA), waliomba kuwekeza katika Mradi wa BSEZ na Bandari ya Bagamoyo. Baadaye kidogo, Korea Kusini nao, kupitia Taasisi yao ya Science and Technology Policy Institute” (“STEPI”) ilikamilisha Upembuzi Yakinifu wa kuwekeza katika kujenga na kuendeleza “Bagamoyo High Technology Park” kwa kushirikiana na EPZA pamoja na COSTECH. Kwahiyo hoja nyingine ya kuzingatia hapa ni kwamba Bagamoyo sio uwekezaji wa Wachina pekee, kama inavyodhaniwa. Yapo mataifa mengine. Oman wanaweka pesa yao nyingi. Na Korea Kusini nao wanaweka pesa na maarifa yao.

Kama nilivyoeleza hapo awali, kwa mujibu wa Mpango wa Pili wa Miaka Mitano wa Maendeleo (“FYDP II), Mradi wa Bagamoyo Special Economic Zone (BSEZ) ni Mradi wa Taifa wa Kielelezo. Mradi huo unatarajiwa kuwa utavutia uwekezaji wa Dola za Kimarekani bilioni 10; utakuwa na Viwanda 760 na hatimaye kutoa ajira 270,000 kwa awamu ya kwanza. Majadiliano ya Utatu wa Serikali ya Tanzania, China Merchants na Mfuko wa Uwekezaji wa Oman yalikuwa yanaendelea kuelekea makubaliano na hatimaye kuingia Mikataba ya Uwekezaji kabla ya kusimamishwa.

Zipo hoja kubwa tatu zinazosemwa kuhusu mradi huu: (1) utatutwika madeni kama vile Kenya na Sri Lanka ambapo Wachina walilazimika kutaifisha Bandari; (2) tutaua bandari ya Dar es Salaam; (3) haturuhusiwi kuendeleza Bandari yoyote na haturuhusiwi kutia mguu pale Bagamoyo kwa miaka 99.

Hoja hizi zote sio za kweli, na kwa kweli wawekezaji wa huu mradi wamekuwa wana-struggle namna ya kuzijibu kwasababu zinatolewa na watu wakubwa, na hao wawekezaji, hasa wa Oman, ni mamlaka za Serikali na wasingependa malumbano na Serikali yetu.

Hoja ya kwanza, kwamba tutakopa na kujitwika deni kubwa sio ya kweli: kwenye mradi huu hakuna hata senti tano ya mkopo tunachukua. Huu ni uwekezaji. Hakuna deni hapa, ni pesa ya kigeni inaingia kuwekezwa.

Hoja ya pili kwamba tutaua bandari ya Dar haina mantiki, kwasababu hata kabla Wachina hawajafika ilikuwa ni ndoto na mipango ya Mamlaka ya Bandari kujenga Bandari ya Bagamoyo. Ukisoma Mpango Kabambe wa Miaka 20 wa Uendelezwaji wa Bandari za Tanzania (The Tanzania Port Development Master Plan 2009-2028), wenyewe Mamlaka ya Bandari walitaka Bandari ya Bagamoyo iwe imejengwa ifikapo mwaka 2023. Bandari za Bagamoyo na Dar sio bandari shindani. Ni bandari zitakazosaidiana kuongeza shehena ya mzigo unaopita nchi mwetu. Full stop! Pia Bandari ya Bagamoyo itajengwa kwa kuzingatia teknolojia ya uundwaji wa meli za kisasa (4th Generation Shipbuilding Technology Port). Meli hizi, ambazo zitakuwa zinaongezeka kadri miaka inavyokwenda, haziwezi kutia nanga kwenye bandari ya Dar. Na kama unaitazama nchi kwa miaka 30, 50 ijayo, Bandari ya Dar ina ukomo wa upanuzi. Lazima kama nchi kujenga Bandari mpya kubwa katika ukanda huu ili kuendelea kunufaika na faida ya kijiografia.

