Tusiwabeze wanaosomesha watoto shule za Tsh. Milioni 40

upo sahihi ndg.
mohamed dewji,abubakar bakhresa, yusuph bakhresa, mjukuu wa mzee bakhresa anaitwa zayid bakhresa na wengineo wa hadhi hiyo,wamesoma international school of tanganyika.
 
Acha uongo mkuu, hizi shule zinapatikana hata maeneo mengine ya nchi.

Mwanza kuna, "Mwanza international school"

Iringa pia ipo "Iringa international school"

Hata "Savanah plains" ya Shinyanga Zamani ilikuwa inatumia mitaala ya kimataifa.

Kwa hiyo ni uongo kusema shule hizo ziko Moshi na Arusha tu.
 
hata morogoro ipo lakini hii mikoa zipo moja moja, si kama arusha na moshi zipo nyingi
 
Master J ni Engineer na kasoma UK
 
Hebu taja Arusha zipo ngapi na Moshi zipo ngapi?

Usije sema zipo nyingi kumbe zipo mbili au tatu.

Zikizidi tano mkoa mmoj, mods wanipige ban.
Arusha na moshi ni miji ya karibu sana wanashea vingi hata airport, wengi hufanya shughuli Arusha wanarudi Moshi and viceversa,

unataka list ya shule, ok!

Arusha Meru International school .
International school of Moshi
International school of Tanganyika
The Tanganyika schools
Keneddy house
St Constatine
UWC East Africa
Jaffery Academy
Christ Church International School
Sunflower internationa school

Kiufupi hawa watu wa Moshi na Arusha kwenye elimu wapo mbali mno, mtu akiwa na iwezo wa pesa haoni anasomesha huko.

Huko kwengine naona matajiri wengi bado wanakazania watoto wao shule hizi za Necta, bado wana mwamko mdogo kuamini kwamba shule ni saint marys ama saint francis.
 
Mikoa iliyo karibu karibu ni mingi, hata Dar na pwani ni karibu na wanashare vingi.

Taja mkoa mmoja kati ya Arusha au Moshi, wenye shule angalau tano za international. Kama hazifiki maana yake hata huko nako ni chache tu.

Unaandika as if watu wa Arusha au Moshi watoto wao wote wanasoma international school. Kumbe kila mkoa shule hazifiki hata tano. Asilimia 99.9 ya wanafunzi wa Arusha na Moshi hawasomi International school. Na bado hakuna ushahidi watu wanaosoma hizo shule wote wanatokea Arusha au Moshi.

Ulisema mikoa mingine hakuna international school, tumekutajia kukuonyesha hata sehemu zingine zinapatikana. Unaleta hoja ya wingi, kumbe hata unakosema ni nyingi bado chache.
 
Kwa arusha zinazidi tano
St costantine
Braeburn
St jude etc
 

Da Mange pia alisoma Arusha St constantine.
 
Hizo international schools kwa Tanzania nzima zipo chache sana sidhani hata kama zinafika 30.

Ni shule ambazo wenye uwezo wa kusomesha huko ni wachache sanaaa, hata hawa waarabu na wahindi wengi tu wanasomesha watoto hizi english medium

Wanaopeleka huko ukiachana na mabalozi wa ulaya wanaosomeshewa na bajeti za nchi zao ni mpaka uwe Tajiri, ujue utofauti wa shule hizo na hizi za Necta, uwe na exposure flan ya maisha ya nje.

Kwa watu wa mkoa wa Kilimanjaro huku mwamko wa elimu ni mkubwa sana na shule ni nyongi sana toka zamani, na wengi walipata exposure ya kusoma ulaya huko tangu miaka ya zamani hivyo kuna mwamko wa elimu, wengine nao walishasomeshwa hizo shule nao wanaendeleza utamaduni wa kusomesha watoto wao, pia zikitokea nafasi za kusomesha watanzania bure wanawekana wao chapchap.

Sio shule za kila mtu hizi,
 
Uwe unajiongeza basi kabla ya kukngea, hivi kweli kabisa umeamua kuilinganisha Jiji kubwa la Dar linalozidi kupanukia mkoa wa Pwani na jiji dogo hili la Arusha ambalo limepewa hadhi ya jiji juzi tu hapo ?

Ila tatizo hapo Dar na Pwani wazawa wa hapo wazaramo wana mwamko mdogo wa elimu hata awe tajiri mwamko bado mdogo kupeleka mtoto hizo shule, hata huko Dar bado hizo shule unakuta kwa jamii zetu za makabila ya hapa kwetu ni watu wa Moshi ndio wamejaa kimtindo, hata huyo master J usione hatembelei magari mazuri, watoto wake wote watatu wanasoma shule hizo
 
40M per yr sio kubwa ni umaskini tu.

Imagine mtu analalamika kutoa Tsh.500 kila jumamosi kwa mwezi mmoja yaani Tsh.2000 tu. Anasema walimu wanamuibia wakati elimu ni ya mwanae.

Mwanangu lazima asome shule za namna hiyo.
 
Wewe mchaga umefanya tafiti kujua hizo shule wengi ni watu wa huko au kisa huyo master j??

Acha mambo ya ukanda, una hoja sometimes utafika mbali.
 
Hebu taja Arusha zipo ngapi na Moshi zipo ngapi?

Usije sema zipo nyingi kumbe zipo mbili au tatu.

Zikizidi tano mkoa mmoj, mods wanipige ban.
Kennedy House International School


Jaffery international school


Tanganyika Junior School


Braeburn School


Arusha Meru Int.School Primary School


UWC East Africa — Arusha Campus


St. Constantine's International School

Litletreasure and blossom international school
 
Taja zinapatikana Arusha zifike tano.

Na moshi zifike tano.

Kilimanjaro na Arusha ni mikoa tofauti.
 
Taja zinapatikana Arusha zifike tano.

Na moshi zifike tano.

Kilimanjaro na Arusha ni mikoa tofauti.
Kilimanjaro na Arusha ni mikoa tofauti ila mji wa moshi na jiji la arusha ni pua na mdomo.

watu wengi tu hufanya kazi upande mwengine wanarudi kulala kwengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…