Tutamkumbuka kwa lipi Ummy Mwalimu?

Tutamkumbuka kwa lipi Ummy Mwalimu?

Ummy kashindwa kuidhibiti NHIF, NHIF watu wanaiba sana mpaka hpspitali hazilipwi. Aga Khan wamefunga, Hospitali zingine mfano Tiba, sasa hivi hawapokei bima za NHIF.

NHIF kuna pesa nyingi sana lakini kuna madudu ya kufa mtu, kama haijapewa kampuni binafsi kuiendesha, itawaondosha wengi sana.

Madudu NHIF na Madudu MADAWA ni ya kufa mtu.
Kwani yote haya yameanza wakati wa Ummy? Mara nyingi tatizo kubwa katika mifuko kama hii bi serikali kukopa bila kurudisha. Wizi na ubadhirifu unachangia lakini sio kama ukopaji wa serikali. Bila kulishughulikia hili NHIF haiwezi hata siku moja kutimiza majukumu yake ipasavyo. Hata aje nani.

Amandla...
 
Uteuzi uliofanywa na Mhe. Rais SSH tatehe 14 Agosti 2024 umemtema nje bi Ummy Mwalimu kutoka Wizara ya Afya.

Kutokana na unyeti wa Wizara ya Afya, umuhimu wake ni mkubwa kwenye jamii. Pamoja na kusimamia sera ya Afya nchini lakini ndiyo wizara inayosimamia taaluma ya wahudumu wa Afya.

Je tuna lipi la kumkumbuka dada Ummy kama mchango wake kwenye kuimarisha ama kuidhoofiaha sekta ya afya nchini

Pia soma: Ummy Mwalimu atenguliwa Uwaziri wa Afya
Kwa kusababisha vifo kwa watoto wa masikini kwa kuwaondolea toto afya kadi
 
Tatizo letu ni kuwa tunashughulikia individuals wakati tatizo ni mfumo. Huyo waziri tunayemsema hana nguvu kiasi tunavyoaminishwa. Kinachotakiwa ni kurekebisha mfumo. Lakini hamna political will ya kufanya hivyo.

Amandla...
 
Ccm yote imeoza, hawana jipya wakae pembeni.

Chadema pelekeni kesi mahakamani, hii ni timing ya kuwaondowa kudai haki ili mjikite kwenye Futuhi za ccm.

Kila siku tunasema hapa mawaziri wasitokane na wabunge hawatusikii, matokeo yake umeishiwa wa kuteuwa unakuja kuturudishia kituko kama Kabudi, Uprofesa wake zero kabisa kazi kutowa mijicho tu.
Vyeo vya mawaziri ni vya shukrani wala havina tija yoyote kwa nchi
 
Ujenzi
Amesimamia mageuzi mapya katika sekta ya Afya kwa awamu ya 4 na 5! Ujenzi wa vituo vya afya,hospitali za wilaya,ununuzi wa vifaa mbali mbali vya Matibabu,uboreshaji wa majengo,nk
Kwa kweli alijitahidi,mnyonge mnyongeni lakini yake mpe!
Nadhani Mama ameamua kumpumzisha kama Prof.Kabudi na Lukuvi,huenda atamrusha kama ataendelea mpaka 2030!
Wa vituo vya afya na hopsitali ni tamisemi
 
Namkumbuka Ummy kwa kukiri kuwa Covid imeingia nchini na kutoa takwimu mara kwa mara za watu waliothirika. Kwenye hili nampongeza.

Amandla...
 
Kwani yote haya yameanza wakati wa Ummy? Mara nyingi tatizo kubwa katika mifuko kama hii bi serikali kukopa bila kurudisha. Wizi na ubadhirifu unachangia lakini sio kama ukopaji wa serikali. Bila kulishughulikia hili NHIF haiwezi hata siku moja kutimiza majukumu yake ipasavyo. Hata aje nani.

Amandla...
Nani akasema "yamneanza wakati wa Ummy Mwalimu", hivi huwa hamuelewi mnachokisoma au mnakurupuka tu?

Ummy mwalimu katekeleza majukumu yake kwenye baraza la mawaziri, sasa inabidi apate muda wa kujifungua kitu kipya na kulea wanawe wengine.

Kama ulikua huelewi, naona sasa umeelewa. Utamuona bungeni kama mtoto atawacha kumchagiza tumboni.
 
Kwani nimemtaja mtu? Mimi nimeuliza swali ambalo inaelekea hautaki kulijibu. Nilichokisema ni kuwa tatizo NHIF sio la Ummy bali ni la mfumo mzima.

Ummy bado ni mbunge kwa hiyo hilo la kuonekana bungeni sio habari mpya. Hilo la uja uzito wala halituhusu.

Amandla...
 
Back
Top Bottom