Hoja ya tatu kwamba Wachina wanataka tusijenge wala kuendeleza Bandari yoyote kwa miaka 99 na tuwape wao bandari hiyo bila sisi kutia mguu pale sio ya kweli. Hakuna pahala popote wawekezaji wametoa hayo madai. Ukweli ni kwamba kote duniani mwekezaji anapoweka hela yake mwenyewe kwenye mradi atataka muda wa kutengeneza faida kabla hajakukabidhi mradi. Hapa Wachina na Wa-Oman walitaka miaka 33 ya concession. Je, ni mingi au ni michache? Inategemea pesa iliyowekwa (US$10bn) na standard practice kwingine duniani. Reli ya kuunganisha UK na France, ambayo imejengwa na sekta binafsi ina concession ya miaka 50. Kwa bandari standard practice ni miaka 25-40, kutegemeana na ukubwa wa uwekezaji. Cha msingi kwa timu ya negotiators wetu ni kupata financial models za wawekezaji na kuzichambua na kuona wanaanza kupata faida baada ya muda gani. Na cha kutambua pia ni kwamba concession inahusu tu faida ya Bandari na kwamba katika kipindi hiki cha concession bado TRA itakuwa inakusanya kodi nyingine zote husika za mizito bandarini.

Suala lingine la kutazama katika kufanya maamuzi ni kuangalia dunia inaelekea wapi kwenye biashara ya kimataifa. Tutake tusitake, nchi yetu inategemea biashara ya nje kimapato na China kwasasa ndio kinara wa biashara ya import and exports duniani. Inaongoza kwa kuagiza na kuuza bidhaa nje na itaendelea kuwa kinara kwa miaka 50 inayokuja. Ukifungamana nao, utashinda. Kwa mujibu mpango wa China wa Belt-and-Road-Initiative (BRI), meli kubwa za bidhaa zitakazopita katika 21st Century Maritime Silk Road kusafirisha bidhaa kati ya China na Afrika ya Kati na Kusini, zitafikia katika moja ya Bandari za Mwambao wa Mashariki ya Afrika, kama Mlango na Kituo Kikubwa cha kupokea, kuhifadhi kwa muda na kusafirisha shehena kwa meli au usafiri wa nchi kavu. Kulingana na kudra ya kijiografia ya Tanzania ambayo inaimarishwa na uwepo wa Reli ya Kati (SGR) tunayojenga pamoja na reli ya TAZARA, Bandari ya Bagamoyo ambayo itaunganishwa na Reli ya Kati na TAZARA, itakuwa haina mshindani Nje ya Tanzania katika dhana nzima ya ushirikiano wa maendeleo ya uchumi baina ya China na Afrika, kupitia BRI kwa muktadha wa 21st Century Maritime Silk Road.

Mwisho, ni muhimu kutambua kwamba kuna siasa za ushindani na majirani zetu kwenye hili suala. Jirani zetu Kaskazini yetu wanapigana kufa na kupona mradi huu usitokee. Kwahiyo mtaona disinformation nyingi kuhusu huu mradi huku baadhi ya watu wetu wakitumika bila kujijua.

Wenzetu tayari wameanza tena kuifuata kampuni ya China Merchant kuwashawishi wahamishie ule mradi Kenya kule LAMU. Mwaka 2018 wakati wa mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), kiongozi wao alikwenda Shenzen kuzungumza na China Merchant kuwashawishi waende kwao. China Merchat walikataa na ndio walikutana na Waziri Mkuu Mhe Majaliwa. Na majuzi, tarehe 25 Machi 2021 wameandika barua tena China Merchant kuomba mradi upelekwe kwao (barua nimeiona).

