Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Hakuna nyimbo Titanic ya ferre golla.
Ipo moja tu TITANIC ,
JB Mipana & Wenge BCBG 4×4
umeandika ili kujifurahisha ktk hali ya kunogesha mjadala au umeandika ili tu kuleta mabishano?.

twende kazi.
mwaka 2017, ferre gola alitoa album aliyoipa jina la QQJD.

album hii aliitoa kwa mtindo wa volume 1&2. kila volume ina nyimbo 11.

katika volume 1, track namba 11 ni wimbo mzuri wenye maadhi ya rumba unaokwenda kwa title ya jina "titanic".

wimbo wenyewe ni huu hapa:
Titanic | Boomplay Music tumia app ya boomplay kuusikiliza.

au kama vipi ingia hapa youtube.


na huu ndio mpangilio wa track list katika album yake ya QQJD volume1. titanic ni namba 11
View attachment 2306030View attachment 2306029
 
Fikiri Madinda, alikuwa ni dereva wa serikali pale Mifugo na uvuvi kwa sasa Temeke. shughuli yake kubwa ilikuwa ni kufunga mitambo ya bendi. alikuwa anafanya kazi ikifika saa tisa gari imeshapaki anaaga anakwenda kwenye kazi za bendi ambazo mara nyingi ilikuwa inaanza kutumbuiza mida ya jioni.
Uko sahihi miaka kadhaa nilikuwa nafanya kaz fulan baraza la vetenari tulikuwa tunakutana Sana pale canteen
 
Umemsahau Papaa Shabani Ngalawa (R.I.P). Huyu alikua mwalimu mzuri wa tution miaka ya 1995-2001 hizi za shule ya msingi. Miaka ambayo mtaa mzima unakuta waliofaulu la saba ni wawili au hakuna na katika hao waliofaulu wote walisoma tution kwa huyu mwalimu shabani..

Nakumbuka alichukuaga mkopo wa milioni 200 lengo likiwa kujenga shule yake binafsi maeneo ya kibamba. Akaweka rehani nyumba na shamba lake. Mwisho wa siku pesa zote zikaishia kuwatunza akina ally choki na mwinjuma muumini ktk mabendi na nyingine akanunulia toyota baloon. Benki ikaja ikapiga mnada nyumba na shamba wakamfilisi mazima.

Alitajwa sana kwenye nyimbo za Mwinjuma hasa ile ya Kilio cha Yatima. Alikuja kuugua mda mrefu na aliisha akawa kama mtoto. Amefariki akiwa hana hata pa kulala. Sad!
200M,aisee ..kumbe watu washakula bata, ni majuzi nimefyekekea 5M nikajiona mjinga..kumbe kuna viumbe washachafua sana hali ya hewa..aliondoka alivyokuja duniani.
 
umesahau kutaja jina la Alita Tchamala.
hili jina limekuwa likiimbwa na wanamuziki wakubwa wa drc tangu miaka ya 80.

hawa wa kizazi cha sasa akina ferre na fally ipupa halibanduki vinywani mwao, wanalitaja sana.

msikilize ferre gola hapa[emoji116][emoji116]
Alita | Boomplay Music

marehemu Josky Kiambukuta alilitaja sana hilo jina kwenye track yake iliyotoka mwaka 1983 yenye jina hilohilo la alita tchamala.


natamani kujua ni infuence kubwa kiasi gani anayo mtu huyu kwa wanamuziki wa drc kiasi cha jina lake kutajwa kwenye mashairi ya mziki tangu miaka ya 80.

mwenye data tafadhali ashushe hapa

Wanamuziki wa Congo kumtaja mtu huwa sababu kuu ni pesa. Bila kuwa na hela labda uwe ndugu yake. Mimi namfahamu Mike Mosisi ambaye katungiwa hadi wimbo na Koffi Olomide. Huyo jamaa ni mwanasiasa pia mfanyabiashara. Familia yake pale Lubumbashi wanaishi kifalme. Huwezi amini kama ndo DRC yenye maskini walioshindikana. Kuna mdogo wake sharobaro alikuwa akiagiza kitu Dar hajali kabisa kuhusu bei.
 
Huu wimbo wa kibinda nkoyi naupataje mkuu

Ikibinda nkoyi ni verse za kuchagizia wimbo aka rap za Allan Mulumba Kashama mstahiki Meya sio kua ninwimbo, tafuta nyimbo za Diamond Sound Banda utakuna na hizo rap.
 
Unaujua ule wimbo
Nimepoteza kipenzi changu hapa tanzaniaaa[emoji445]
Nimepoteza mkanda wa kiuono[emoji445]
Nitarudii kwa Hidayaa[emoji445] hidayaaa hidayaaa[emoji445]

Unaambiwa Hidaya alikua ni mrembo vibaya sana enzi za uhai wake akiwa kijana

Shikamo seye” wa Joseph Kabasele Yampanya aka Pepe Kalle
Hidaya ni mama Yetu wa A CITY !
 
Ni neno moja tu Hidaya na hedaya. Labda tusaidie huyo mtoto amezaa naye mwaka gani ili upewe full kisa ndipo ujue wabongo wanajua kuchangamkia fursa. Sikatai kwamba huyo Hidaya wa Pepe Kale kama mnavyomuita alikuwepo, ila kilichoimbwa kwenye wimbo sio Hidaya mwanamke. Ila wabongo kwa kuchangamkia fursa mko vizuri. Stori ndefu kidogo na muda hautoshi.

Hakuna wimbo unaitwa Hidaya
Wimbo unaitwa Shikamo Seye! Alafu Hidaya katajwa sasa humo ndani!
 
Back
Top Bottom