Tutamkumbuka kwa lipi Ummy Mwalimu?

Kwani yote haya yameanza wakati wa Ummy? Mara nyingi tatizo kubwa katika mifuko kama hii bi serikali kukopa bila kurudisha. Wizi na ubadhirifu unachangia lakini sio kama ukopaji wa serikali. Bila kulishughulikia hili NHIF haiwezi hata siku moja kutimiza majukumu yake ipasavyo. Hata aje nani.

Amandla...
 
Kwa kusababisha vifo kwa watoto wa masikini kwa kuwaondolea toto afya kadi
 
Tatizo letu ni kuwa tunashughulikia individuals wakati tatizo ni mfumo. Huyo waziri tunayemsema hana nguvu kiasi tunavyoaminishwa. Kinachotakiwa ni kurekebisha mfumo. Lakini hamna political will ya kufanya hivyo.

Amandla...
 
Vyeo vya mawaziri ni vya shukrani wala havina tija yoyote kwa nchi
 
Hii teua tumbua haitokuwa na mantiki mpaka siku akimtumbua Mwigulu Nchemba.
 
Ujenzi
Wa vituo vya afya na hopsitali ni tamisemi
 
Namkumbuka Ummy kwa kukiri kuwa Covid imeingia nchini na kutoa takwimu mara kwa mara za watu waliothirika. Kwenye hili nampongeza.

Amandla...
 
Nani akasema "yamneanza wakati wa Ummy Mwalimu", hivi huwa hamuelewi mnachokisoma au mnakurupuka tu?

Ummy mwalimu katekeleza majukumu yake kwenye baraza la mawaziri, sasa inabidi apate muda wa kujifungua kitu kipya na kulea wanawe wengine.

Kama ulikua huelewi, naona sasa umeelewa. Utamuona bungeni kama mtoto atawacha kumchagiza tumboni.
 
Kwani nimemtaja mtu? Mimi nimeuliza swali ambalo inaelekea hautaki kulijibu. Nilichokisema ni kuwa tatizo NHIF sio la Ummy bali ni la mfumo mzima.

Ummy bado ni mbunge kwa hiyo hilo la kuonekana bungeni sio habari mpya. Hilo la uja uzito wala halituhusu.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…