Mwisho, nitamalizia kwa hadithi ndogo: mwaka 1970, wakati Dubai bado ni kamji kadogo jangwani, wazungu waliona potential ya location ya Dubai kibiashara na wakamwendea mfalme wa wakati huo Rashid bin Saeed Al Maktoum kupendekeza wakajenge bandari na waiendeshe kwa miaka 30. Washauri wake wakamwambia tusiwape Wazungu bandari kwenye nchi yetu. Sheikh akawauliza “sisi tuna pesa ya kujenga?”, wakajibu hapana, akawauliza “tutaipata lini”, wakasema hatujui, akawauliza “Dubai itaendelea kuwepo miaka 30 ijayo?”, wakajibu ndio, akawauliza “baada ya miaka 30 wataing’oa bandari na kuondoka nayo?”, wakajibu hapana, akasema “tuwape”. Wazungu wakajenga Port Rashid mwaka 1972. Miaka 30 ikapita haraka. Watu wa Dubai wakajenga uwezo wa kuendesha bandari na wakaanzisha Dubai Port World (DP World), moja ya makampuni makubwa duniani. Dubai sasa ni kinara wa bandari duniani. Majuzi wamechukua bandari za Senegal na Angola. Na wamejenga bandari hadi Rwanda ambapo hakuna hata bahari, wanawasaidia Rwanda kwenye biashara ya logistics.

Mpendwa wetu hayati Rais Magufuli alipenda maendeleo. Alitaka nchi yetu ipate manufaa kwenye miradi na mikataba. Namna ya kumuenzi na kufanya makubaliano yenye tija kwa taifa kwenye mradi wa Bagamoyo. Na hilo linawezekana kama timu yetu ya negotiators itakuwa makini kuzingatia maslahi ya nchi.

Haya ni mawazo ya mtu binafsi,binafsi nitaendelea kumwamini Kakoko kwasababu alikuwa kwenye nafasi ya kuuona Mkataba wenyewe. Labda niulize tu swali dogo hapa,kwenye clip ya Kakoko anasema waliandika hadi barua ya kuwakumbusha kurudi kwa meza ya majadiliano ili waendelee na ujenzi baada ya kufikia muafaka,ni nini kiliwafanya hao Wawekezaji wasirudi tena pamoja na kuandikiwa barua rasmi? Na kwanini waibuke sasa hivi baada ya JPM kufariki na kuona kuna utawala mpya? Ni kwamba hawakutaka tena majadiliano na Uongozi uliokuwepo na hapo ndipo penye “red flags”
 
Tusiukubali kwa naamna vip? Kwa kutoa comment humu?.

Tanzania tutaendelea kuamuliwa siku zote na wanasiasa kwasabab kama wananchi ndivyo tulivyoamua...who can stop them!?...we have long way to go kama taifa.

Kwenye hili tuendelee kusubili Nini wao wataamua kwasabab hakuna namna, likiwa jema tutashukuru na likiwa baya tutalalamika halafu mwishoe tutawaacha kama walivyo. This is Africa
 
Tuna sababu moja kubwa ya kuukata Mradi wa Wachina wa Bandari ya Bagamoyo nayo ni historia mbaya ya China kona mbalimbali za dunia walipotekeleza miradi ya aina hii au walipozikopesha nchi mikopo mikubwa ya miondombinu. Wamechukua bandari Sri Lanka, Pakistan, Australia na Djibouti kupitia mikataba ambayo haieleweki ni yenye utata sana.

Kama huko wameweza kufanya hivyo sisi hatutaweza kuwadhibiti na kuibakiza bandari ya Bagamoyo kuwa bado mali yetu endapo tukiwakubalia wajenge bandari hapo.
Tusijidanganye, sote tunafahamu jinsi gani mikataba midogo tu ya madini imekuwa changamoto kubwa kwa taifa hili, huu ukizingatia na usiri wa mikataba utakuwa funga kazi, tutauzwa mchana kweupe kama enzi za Mangungo wa Msovero.

