Tutafakari pamoja: Waziri Mkenda anaposema wasaidizi wa Rais waliweka kauzibe asimwone mkuu wa nchi, hadhi ya Waziri ipoje kwani?

Tutafakari pamoja: Waziri Mkenda anaposema wasaidizi wa Rais waliweka kauzibe asimwone mkuu wa nchi, hadhi ya Waziri ipoje kwani?

Nyie mnaamini anayosema huyu waziri ? Kuna njia nyingi za waziri kuonana na rais. La mwisho angeweka tatizo lake rasmi kwa maandishi.
 
Waziri wa Elimu ndugu Mkenda katika hotuba yake ya uzinduzi wa Mtaala mpya wa elimu ametoa kali ya mwaka pale aliposema kuwa Yeye na timu ya wataalam walipata ugumu kuonana na Rais ili wampatie briefing ya yaliyomo kwenye mtaala mpya. Nimezalisha maswali kadhaa ya tafakuri hapa....
  1. Waziri ambaye ameteuliwa na kuapa mbele ya Rais, na ambaye ni mjumbe wa Baraza La Mawaziri ambalo maamuzi yake hayahojiwi na chombo chochote nchini, ana hadhi kiwango gani ndani ya serikali?
  2. Waziri na Rais wanawasiliana ama kuonana vipi ilihali Rais ndiye amewateua kama wasaidizi muhimu kusimamia sekta zote nchini?
  3. Wasaidizi wa rais wana mamlaka gani kumzuia Waziri kuonana na rais pale anapoomba kufanya hivyo?
  4. Ikulu yetu ina utaratibu gani wa kumsaidia rais kutekeleza majukumu yake ikiwemo kuonana ama kujadiliana ama kuwasiliana kwa karibu na wasaidizi wake muhimu na wakuu wa sekta zote nchini? yaani Mawaziri na manaibu wao..
  5. Kauli ya Waziri Mkenda inatuma ujumbe gani kwetu sisi wapigakura ambao hapo Oktoba tutatumia vichinjio vyetu kuchagua viongozi wa nchi?

Karibuni tujadili
Steve Nyerere au Shilole wana nguvu kuliko Waziri
 
Kuna dogo mmoja kanambia vitu vya kuhuzunisha na vimenifikirisha..

Kwenye hizi interview za ualimu ana division one o- level na a-level na chuo gpa 3.6 kwenye pepa za utumishi not selected

From credible source mitiani ya ualimu utumishi inavuja na watoto wa maskini Hawa penyi kwenye saili za uonevu..

Pole kwa WATANZANIA wa Hali ya Chini..
😲😲😲
 
Sasa huyo Waziri kama kweli alikuwa na lengo la kuonana na rais akakataliwa alishindwa nini kumpigia Steve Mengele, au Shilole au Mwijaku wamsaidie? Ina maana hana namba zao?
🤔 🤔 🤔
 
Mnadhan Prof Mkenda ni mjinga hadi aseme yale yote hadharani mbele ya WaTz...? Anajua nini kitatokea na amejipanga.
Ndiyo maana hata kile kikaratasi amekisoma kwa kujiamini huku akiwageukia walimpatia.
Prof Mkenda October apigiwe kura nyingi arudi bungeni huyu mzee ana faida kwa nchi yetu.
Ukitzama vyema yule mleta kikaratasi alipita nyuma hadi upande aliokuwa amekaa katibu wa rais then ndio akaja na kimemo
 
Dogo shule kwanza picha linaanza time over dogo kagoma kukusanya pepa anaendelea kujaza anaambiwa time is over anaendelea kujaza kwa hio ticha sababu dogo ni mtoto wa mkubwa inabidi amuache aendelee kujaza mpaka atakapojisikia yeye kukusanya chumba kizima kabakia peke yake
Mwaka gani na mzazi alikuwa na cheo gani?
 
Rais ni Taasisi..lile jumba leupe limejaa watu wanapiga kazi - Samia hajai jumba lote lile - hao watu ndo wanaongoza nchi, hao watu ndo wanateua hao mawaziri kwa niaba ya Rais, hao watu ndo wanateua wakuu wa mikoa, wilaya etc.Rais akifanya kila kitu si atakufa kabisa - watu wanareport kwenye PRESIDENCY - Ndio maana Samia anatembea ulimwenguni huko lkn huko nchi inatembea na mikeka inatoka.
Usishangae..huo ndo ukweli mawaziri sio watawala - sio Dola but Wakuu wa Mikoa na Wilaya ni sehemu ya watawala na Dola.
 
Mnadhan Prof Mkenda ni mjinga hadi aseme yale yote hadharani mbele ya WaTz...? Anajua nini kitatokea na amejipanga.
Ndiyo maana hata kile kikaratasi amekisoma kwa kujiamini huku akiwageukia walimpatia.
Prof Mkenda October apigiwe kura nyingi arudi bungeni huyu mzee ana faida kwa nchi yetu.
Mkenda yuko tayari kwa lolote hataki ujinga na hili lilimkera sana ndo maana ameongea hapo!
 
Back
Top Bottom