Tukubali tu kwamba wao ni wajanja na kutekeleza kwa miradi ya aina hii duniani kumewapa ujanja zaidi. Tusikubali bandari zetu kujengwa na kuendelezwa na wageni kwa sababu yoyote ile. Kama tunafikiri ni muhimu sana na tunatakiwa kuwa na Bandari Bagamoyo tukope pesa tujenge wenyewe, vinginevyo tutaiuza nchi yetu nzuri.
Hatuna presha ya kujenga bandari ya bagamoyo kwani bandari ya Dar na zile nyingine bado hazijazidiwa, jambo ambalo linatoa mwanya wa kuweza kujenga bandari ya bagamoyo kwa pesa zetu za ndani, kuliko kuuzwa kama kuku..
 
Unaifahamu vizuri serikali yako mkuu. Hawana utaratibu wa kuweka mikataba ya uwekezaji hadharani hivyo usitegee kuna siku utauona. Endapo mkataba utaridhiwa watakuja na maneno matamu tu ya kuupamba na kuwaaminisha wananchi kila jambo liko sawa kama ilivyofanyika kwenye mikataba mingine.
Walioko madarakani ni Ccm na tuliambiwa ni wazalendo kweli kweri.
Nchi hii imeriwa sana
 
Haya ni mawazo ya mtu binafsi,binafsi nitaendelea kumwamini Kakoko kwasababu alikuwa kwenye nafasi ya kuuona Mkataba wenyewe. Labda niulize tu swali dogo hapa,kwenye clip ya Kakoko anasema waliandika hadi barua ya kuwakumbusha kurudi kwa meza ya majadiliano ili waendelee na ujenzi baada ya kufikia muafaka,ni nini kiliwafanya hao Wawekezaji wasirudi tena pamoja na kuandikiwa barua rasmi? Na kwanini waibuke sasa hivi baada ya JPM kufariki na kuona kuna utawala mpya? Ni kwamba hawakutaka tena majadiliano na Uongozi uliokuwepo na hapo ndipo penye “red flags”
Ni vizuri mambo yawe transparent kwa faida ya jamii kwani leo na kesho wenye madaraka huondoka lakini nchi inabaki na wananchi wake.
 
Tanzania gives Chinese firm conditions for Bagamoyo port

Sunday October 20 2019

Tanzania say conditions set by the investor were tantamount to selling Tanzania to China.

The government of Tanzania has issued an ultimatum to the Chinese investor in the $10 billion Bagamoyo port project to either accept and work with its terms and conditions of the contract or leave.

Tanzania Ports Authority chief executive Deusdedit Kakoko said the government rejected and revised five stringent demands made by the investor—Beijing-based China Merchants Holdings International—because they were not beneficial to the country.

The Chinese investor has now been offered a 33-year lease instead of the 99-year one asked for.

Two, the investor has been informed that there will be no tax holiday and they will be subjected to all taxes designed by the Tanzania Revenue Authority.

Three, that there would be no special status and they would be required to pay the market rate for water and electricity like any other investor.

Four, they could not start and run any other business they deemed necessary within the port without government’s approval and were open to scrutiny and regulation by relevant agencies in line with law like any other investor.

Five, they were informed that the government of Tanzania was free to develop other ports to be in direct competition with Bagamoyo.

Once the Chinese firm agrees in principal with the government’s new conditions, the project can move to the next stage which is execution in collaboration with the Oman’s State General Reserve Fund (SGRF).

The Bagamoyo port development project was initiated late into the tenure of retired president Jakaya Kikwete.

But President John Magufuli ordered an immediate suspension of the project in January 2016, saying the conditions set by the investor were tantamount to selling Tanzania to China.

The port, to be built in Bagamoyo, 75 kilometres north of Dar es Salaam, would dwarf neighbouring Kenya’s port at Mombasa, east Africa’s trade gateway some 300 kilometres to the north, and include an industrial zone and rail and road links to a region hoping to exploit new oil and gas finds.

Reference
 
Ni mlevi mwendawazimu tu anayeweza kukubali masharti ya huo mradi, hayo ni maneo ya hayati JPM
 
Back
Top Bottom